1 Petro 2 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Petro 2:1-25

Jiwe Lililo Hai Na Watu Waliochaguliwa

12:1 Efe 4:22; Yak 4:11Kwa hiyo, wekeni mbali nanyi uovu wote na udanganyifu wote, unafiki, wivu na masingizio ya kila namna. 22:2 1Kor 3:2; Ebr 5:12-13; Efe 4:15-16Kama watoto wachanga, waliozaliwa sasa, yatamanini maziwa ya kiroho yasiyochanganywa na kitu kingine chochote, ili kwa hayo mpate kukua katika wokovu, 32:3 Za 34:8; Ebr 6:5ikiwa kweli mmeonja ya kwamba Bwana ni mwema.

42:4 Za 118:22; Mt 21:42; Mdo 4:11Mnapokuja kwake, yeye aliye Jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kwake, 52:5 Mit 9:1; Efe 2:20-22; 1Tim 3:15; Kut 19:6; Ufu 5:10; Ebr 13:15ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mnajengwa kuwa nyumba ya kiroho, ili mpate kuwa ukuhani mtakatifu, mkitoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. 62:6 Efe 2:20; Rum 10:11Kwa maana imeandikwa katika Maandiko:

“Tazama, naweka katika Sayuni,

jiwe la pembeni teule lenye thamani,

na yeyote atakayemwamini

hataaibika kamwe.”

72:7 2Kor 2:16; Mdo 4:11Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hili ni la thamani. Lakini kwao wasioamini,

“Jiwe walilolikataa waashi

limekuwa jiwe kuu la pembeni,”

82:8 Isa 8:14; 1Kor 1:23; Rum 9:22tena,

“Jiwe lenye kuwafanya watu wajikwae,

na mwamba wa kuwaangusha.”

Wanajikwaa kwa sababu hawakulitii lile neno, kama walivyowekewa tangu zamani.

92:9 1Sam 12:22; Kut 19:6; Mdo 26:18Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki ya Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. 102:10 Rum 9:25-26; Hos 1:9, 10; 2:23Mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni taifa la Mungu. Mwanzo mlikuwa hamjapata rehema, lakini sasa mmepata rehema.

112:11 Rum 13:14; Yak 4:1Wapenzi, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapitaji hapa ulimwenguni, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupigana vita na roho zenu. 122:12 Tit 2:8, 14; Mt 5:16; 9:8Kuweni na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasingizia kuwa watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema nao wamtukuze Mungu siku atakapokuja kwetu.

Kuwatii Wenye Mamlaka

132:13 Tit 3:1; Rum 13:1; Mt 22:21Kwa ajili ya Bwana, tiini kila mamlaka iliyowekwa na wanadamu: Kwa mfalme kwani ndiye aliye na mamlaka ya juu zaidi, 142:14 Rum 13:3-4au kwa maafisa aliowaweka, kwa kuwa mfalme amewatuma ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale watendao mema. 152:15 1Pet 3:17; 4:19Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema mnyamazishe maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 162:16 Yn 8:32; Rum 6:22Ishini kama watu huru, lakini msitumie uhuru wenu kama kisingizio cha kutenda uovu, bali ishini kama watumishi wa Mungu. 172:17 Rum 12:10; Mit 24:21; 1Pet 2:18; Efe 6:5; Yak 3:17Mheshimuni kila mtu ipasavyo: Wapendeni jamaa ya ndugu waumini, mcheni Mungu, mpeni heshima mfalme.

182:18 1Kor 6:20; 7:23; Eze 20:18; 1Pet 4:3Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu kwa heshima yote, si wale mabwana walio wema na wapole peke yao, bali pia wale walio wakali. 192:19 1Pet 3:14-17; Mt 5:10; Rum 13:5; 1Pet 3:14Kwa maana ni jambo la sifa kama mtu akivumilia anapoteswa kwa uonevu kwa ajili ya Mungu. 202:20 1Pet 3:14; 4:14, 15Kwani ni faida gani kwa mtu kustahimili anapopigwa kwa sababu ya makosa yake? Lakini kama mkiteswa kwa sababu ya kutenda mema, nanyi mkastahimili, hili ni jambo la kusifiwa mbele za Mungu.

Mfano Wa Mateso Ya Kristo

212:21 Flp 1:29; Mt 11:29Ninyi mliitwa kwa ajili ya haya, kwa sababu Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo, ili mzifuate nyayo zake.

222:22 Isa 53:7-9“Yeye hakutenda dhambi,

wala hila haikuonekana kinywani mwake.”

232:23 Lk 23:46Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutishia, bali alijikabidhi kwa yeye ahukumuye kwa haki. 242:24 Isa 53:4-11; Rum 6:2; Za 103:3; Ebr 12:13Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, ili tufe kwa mambo ya dhambi, bali tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa. 252:25 Isa 53:6; Yn 10:11Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmerudi kwa Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.