Walawi 25 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 25:1-55

Mwaka Wa Sabato

(Kumbukumbu 15:1-11)

125:1 Kut 19:11Bwana akamwambia Mose katika Mlima Sinai, 225:2 Kut 23:10; Law 26:34-35; 2Nya 36:21“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili ya Bwana. 325:3 Kut 23:10; 25:4Kwa miaka sita mtapanda mazao katika mashamba yenu, nanyi kwa miaka sita mtaikata mizabibu yenu matawi na kuvuna mazao yake. 425:4 Law 26:35; 2Nya 36:21; Isa 36:16; 37:30Lakini mwaka wa saba nchi lazima iwe na Sabato ya mapumziko, Sabato kwa Bwana. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi. 525:5 2Fal 19:29; Mwa 40:10; Hes 6:3; 13:20; Kum 23:24; Neh 13:15; Isa 5:2; 37:30Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko. 6Chochote nchi itoacho katika mwaka wa Sabato kitakuwa chakula chenu wenyewe, watumishi wenu wa kiume na wa kike, mfanyakazi aliyeajiriwa, na mkazi wa muda anayeishi miongoni mwenu, 725:7 Kut 23:11vilevile malisho ya mifugo yenu na wanyama pori katika nchi yenu. Chochote nchi itakachozalisha kinaweza kuliwa.

Mwaka Wa Yubile

8“ ‘Hesabu Sabato saba za miaka, yaani miaka saba mara saba, ili Sabato saba za miaka utakuwa muda wa miaka arobaini na tisa. 925:9 Law 16:29; 23:24; Hes 10:8; Yos 6:4; Amu 3:27; 7:16; 1Sam 13:3; Isa 27:13; Zek 9:14; Kut 30:10Ndipo tarumbeta itapigwa kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho, piga tarumbeta katika nchi yako yote. 1025:10 Isa 61:1; Yer 34:8, 15, 17; Lk 4:19; Law 27:17, 21; Hes 36:4; Eze 46:17; Kut 20:2; Ezr 6:3; Gal 5:1Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni yubile25:10 Yubile ni baragumu iliopigwa kila mwaka wa hamsini; ni Sabato ya nchi ya kila mwaka wa hamsini uliokuwa mwaka wa ukombozi, yaani kuachia huru. kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake. 11Mwaka wa hamsini utakuwa yubile kwenu, msipande wala msivune kile kiotacho chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa. 12Kwa kuwa ni yubile, nayo itakuwa takatifu kwenu; mtakula tu kile kilichotoka moja kwa moja mashambani.

13“ ‘Katika huu Mwaka wa Yubile, kila mmoja atarudi kwenye mali yake mwenyewe.

1425:14 Law 19:13; 1Sam 12:3-4; 1Kor 6:8; Za 10:18; Mik 2:2“ ‘Ikiwa utauza ardhi kwa mmoja wa wazawa wa nchi yako, au ukinunua ardhi kutoka kwake, mmoja asimpunje mwingine. 1525:15 Law 27:18, 23Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kwa misingi ya hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye ataiuza kwako kwa misingi ya hesabu ya miaka iliyobaki kwa kuvuna mavuno. 16Miaka inapokuwa mingi, utaongeza bei, nayo miaka ikiwa michache, utapunguza bei, kwa sababu kile anachokuuzia kwa hakika ni hesabu ya mazao. 1725:17 Law 19:13, 14, 32; Ay 31:16; Mit 22:22; Yer 7:5-6; 21:12; 22:3; Zek 7:9-10; 1The 4:6; Mit 14:31; Eze 22:29Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

