1 Petro 4 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

1 Petro 4:1-19

Kuishi Kwa Ajili Ya Mungu

14:1 1Pet 3:18; Rum 6:2, 7; Gal 5:24; Kol 3:3, 5Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni nia iyo hiyo kwa maana mtu aliyekwisha kuteswa katika mwili ameachana na dhambi. 24:2 Rum 6:2; 1Pet 1:14Kwa hivyo, haishi maisha yake yaliyobaki ya kuishi hapa duniani kwa tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi kwa mapenzi ya Mungu. 34:3 Efe 2:2; Eze 44:6; 45:9; Mdo 17:30; Efe 4:17; 1The 4:15Maana wakati uliopita mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu mkifanya yale ambayo wapagani hupenda kutenda: wakiishi katika uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulafi, vileo, ngoma mbaya, na ibada chukizo za sanamu. 44:4 1Pet 3:16; Mdo 13:45; 18:6; 1Pet 3:16Wao hushangaa kwamba ninyi hamjiingizi pamoja nao katika huo wingi wa maisha ya ufisadi, nao huwatukana ninyi. 54:5 Mdo 10:42; 2Tim 4:1Lakini itawapasa wao kutoa hesabu mbele zake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 64:6 1Pet 3:19Kwa kuwa hii ndiyo sababu Injili ilihubiriwa hata kwa wale waliokufa, ili wahukumiwe sawasawa na wanadamu wengine katika mwili, lakini katika roho waishi kulingana na Mungu aishivyo.

74:7 Rum 13:11; 1Pet 4:8Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo kuweni na akili tulivu na kiasi, mkikesha katika kuomba. 84:8 Ebr 13:1; Kol 3:14; Mit 10:12; 1Kor 13:7; Yak 5:20Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi. 94:9 Flp 2:14; 1Pet 4:10; Rum 12:6-7; 1Kor 4:2Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manungʼuniko. 104:10 Rum 12:6; 1Kor 4:7; Mt 24:45; Lk 12:42; 1Kor 4:1, 2Kila mmoja na atumie kipawa chochote alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu. 114:11 Efe 6:10; 1Kor 10:31Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.

Kuteseka Kwa Kuwa Mkristo

124:12 1Pet 1:6-7; 1Kor 3:13Wapenzi, msione ajabu kwa yale mateso yanayotukia miongoni mwenu, kana kwamba ni kitu kigeni kinachowapata. 134:13 Rum 8:17; 1Pet 4:14; Mt 5:11Bali furahini kuwa mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili mpate kufurahi zaidi wakati utukufu wake utakapofunuliwa. 144:14 Mt 5:11; 2Kor 12:10; Yak 1:12; 1Pet 2:19, 20Kama mkitukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu yenu. 154:15 Mdo 5:41; 1Pet 2:20; 1The 4:11; 1Tim 5:13Lakini asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu anayeteswa kwa kuwa ni muuaji, au mwizi, au mhalifu wa aina yoyote, au anayejishughulisha na mambo ya watu wengine. 164:16 Mdo 5:41Lakini kama ukiteseka kwa kuwa Mkristo, usihesabu jambo hilo kuwa ni aibu, bali mtukuze Mungu kwa sababu umeitwa kwa jina hilo. 174:17 Eze 9:6; 1Tim 3:15; 2The 1:8Kwa maana wakati umewadia wa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Basi kama ikianzia kwetu sisi, mwisho wa hao wasiotii Injili ya Mungu utakuwaje? 184:18 Mit 11:31; Lk 23:31Basi,

“Ikiwa ni vigumu kwa mwenye haki kuokoka,

itakuwaje kwa mtu asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?”

194:19 Za 31:5; Lk 23:46; 2Tim 1:12Kwa hiyo, wale wanaoteswa kulingana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu, huku wakizidi kutenda mema.