Yohana 16 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 16:1-33

116:1 Yn 15:18-27; Mt 11:16“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. 216:2 Yn 12:42; Isa 66:5; Ufu 6:9Watawatenga na masinagogi. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. 316:3 Yn 17:25; 1Yn 3:1Nao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. 416:4 Yn 14:29Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.

Kazi Ya Roho Mtakatifu

516:5 Yn 16:10, 17, 28; 7:33; 13:36; 14:5“Sasa mimi ninakwenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unakwenda wapi?’ 616:6 Yn 6:22; 14:1Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. 716:7 Yn 14:16, 26; 15:26Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, lakini nikienda nitamtuma kwenu. 816:8 1Kor 14:24; Ebr 4:12Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 916:9 Yn 15:22Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi, 1016:10 Rum 1:17; 1Pet 3:18kwa habari ya haki, kwa sababu ninakwenda kwa Baba, nanyi hamtaniona tena, 1116:11 Yn 12:31kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.

1216:12 1Kor 3:2“Bado ninayo mambo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa. 1316:13 Yn 14:17; Za 25:5Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo. 14Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi. 1516:15 Yn 17:10Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo yangu na kuwajulisha ninyi.

1616:16 Yn 7:33; 16:22; 14:18-24“Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona.”

Huzuni Itageuka Kuwa Furaha

1716:17 Yn 16:16; 16:5Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? Naye ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa Baba’?” 18Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Kitambo kidogo’? Hatuelewi hilo analosema.”

19Yesu akatambua kuwa walitaka kumuuliza juu ya hilo, hivyo akawaambia, “Je, mnaulizana nina maana gani niliposema, ‘Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona’? 2016:20 Mk 16:10; Yn 20:20Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 2116:21 Mik 4:9; 1The 5:3Mwanamke anapokuwa na utungu wa kuzaa huwa na maumivu kwa sababu saa yake imewadia. Lakini mtoto akiisha kuzaliwa, yule mwanamke husahau maumivu hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto ulimwenguni. 2216:22 Isa 60:14; Lk 24:41, 52; Yn 14:1, 27; Mdo 2:46; 13:52; 1Pet 1:8Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 2316:23 Mt 7:7; Yn 15:16Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, kama mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa. 2416:24 Yn 3:29; 15:11Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.

Amani Kwa Wanafunzi

2516:25 Yn 10:6“Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba. 2616:26 Yn 16:23, 24Siku hiyo mtaomba kwa Jina langu. Wala sitawaambia kwamba nitamwomba Baba kwa ajili yenu, 2716:27 Yn 14:21, 23kwa maana Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. 2816:28 Yn 5:10, 17; 13:3Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni, sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.”

2916:29 Yn 16:25Ndipo wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza waziwazi, wala si kwa mafumbo. 3016:30 1Fal 17:24; Yn 16:27; 13:3; 2:25Sasa tumejua kwamba wewe unajua mambo yote, wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa jambo hili tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”

31Yesu akawajibu, “Je, sasa mnaamini? 3216:32 Yn 16:2, 25; Mt 26:31; 26:56; Yn 8:16, 29Saa inakuja, naam, imekwisha kuwadia, mtakapotawanyika kila mmoja kwenda nyumbani kwake na kuniacha peke yangu. Lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yu pamoja nami. 3316:33 Yn 14:27; 15:18-21; 1Yn 5:4; Ufu 21:7Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

約翰福音 16:1-33

聖靈的工作

1「我把這些事告訴你們,以免你們背棄信仰。 2人們將把你們趕出會堂,時候將到,殺害你們的人還以為是在事奉上帝。 3他們這樣做,是因為他們根本不認識父,也不認識我。 4我把這些事提前告訴你們,是要叫你們到時候可以想起我曾跟你們講過這些事。我以前沒有告訴你們,那是因為我還跟你們在一起。

5「現在我要去差我來的父那裡,你們沒有人問我去哪裡。 6因為我把這些事告訴了你們,你們心裡充滿了憂愁。 7然而,我把實情告訴你們,我去對你們是有益的,因為如果我不去,護慰者就不會來,我去了就會派祂到你們這裡來。 8祂來了,必讓世人在罪、義和審判方面知罪。 9關於罪,是因為他們不信我; 10關於義,是因為我要去父那裡,你們再也看不到我了; 11關於審判,是因為這世界的王受了審判。

12「我還有許多事情要告訴你們,可是你們現在還不能承受。 13等到真理之靈來了,祂會引導你們進入一切真理。祂不憑自己說話,而是把祂所聽見的和有關將來的事告訴你們。 14祂也要把從我領受的指示你們,使我得榮耀。 15父的一切都是我的,所以我才說聖靈要把從我領受的指示你們。

轉憂為喜

16「不久,你們就見不到我了。再過不久,你們還會看見我。」

17幾個門徒彼此議論說:「祂說,『不久,你們就見不到我了,再過不久,你們還會看見我』,又說,『因為我要去父那裡』,這到底是什麼意思呢? 18祂說『不久』是什麼意思呢?我們真不明白祂在說什麼!」

19耶穌知道他們想問祂,就說:「我說,『不久,你們就見不到我了。再過不久,你們還會看見我。』你們在議論這話是什麼意思嗎? 20我實實在在地告訴你們,你們將痛哭、哀號,世人卻要歡喜;你們將憂愁,然而你們的憂愁將變為喜樂。 21婦人分娩時都會痛苦,但孩子生下來後,她就會因為這世界添了一個新生命而歡喜,忘掉了生產的劇痛。 22同樣,現在你們痛苦,但到我再見你們的時候,你們的心必歡喜,而且這份喜樂是誰也奪不去的。

23「到那一天,你們就什麼也不用問我了。我實實在在地告訴你們,你們奉我的名無論向父求什麼,祂都會賜給你們。 24你們從來沒有奉我的名求過什麼,你們現在求,就必得到,好使你們的喜樂滿溢。

勝過世界

25「我一直用比喻跟你們講這些事,不久,我就不再用比喻了,而是清楚地把父的事告訴你們。 26到那天,你們將要奉我的名祈求,我不是說我要為你們向父祈求。 27父愛你們,因為你們一直愛我,並且相信我來自上帝。 28我從父那裡來到這個世界,現在我要離開這個世界回到父那裡。」

29門徒說:「現在你直截了當地告訴我們,不再用比喻了。 30現在我們知道你無所不知,無需人問你什麼,因此我們相信你來自上帝。」

31耶穌說:「你們現在相信嗎? 32看啊!時候快到了,現在就是,你們將要分散,各自回家,只留下我一人。不過,我並非一人,因為父與我在一起。 33我把這些事告訴你們,是要叫你們在我裡面有平安。你們在世上會有苦難,但你們要放心,我已經勝過這個世界。」