1825:18 Mwa 26:5; Law 26:4-5; Kum 12:10; 33:28; Ay 5:22; Za 4:8; Yer 23:6; 30:10; 32:37; 33:16; Eze 28:26; 34:25; 38:14“ ‘Fuateni amri zangu, mwe waangalifu kutii amri zangu, nanyi mtaishi salama katika nchi. 1925:19 Law 26:4; Kum 11:14; 28:12; Isa 55:10; Mt 6:25; Hes 11:4-13; 2Fal 6:15Kisha nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba na kuishi humo kwa salama. 20Mwaweza kuuliza, “Tutakula nini katika mwaka wa saba ikiwa hatutapanda wala kuvuna mazao yetu?” 2125:21 Kum 28:8-12; Za 133:3; 134:3; 147:13; Eze 44:30; Hag 2:19; Mal 3:10; Kut 16:5Nitawapelekeeni baraka ya pekee katika mwaka wa sita, kwamba nchi itazalisha mazao ya kutosha kwa miaka mitatu. 2225:22 Law 26:10; 2Fal 19:29; Yos 5:11Mnapopanda mwaka wa nane, mtakula mavuno ya miaka iliyopita. Pia mtaendelea kuyala mazao hayo hadi mvune mavuno ya mwaka wa tisa.

2325:23 Hes 36:7; 1Fal 21:3; Eze 46:18; Kut 19:5; Mwa 23:4; Ebr 11:13“ ‘Kamwe ardhi isiuzwe kwa mkataba wa kudumu, kwa sababu nchi ni mali yangu, nanyi ni wageni na wapangaji wangu. 2425:24 Rut 4:7; Yer 32:8Katika nchi yote mtakayoshika kuwa milki yenu, ni lazima mtoe ukombozi wa ardhi.

2525:25 Rut 2:20; 4:4; Yer 32:7; Law 27:13-31“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini na akauza baadhi ya mali yake, ndugu yake wa karibu atakuja na kukomboa kile ndugu yako alichokiuza. 26Iwapo mtu huyo hana jamaa wa karibu wa kukomboa mali hiyo kwa ajili yake, lakini yeye mwenyewe akafanikiwa na kupata mali itoshayo kuikomboa, 27ataamua tena thamani yake kwa miaka tangu alipoiuza, na kurudisha kiasi kilichobaki cha thamani kwa mtu ambaye alikuwa amemuuzia mali hiyo, naye ataweza kuirudia mali yake. 28Lakini kama hatapata njia ya kumlipa mnunuzi, ile mali aliyouza itabaki kumilikiwa na mnunuzi mpaka Mwaka wa Yubile. Mali hiyo itarudishwa mwaka wa Yubile, naye ataweza kuirudia mali yake.

29“ ‘Ikiwa mtu atauza nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta, yeye anayo haki ya kuikomboa mwaka mzima baada ya mauzo ya hiyo nyumba. Wakati huo anaweza kuikomboa. 30Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa mwaka wa Yubile. 31Lakini nyumba zilizo vijijini bila ya kuwa na kuta zilizozizunguka zitahesabiwa kama mashamba. Zinaweza kukombolewa, nazo zirudishwe katika mwaka wa Yubile.

3225:32 Hes 35:1-8; Yos 21:2“ ‘Walawi siku zote wana haki ya kukomboa nyumba zao katika miji ya Walawi wanayoimiliki. 33Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wowote wanaoushikilia itarudishwa mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli. 3425:34 Hes 35:2-5; Eze 48:14; Mdo 4:36Lakini nchi ya malisho iliyo mali ya miji yao kamwe isiuzwe, ni milki yao ya kudumu.

3525:35 Kum 24:14-15; 15:8; Za 37:21-26; Mit 21:26; Lk 6:35; Mdo 11:29; Rum 12:18; 1Yn 3:17; Kum 15:7“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie kama vile ambavyo ungelimsaidia mgeni au kama mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi katikati yako. 3625:36 Kut 22:25; Yer 15:10; Law 19:32; Kum 23:19; Neh 5:7; Za 15:5; Mit 28:8; Eze 18:8Usichukue riba wala faida yoyote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi katikati yako. 3725:37 Kut 22:25Usimkopeshe fedha ili alipe na riba, wala usimuuzie chakula kwa faida. 3825:38 Mwa 10:19; 17:7; Law 11:45Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekuleta kutoka nchi ya Misri nikupe nchi ya Kanaani, nami niwe Mungu wako.

