Yuda 1 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Yuda 1:1-25

Salamu

11:1 Yn 14:22; Mdo 1:13; Rum 1:6, 7; Yn 17:12Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo na nduguye Yakobo:

Kwa wale walioitwa, wapendwa katika Mungu Baba na kuhifadhiwa salama ndani ya Yesu Kristo:

21:2 Rum 1:7; 2Pet 1:2Rehema, amani na upendo viwe kwenu kwa wingi.

Dhambi Na Hukumu Ya Watu Wasiomcha Mungu

31:3 Tit 1:4; 1Tim 6:12Wapendwa, ingawa nilikuwa ninatamani sana kuwaandikia kuhusu wokovu ambao tunaushiriki sisi sote, niliona imenipasa kuwaandikia na kuwasihi kwamba mwitetee imani iliyokabidhiwa watakatifu kwa nafasi moja itoshayo. 41:4 Gal 2:4; 2Pet 2:1; 1Yn 2:22Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri katikati yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu, wapotoshao neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi wakimkana yeye aliye Bwana wetu wa pekee, Bwana Yesu Kristo.

Hukumu Kwa Walimu Wa Uongo

51:5 Kum 1:32; 1Kor 10:1-5Ingawa mmekwisha kujua haya yote, nataka niwakumbushe kuwa Bwana akiisha kuwaokoa watu wake kutoka nchi ya Misri, baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini. 61:6 2Pet 2:4, 9; Mwa 6:1; Yn 8:44; Ufu 20:10Nao malaika ambao hawakulinda nafasi zao, lakini wakayaacha makao yao, hawa amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwa kwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu Siku ile kuu. 71:7 Kum 29:23; Mt 25:41; Mwa 19:24; 2Pet 2:6, 10; Mt 10:15Vivyo hivyo, Sodoma na Gomora na pia ile miji iliyokuwa kandokando, ambayo kwa jinsi moja na hao, walijifurahisha kwa uasherati na kufuata tamaa za mwili zisizo za asili, waliwekwa wawe mfano kwa kuadhibiwa katika moto wa milele.

81:8 2Pet 2:10; Kut 22:28Vivyo hivyo, hawa waotao ndoto huutia mwili unajisi, hukataa kuwa chini ya mamlaka na kunena mabaya juu ya wenye mamlaka. 91:9 Dan 12:1; Ufu 12:7; Zek 3:2Lakini hata malaika mkuu Mikaeli alipokuwa anashindana na ibilisi juu ya mwili wa Mose, hakuthubutu kumlaumu, bali alimwambia, “Bwana na akukemee!” 101:10 2Pet 2:12Lakini watu hawa hunena mabaya dhidi ya mambo wasiyoyafahamu. Na katika mambo yale wanayoyafahamu kwa hisia kama wanyama wasio na akili, hayo ndiyo hasa yanayowaharibu.

111:11 Mwa 4:3-8; 2Pet 2:15; Hes 16:1-3; 31:35Ole wao! Kwa kuwa wanaifuata njia ya Kaini, wamekimbilia faida katika kosa la Balaamu na kuangamia katika uasi wa Kora.

121:12 2Pet 2:13; 1Kor 11:20-22; Mit 25:14; 2Pet 2:17; Efe 4:14; Mt 15:13Watu hawa ni dosari katika karamu zenu za upendo, wakila pamoja nanyi bila hofu, wakijilisha pasipo hofu. Wao ni mawingu yasiyokuwa na maji, yakichukuliwa na upepo, miti isiyo na matunda wakati wa mapukutiko, ambayo hunyauka, iliyokufa mara mbili na kungʼolewa kabisa. 131:13 Isa 57:20; Flp 3:19; 2Pet 2:17Wao ni mawimbi makali ya bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba waliowekewa milele.

141:14 Mwa 5:18; 21:24; Kum 33:2; Dan 7:10Enoki, mtu wa saba kuanzia Adamu alitoa unabii kuhusu watu hawa, akisema: “Tazama, Bwana anakuja pamoja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake, 151:15 2Pet 2:6-9; 1Tim 1:9ili kumhukumu kila mmoja na kuwapatiliza wote wasiomcha Mungu kwa matendo yao yote ya uasi waliyoyatenda, pamoja na maneno yote ya kuchukiza ambayo wenye dhambi wamesema dhidi yake.” 161:16 2Pet 2:18; 2:10Watu hawa ni wenye kunungʼunika na wenye kutafuta makosa; wao hufuata tamaa zao mbaya, hujisifu kwa maneno makuu kuhusu wao wenyewe na kuwasifu mno watu wenye vyeo kwa ajili ya kujipatia faida.

