1 Petro 3 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Petro 3:1-22

Mafundisho Kwa Wake Na Waume

13:1 1Pet 2:18; Efe 5:22; 1Kor 7:16Kadhalika enyi wake, watiini waume zenu, ili kama kunao wasioamini lile neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno, 23:2 1Pet 2:12kwa kuuona utakatifu na uchaji wa Mungu katika maisha yenu. 33:3 Isa 3:18-23; 1Tim 2:9; 1Pet 3:4; Rum 7:22; Efe 3:16Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. 43:4 Za 45:13; Rum 2:29; 7:22; 2Kor 4:16Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu. 53:5 1Tim 5:5Kwa kuwa hivi ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu. Wao walikuwa ni watiifu kwa waume zao, 63:6 Mwa 18:12kama Sara alivyomtii mumewe Abrahamu, hata akamwita bwana. Ninyi ni watoto wa Sara kama mkitenda yaliyo mema, bila kuogopa jambo lolote.

73:7 Kol 3:19; 1Kor 7:3; Efe 5:25; Kol 3:10; 1Kor 12:23; 1The 4:14Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, nanyi wapeni heshima mkitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu, na kama warithi pamoja nanyi wa kipawa cha neema cha uzima, ili kusiwepo na chochote cha kuzuia maombi yenu.

Kuteseka Kwa Kutenda Mema

83:8 Rum 12:10; Efe 4:2Hatimaye, ninyi nyote kuweni na nia moja, wenye kuhurumiana, mkipendana kama ndugu, na mwe wasikitivu na wanyenyekevu. 93:9 Rum 12:17; 1The 5:15; 1Pet 2:21-23; Ebr 6:14Msilipe ovu kwa ovu, au jeuri kwa jeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloitiwa ili mpate kurithi baraka. 103:10 Za 34:12; Yak 1:26; 1Pet 2:1, 22; Ufu 14:5Kwa maana,

“Yeyote apendaye uzima

na kuona siku njema,

basi auzuie ulimi wake usinene mabaya,

na midomo yake isiseme hila.

113:11 Za 37:27; Isa 1:16, 17; 3Yn 11; Rum 12:8; 14:19Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema;

lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

123:12 Za 34:12-16; Yn 9:31; Yak 5:16Kwa maana macho ya Bwana

huwaelekea wenye haki,

na masikio yake yako makini

kusikiliza maombi yao.

Bali uso wa Bwana uko kinyume

na watendao maovu.”

Kuvumilia Mateso

133:13 Mit 16:7; Tit 2:14Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? 143:14 1Pet 4:15-16; Isa 8:12-14Lakini mmebarikiwa hata kama ikiwalazimu kuteseka kwa ajili ya haki. “Msiogope vitisho vyao, wala msiwe na wasiwasi.” 153:15 Kol 4:6Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, 163:16 Mdo 23:1; Ebr 13:18; 1Pet 2:12-15mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao.

173:17 1Pet 4:19; 2:20; 4:15-16Kwa maana ni afadhali kupata mateso kwa ajili ya kutenda mema, kama kuteseka huko ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu. 183:18 1Pet 2:21; Kol 1:22; 1Pet 4:1-6Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho. 193:19 1Pet 1:12; 4:6; Isa 42:7; 49:9; 61:1Baada ya kufanywa hai, alikwenda na kuzihubiria roho zilizokuwa kifungoni: 203:20 Mwa 6:3; Ebr 11:7roho hizo ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Noa, wakati wa kujenga safina, ambamo watu wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa ili wasiangamie kwa gharika. 213:21 Mdo 22:16; Tit 3:5Nayo maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi pia: si kwa kuondoa uchafu kwenye mwili, bali kama ahadi ya dhamiri safi kwa Mungu, kwa njia ya ufufuo wa Yesu Kristo. 223:22 Mk 16:19; Mt 28:18; Rum 8:38Yeye ameingia mbinguni na amekaa mkono wa kuume wa Mungu; nao malaika, mamlaka na nguvu zote wametiishwa chini yake.