3925:39 1Fal 5:13; 9:23; Yer 34:14; Kut 21:2; 22:3; Kum 15:12“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini katikati yako, naye akajiuza kwako, usimfanye atumike kama mtumwa. 40Atatendewa kama mfanyakazi aliyeajiriwa, au kama mkazi wa muda katikati yako, naye atatumika mpaka Mwaka wa Yubile. 41Ndipo yeye na watoto wake wataachiwa, naye atarudi kwa watu wa ukoo wake, na kwenye mali ya baba zake. 4225:42 Rum 6:22; 1Kor 7:23Kwa sababu Waisraeli ni watumishi wangu niliowaleta kutoka nchi ya Misri, kamwe wasiuzwe kama watumwa. 4325:43 Kut 1:13; Eze 34:4; Kol 4:1; Mwa 42:18; Isa 47:6; Efe 6:9; Kum 25:18; Mal 3:5Usiwatawale kwa ukatili, lakini utamcha Mungu wako.

44“ ‘Watumwa wako wa kiume na wa kike watatoka katika mataifa yanayokuzunguka; kutoka kwao waweza kununua watumwa. 45Pia waweza kununua baadhi ya wakazi wa muda wanaoishi katikati yako, na jamaa ya koo zao waliozaliwa katika nchi yako, nao watakuwa mali yako. 46Hao waweza kuwarithisha watoto wako kuwa urithi wao, na wanaweza kuwafanya watumwa maisha yao yote, lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili.

4725:47 Neh 5:5; Ay 24:9“ ‘Ikiwa mgeni au mkazi wa muda katikati yako atakuwa tajiri, na mmoja wa wazawa wa nchi yako akawa maskini, naye akajiuza kwa yule mgeni anayeishi katikati yako, au kwa mmoja wa jamaa wa koo za wageni, 48anayo haki ya kukombolewa baada ya kujiuza. Mmoja wa jamaa zake aweza kumkomboa: 49Mjomba wake, au binamu yake, au yeyote aliye ndugu wa damu katika ukoo wake aweza kumkomboa. Au ikiwa atafanikiwa, anaweza kujikomboa mwenyewe. 5025:50 Ay 7:1; 14:6; Isa 16:14; 21:16Yeye na huyo aliyemnunua watahesabu muda kuanzia mwaka aliojiuza hadi Mwaka wa Yubile. Mahali pa kuanzia bei ya kuachiwa kwake itakadiriwa kwa ujira unaolipwa mfanyakazi aliyeajiriwa kwa idadi ya hiyo miaka. 51Ikiwa imebaki miaka mingi, ni lazima atalipia ukombozi wake fungu kubwa la bei iliyolipwa kumnunua yeye. 52Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake, naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake. 5325:53 Kol 4:1Atatendewa kama mtu wa kuajiriwa mwaka hadi mwaka; lazima uone kwamba yule aliyemnunua hamtawali kwa ukatili.

54“ ‘Hata ikiwa hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, yeye na watoto wake wataachiwa katika Mwaka wa Yubile, 5525:55 Law 11:44-45kwa maana Waisraeli ni mali yangu kama watumishi. Wao ni watumishi wangu, niliowatoa kutoka nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

利未記 25:1-55

安息年的條例

1耶和華在西奈山上對摩西說: 2「你要告訴以色列人:你們到了我將要賜給你們的土地後,要讓土地在耶和華面前守安息。 3六年之內,你們可以耕種田地,修整葡萄園,收穫出產。 4但第七年是要向耶和華守的安息年,土地要完全休息。你們不可耕種,不可修整葡萄園。 5不可收割自生自長的莊稼,也不可摘未經修剪而結的葡萄。這一年土地要完全休耕。 6但安息年間土地裡自生自長的,你們和你們的僕婢、雇工與住在你們中間的外族人都可以吃, 7你們的牲畜和境內的野獸也可以吃。