Maonyo Na Mausia

171:17 2Pet 3:2; Efe 4:11; Ebr 2:3Lakini ninyi wapenzi, kumbukeni yale mitume wa Bwana Yesu Kristo waliyonena zamani. 181:18 1Tim 4:1; 2Pet 2:4Kwa kuwa waliwaambia, “Siku za mwisho kutakuwa na watu wenye kudhihaki, watakaofuata tamaa zao wenyewe za upotovu.” 191:19 1Kor 2:14, 15Hawa ndio watu wanaowagawa ninyi, wafuatao tamaa zao za asili, wala hawana Roho.

201:20 Kol 2:7; Efe 6:18Lakini ninyi wapendwa, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu. 211:21 Tit 2:13; 2Pet 3:12; Ebr 9:28; Mt 25:46Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia kwa furaha rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ili awalete katika uzima wa milele.

22Wahurumieni walio na mashaka; 231:23 Amo 4:11; Zek 3:2-5; Ufu 3:4wengine waokoeni kwa kuwanyakua kutoka kwenye moto; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili.

Dua Ya Kutakia Heri

241:24 Rum 16:25; 2Kor 4:14; Kol 1:22Kwake yeye awezaye kuwalinda ninyi msianguke na kuwaleta mbele za utukufu wake mkuu bila dosari na kwa furaha ipitayo kiasi: 251:25 Yn 5:44kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka ni vyake tangu milele, sasa na hata milele! Amen.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

猶大書 1:1-25

1我是耶穌基督的奴僕、雅各的兄弟猶大,現在寫信給蒙父上帝呼召和眷愛、並被耶穌基督看顧的人。

2願你們飽得憐憫、平安和慈愛!

捍衛真道

3親愛的弟兄姊妹,我一直迫切地想寫信跟你們談談我們所共享的救恩,但現在我覺得有必要寫信勸勉你們竭力護衛一次就完整地交給聖徒的真道。 4因為有些不敬虔的人偷偷地混進你們中間,以上帝的恩典作藉口放縱情慾,否認獨一的主宰——我們的主耶穌基督。聖經上早已記載,這樣的人必受到審判。

前車之鑑

5以下的事情,你們雖然都知道,但我還要再提醒你們:從前上帝1·5 「上帝」有些抄本作「主」。把祂的子民從埃及救出來,後來把其中不信的人滅絕了。 6至於不守本分、擅離領地的天使,上帝也用鎖鏈將他們永遠囚禁在幽暗裡,等候最後審判的大日子到來。 7此外,所多瑪蛾摩拉及其附近城鎮的人同樣因為荒淫無度、沉溺於變態的情慾而遭到永遠不滅之火的刑罰。這些事都成為我們的警戒。

假教師的惡行

8同樣,這些作夢的人玷污自己的身體,不服權柄,毀謗有尊榮的。 9當天使長米迦勒摩西的屍體跟魔鬼爭辯的時候,尚且不敢用毀謗的話譴責牠,只說:「願主責罰你!」 10但這些人對自己不懂的事也隨口毀謗,好像沒有理性的牲畜一樣憑本能行事,結果自取滅亡。 11他們有禍了!他們步了該隱的後塵,為牟利而重蹈巴蘭的謬誤,又像可拉一樣因叛逆而滅亡。 12這些人在你們的愛宴中是敗類1·12 「敗類」希臘文是「暗礁」或「污點」的意思。。他們肆無忌憚地吃喝,是只顧餵養自己的牧人;是沒有雨的雲,隨風飄蕩;是深秋不結果子的樹,被連根拔起,徹底枯死; 13是海中的狂濤,翻動著自己可恥的泡沫;是流蕩的星星,有幽幽黑暗永遠留給他們。

14亞當的第七代子孫以諾曾經針對這些人說預言:「看啊!主率領祂千萬的聖者一同降臨, 15要審判所有的人,按不虔不敬的罪人所行的一切不虔不敬之事和他們褻瀆上帝的話定他們的罪。」 16這些人滿腹牢騷,怨天尤人,放縱自己的邪情私慾。他們口出狂言,為了牟利極盡阿諛奉承之事。

牢記警告

17親愛的弟兄姊妹,要謹記主耶穌基督的使徒從前給你們的警告。 18他們曾對你們說:「末世必有不敬虔、好嘲諷的人放縱自己的邪情私慾。」 19這些人製造分裂,血氣用事,心中沒有聖靈。

20親愛的弟兄姊妹,你們要在至聖的真道上造就自己,在聖靈的引導下禱告, 21常在上帝的愛中,等候我們主耶穌基督施憐憫賜給你們永生。

22那些心存疑惑的人,你們要憐憫他們; 23有些人,你們要將他們從火中搶救出來;還有些人,你們要懷著畏懼的心憐憫他們,甚至要厭惡被他們的邪情私慾玷污的衣服。

祝頌

24-25願榮耀歸給我們的救主——獨一的上帝!祂能保守你們不失足犯罪,使你們無瑕無疵、歡歡喜喜地站在祂的榮耀面前。 願榮耀、威嚴、能力和權柄藉著我們的主耶穌基督都歸給祂,從萬世以前直到現今,一直到永永遠遠。阿們!