Ufunuo 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 8:1-13

Lakiri Ya Saba Na Chetezo Cha Dhahabu

18:1 Ufu 6:1Mwana-Kondoo alipoivunja ile lakiri ya saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.

28:2 Ufu 9:1, 13; 11:15; Mt 24:31; Ufu 8:6-13Nami nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.

38:3 Ufu 7:2; 5:8; Kut 30:1-6; Ebr 9:4Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi. 48:4 Za 141:2; Lk 1:10Ule moshi wa uvumba pamoja na yale maombi ya watakatifu, vikapanda juu mbele za Mungu, kutoka mkononi mwa huyo malaika. 58:5 Law 16:12-13; Ufu 4:5; 6:12Kisha yule malaika akachukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la ardhi.

Tarumbeta Ya Kwanza

68:6 Ufu 8:2Basi wale malaika saba waliokuwa na zile tarumbeta saba wakajiandaa kuzipiga.

78:7 Eze 38:22; Ufu 9:15-18; 12:4; 9:4Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, navyo vikatupwa kwa nguvu juu ya nchi. Na theluthi ya dunia ikateketea, theluthi ya miti ikateketea, na nyasi yote mbichi ikateketea.

Tarumbeta Ya Pili

88:8 Yer 51:25; 16:3Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu, 98:9 Ufu 8:7; 16:3theluthi ya viumbe vyenye uhai viishivyo baharini vikafa na theluthi ya meli zikaharibiwa.

Tarumbeta Ya Tatu

108:10 Isa 14:12; Ufu 9:1; 14:7; 16:4Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake, na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa ikaanguka toka angani, ikaangukia theluthi ya mito na chemchemi za maji. 118:11 Yer 9:15; 23:15Nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.

Tarumbeta Ya Nne

128:12 Kut 10:21-23; Ufu 6:12-13Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku.

138:13 Ufu 14:6; 19:17; 11:14; 12:12Nilipokuwa tena nikitazama, nikamsikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, akisema, “Ole! Ole! Ole wa watu waishio duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika hao wengine watatu wanakaribia kuzipiga!”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

啟示錄 8:1-13

揭開第七印

1羔羊揭開第七印時,天上寂靜無聲,約半小時。 2然後,我看見站在上帝面前的七位天使領受了七支號角。

3另一位天使手裡拿著金香爐上前來,站在祭壇旁邊。他接過了許多香,把香和眾聖徒的祈禱一起獻在寶座前的金壇上。 4這香冒出的煙,連同眾聖徒的禱告從那天使的手中向上升到上帝面前。 5天使又拿著香爐,盛滿祭壇的火,將它倒在地上,於是出現雷鳴、巨響、閃電和地震。

天使吹號

6這時,那七位拿著號角的天使也預備要吹號。

7第一位天使吹響了號角,有冰雹和火摻雜著血被拋到地上。地的三分之一、樹木的三分之一和一切青草都被燒毀了。

8第二位天使吹響了號角,有一座好像燃燒的大山被扔進海裡。海洋的三分之一變成了血, 9海中的活物死了三分之一,船隻也被毀了三分之一。

10第三位天使吹響了號角,有一顆好像火炬般燃燒著的巨星從天上墜落在三分之一的河流和水泉裡。 11這顆星名叫「苦艾」,它使三分之一的水都變苦了,許多人因為喝了這種苦水而死去。

12第四位天使吹響了號角,太陽、月亮和星辰的三分之一都受到重擊,以致失去了三分之一的光輝,於是日間的三分之一黯淡無光,夜間也是如此。 13我又看見有一隻鷹在半空中飛翔,聽見牠大聲宣告:「有禍了!有禍了!世上的居民有禍了!還有三位天使要吹響號角。」