禧年的條例

8「你們要計算七個安息年,即七個七年,共四十九年。 9第五十年的七月十日贖罪日那天,你們要在境內各地吹號。 10你們要以這一年為聖年,向境內所有居民宣告自由。這一年將成為你們的禧年。你們要各歸祖業,各回本家。 11第五十年是你們的禧年。這一年你們不可耕種,不可收割自生自長的莊稼,也不可摘未經修剪而結的葡萄。 12這是禧年,是你們的聖年,你們可以吃土地裡自生自長的。 13在禧年,各人要回到祖業。 14因此,你們和同胞買賣田地時,不可彼此虧負。 15買賣雙方要按照距下個禧年的年數和收成的年數定價。 16距下個禧年的年數多,價錢就高;年數少,價錢就低。因為賣的是田地收成的次數。 17要敬畏你們的上帝,不可彼此虧負。我是你們的上帝耶和華。 18你們要遵行我的律例,持守我的典章,就可以在那片土地上安居。 19土地會出產豐富,使你們豐衣足食、安然居住。 20你們可能會問,『第七年不種不收,我們吃什麼?』 21我要在第六年賜福給你們,使田地的出產夠你們吃三年。 22第八年開始耕種時,你們仍會吃陳糧,一直吃到第九年的收割季節。

贖回土地的條例

23「你們不可永遠賣掉土地,因為土地是我的,你們只不過是寄居在那片土地上的過客。 24你們購買每一塊土地時,都必須讓原主保留贖回的權利。 25如果有人因貧窮而賣掉土地,他的近親要把賣掉的土地贖回來。 26如果無人為他贖回,而他自己漸漸富裕起來,有能力贖回, 27他要計算賣掉土地的年數,退還距下個禧年所剩年數的地價,便可以贖回自己的土地。 28如果他沒有能力贖回,所賣的土地在禧年之前要屬於買主。到了禧年,買主必須把土地歸還原主。

贖回房屋的條例

29「如果有人賣掉自己城裡的房子,要保留一年贖回權。賣掉房子的一年之內,他可以贖回。 30如果一年之內他沒有贖回,房子便永遠歸買主所有,就是到了禧年也不用歸還。 31如果房子在四圍無牆的鄉村,要視房子為鄉下的土地,原主可以贖回;到了禧年,買主必須將房子歸還。 32利未人的城邑裡,利未人永遠有權贖回所賣的房子。 33如果他們沒有贖回,到了禧年要把房子歸還他們,因為在利未人的城裡,利未人的房屋是他們在以色列人中所擁有的產業。 34但不可出賣利未人城郊的草場,那是他們永遠擁有的產業。

照顧同胞的條例

35「如果你們的同胞生活日益貧窮,難以維生,你們要像照顧外族人和寄居者一樣照顧他的生活,讓他住在你們當中。 36不可向他放債取利,要敬畏你們的上帝,讓他住在你們當中。 37你們借錢給他,不可收取利息;借糧給他,不可謀利。 38我是你們的上帝耶和華。我曾經帶領你們離開埃及,為要把迦南賜給你們,並做你們的上帝。

買賣奴隸的條例

39「如果你們的同胞窮得把自己賣給你們,不可把他當作奴隸, 40要待他像雇工和寄居者一樣。他要為你工作到禧年。 41到了禧年,他和孩子們便可以離開你們,回到自己的宗族和祖業。 42因為以色列人是我的僕人,是我從埃及帶出來的,所以他們不可賣身為奴。 43你們也不可苛待他們,要敬畏你們的上帝。 44你們可以從鄰國購買奴隸, 45也可以買居住或出生在你們境內的外族人。這些人可以作你們的產業。 46你們可以將他們作為產業傳給你們的子孫,使他們終身做奴隸。但你們不可苛待自己的同胞。

47「如果你們中間的外族人漸漸富裕,你們同胞中卻有人日益貧窮,把自己賣給外族人或他們的族人, 48他可以保留贖身的權利。他的兄弟、 49叔伯、堂兄弟或其他近親都可以贖回他。如果他富裕起來,也可以贖回自己。 50他要和買主計算從自己賣身為奴到下個禧年之間的年數,然後按雇工的工價,照年數計算贖價。 51如果離禧年還有很多年,他就要按年數和當初賣價的比例償還贖價。 52如果離禧年只有不多的幾年,他就要按年數償還贖身費。 53買主要待他如按年雇用的工人。你們要確保買主不會苛待他。 54如果禧年來臨前他沒有被贖回,到了禧年他和孩子們都要獲得自由。 55因為以色列人是我的僕人,是我從埃及領出來的僕人。我是你們的上帝耶和華。