KITABU CHA NNE
(Zaburi 90–106)
Zaburi 90
Umilele Wa Mungu Na Udhaifu Wa Mwanadamu
Maombi ya Mose, mtu wa Mungu.
190:1 Kum 33:27; Efe 2:22; Ufu 21:3Bwana, wewe umekuwa makao yetu
katika vizazi vyote.
290:2 Ay 38:4, 5; 10:5; 15:7; Mwa 21:33; Isa 9:6; 57:15; Za 102:24-27; Mit 8:23-26Kabla ya kuzaliwa milima
au hujaumba dunia na ulimwengu,
wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
390:3 Mwa 2:7; 3:9; Ay 7:21; 34:15; 1Kor 15:47; Mhu 12:7Huwarudisha watu mavumbini,
ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”
490:4 Ebr 13:8; 2Pet 3:8; Ay 10:5Kwa maana kwako miaka elfu
ni kama siku moja iliyokwisha pita,
au kama kesha la usiku.
590:5 Mwa 19:15; Isa 40:6Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo,
nao ni kama majani machanga ya asubuhi:
690:6 Isa 40:6-8; Ay 14:2; Za 92:7ingawa asubuhi yanachipua,
ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka.
7Tumeangamizwa kwa hasira yako
na tumetishwa kwa ghadhabu yako.
890:8 2Kor 4:2; Efe 5:12; Ebr 4:13; 4:12, 13; Za 19:12; 50:21; Yer 16:17; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1Kor 4:5Umeyaweka maovu yetu mbele yako,
dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako.
990:9 Za 78:33Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako,
tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza.
1090:10 Isa 23:15, 17; 2Sam 19:35; Ay 5:7; 20:8; 34:15; Yer 25:11Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,
au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,
lakini yote ni ya shida na taabu,
nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
1190:11 Za 7:11; 76:7Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako?
Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa
kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako.
1290:12 Za 39:4; 139:16; Mit 16:9; 20:24; Kum 32:29Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,
ili tujipatie moyo wa hekima.
1390:13 Za 6:3; Kum 32:36Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini?
Wahurumie watumishi wako.
1490:14 Za 103:5; 107:9; 145:16, 19; 31:7; 77:8; 143:8Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma,
ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu,
kulingana na miaka tuliyotaabika.
1690:16 Za 44:1; Hab 3:2Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,
utukufu wako kwa watoto wao.
1790:17 Isa 26:12; 2The 2:16, 17Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu;
uzithibitishe kazi za mikono yetu:
naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu.