Zekaria 4 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 4:1-14

Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili

14:1 Dan 8:18; Yer 31:26Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizi wake. 24:2 Yer 1:13; Kut 25:31; Ufu 1:12; 4:5Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. 34:3 Ufu 11:4; Za 1:3Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.”

4Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?”

54:5 Zek 1:9Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?”

Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.”

64:6 1Nya 3:19; Ezr 5:2; 1Sam 2:9; 13:22; 1Fal 19:12; Neh 9:20; Dan 2:34; Isa 11:2-4Kisha akaniambia, “Hili ni neno la Bwana kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

74:7 Za 26:12; 118:22; Yer 51:25; 1Nya 15:28; Isa 40:3-4; Mt 21:21; Ezr 3:11“Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ”

8Kisha neno la Bwana likanijia: 94:9 Ezr 3:11; 6:15; Zek 2:9; 6:12; 1Kor 2:4“Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu.

104:10 Hag 2:23; Ezr 5:1; Neh 12:1; Ay 38:5; 2Nya 16:9; Ufu 5:6“Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli.

“(Hizi saba ni macho ya Bwana ambayo huzunguka duniani kote.)”

114:11 Ufu 11:4Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?”

12Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?”

13Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?”

Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.”

144:14 Kut 29:7; 40:15; Za 45:7; Isa 20:3; Dan 9:24-26Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

撒迦利亞書 4:1-14

金燈臺和橄欖樹

1那位與我說話的天使又來喚醒我,像喚醒睡覺的人一樣。 2他問我:「你看見了什麼?」

我說:「我看見一個純金的燈臺,燈台頂端有一個油碗,燈臺上有七盞燈,每盞燈有七個燈芯。 3燈臺旁邊有兩棵橄欖樹,左右各一棵。」 4我問與我說話的天使:「主啊,這是什麼意思?」 5他說:「你不知道嗎?」我說:「主啊,我不知道。」

6他對我說:「這是耶和華對所羅巴伯講的話。萬軍之耶和華說,『不靠權勢,不靠才能,乃靠我的靈。 7大山啊,你算什麼?你必在所羅巴伯面前化為平地。他必搬出那塊封殿頂的石頭,伴隨著歡呼聲:願恩典、恩典歸於這殿!』」

8耶和華對我說: 9所羅巴伯的手已經奠立這殿的根基,他的手也必完成這項工程。那時你便知道,是萬軍之耶和華差遣我到你們這裡來的。 10誰敢藐視這微不足道的日子?他們看見所羅巴伯手中拿著線錘時,就必歡喜。這七盞燈是耶和華遍察天下的眼睛。」

11我又問天使:「燈臺左右的兩棵橄欖樹是什麼意思?」 12然後我又問道:「流出金色橄欖油的兩個金管旁邊的兩根橄欖枝是什麼意思?」 13他說:「你不知道嗎?」我說:「主啊,我不知道。」 14他說:「這是侍立在天下之主旁邊的兩位受膏者。」