Wagalatia 2 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version

Wagalatia 2:1-21

Paulo Akubaliwa Na Mitume

12:1 Mdo 15:2; 4:36; 2Kor 2:13Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nilipanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito ili awe pamoja nami. 22:2 Mdo 15:4; 12; 1Kor 9:24; Flp 2:16Nilikwenda kwa sababu nilikuwa nimefunuliwa na Mungu, ili nikawaeleze kwa faragha wale walioonekana kuwa viongozi, ile Injili ninayoihubiri kwa watu wa Mataifa. Nilifanya hivyo kwa kuhofia kwamba nisije nikawa nilikuwa ninakimbia au nilikimbia bure. 32:3 2Kor 2:13; Mdo 16:3; 1Kor 9:21Lakini hata Tito ambaye alikuwa Myunani, hakulazimika kutahiriwa. 42:4 2Kor 11:26; Yud 24; Mdo 15:1; Gal 5:1, 13Lakini kwa sababu ya ndugu wa uongo ambao walijiingiza kwa siri katikati yetu ili kupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, wapate kututia utumwani, 52:5 Gal 2:14; 3:1; 4:16hatukukubaliana nao hata dakika moja, ili kwamba ukweli wa Injili ubaki nanyi.

62:6 Gal 6:3; Mdo 10:34Kwa habari ya wale waliokuwa wakubaliwe kuwa viongozi (kwangu mimi sikujali vyeo vyao, maana Mungu hana upendeleo), wale watu hawakuniongezea chochote. 72:7 1The 2:4; 1Tim 1:11; Mdo 9:15Badala yake walitambua kwamba nilikuwa nimekabidhiwa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa Mataifa, kama vile Petro alivyokabidhiwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi. 82:8 Mdo 1:25; 1Kor 1:1; Mdo 9:15; 13:2; 22:21Kwa maana, Mungu aliyekuwa akitenda kazi katika huduma ya Petro kama mtume kwa Wayahudi, ndiye pia aliyekuwa anatenda kazi katika huduma yangu kama mtume kwa watu wa Mataifa. 92:9 1Tim 3:15; Mdo 4:36; Rum 12:3; Mdo 15:13; Gal 2:7, 11, 14; 1Tim 3:15; Ufu 3:12Basi, Yakobo, Kefa2:9 Yaani Petro, pia mstari 11, 14. na Yohana, walioonekana kama nguzo za kanisa, walitupa mkono wa shirika, mimi na Barnaba walipotambua ile neema niliyopewa. Wakakubali kwamba sisi twende kwa watu wa Mataifa na wao waende kwa Wayahudi. 102:10 Mdo 24:17; 11:30; 12:25; Rum 15:25; 1Kor 16:1; 2Kor 8:9Walichotuomba ni kwamba tuendelee kuwakumbuka maskini, jambo ambalo ndilo nililokuwa na shauku ya kulifanya.

Paulo Ampinga Petro Huko Antiokia

112:11 Mdo 11:19; 15:35Lakini Petro alipofika Antiokia, mimi nilimpinga ana kwa ana kwa sababu alikuwa amekosea kwa wazi. 122:12 Mdo 11:2-3Kabla baadhi ya watu waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa. Lakini hao watu walipofika alianza kujiondoa na kujitenga na watu wa Mataifa kwa sababu aliwaogopa wale wa kundi la tohara. 132:13 Mdo 4:36Pia Wayahudi wengine waliungana naye katika unafiki huu, hata Barnaba naye akapotoshwa na unafiki wao.

142:14 Mdo 10:28; 1Tim 5:20; Mdo 11:3Nilipoona kwamba hawatendi sawasawa na kweli ya Injili, nilimwambia Petro mbele ya wote, “Wewe ni Myahudi, nawe unaishi kama mtu wa Mataifa na wala si kama Myahudi. Imekuwaje basi, mnawalazimisha watu wa Mataifa kufuata desturi za Kiyahudi?

Wayahudi Na Watu Wa Mataifa Wanaokolewa Kwa Imani

152:15 Flp 3:4-5; 1Sam 15:18“Sisi wenyewe ni Wayahudi kwa kuzaliwa na si watu wenye dhambi kama watu wa Mataifa, 162:16 Mdo 13:39; Rum 9:30bado tunajua ya kwamba mtu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Hivyo sisi pia, tumemwamini Kristo Yesu ili tupate kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Kristo, wala si kwa matendo ya sheria, kwa sababu kwa kushika sheria hakuna hata mtu mmoja atakayehesabiwa haki.

172:17 Gal 3:21“Lakini tukitafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, inakuwa dhahiri kwamba sisi ni wenye dhambi. Je, ina maana kwamba Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha! 18Lakini ikiwa mimi ninajenga tena kile ambacho nimekwisha kukibomoa, basi ninaonyesha kwamba mimi ni mkosaji. 192:19 Rum 7:4; 6:10-14; 2Kor 5:15Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. 202:20 Rum 6:6; 1Pet 4:2; Mt 4:3; Rum 8:37; Gal 1:4Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi, bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu. 212:21 Gal 3:21Siibatilishi neema ya Mungu, kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure!”

New International Version

Galatians 2:1-21

Paul Accepted by the Apostles

1Then after fourteen years, I went up again to Jerusalem, this time with Barnabas. I took Titus along also. 2I went in response to a revelation and, meeting privately with those esteemed as leaders, I presented to them the gospel that I preach among the Gentiles. I wanted to be sure I was not running and had not been running my race in vain. 3Yet not even Titus, who was with me, was compelled to be circumcised, even though he was a Greek. 4This matter arose because some false believers had infiltrated our ranks to spy on the freedom we have in Christ Jesus and to make us slaves. 5We did not give in to them for a moment, so that the truth of the gospel might be preserved for you.

6As for those who were held in high esteem—whatever they were makes no difference to me; God does not show favoritism—they added nothing to my message. 7On the contrary, they recognized that I had been entrusted with the task of preaching the gospel to the uncircumcised,2:7 That is, Gentiles just as Peter had been to the circumcised.2:7 That is, Jews; also in verses 8 and 9 8For God, who was at work in Peter as an apostle to the circumcised, was also at work in me as an apostle to the Gentiles. 9James, Cephas2:9 That is, Peter; also in verses 11 and 14 and John, those esteemed as pillars, gave me and Barnabas the right hand of fellowship when they recognized the grace given to me. They agreed that we should go to the Gentiles, and they to the circumcised. 10All they asked was that we should continue to remember the poor, the very thing I had been eager to do all along.

Paul Opposes Cephas

11When Cephas came to Antioch, I opposed him to his face, because he stood condemned. 12For before certain men came from James, he used to eat with the Gentiles. But when they arrived, he began to draw back and separate himself from the Gentiles because he was afraid of those who belonged to the circumcision group. 13The other Jews joined him in his hypocrisy, so that by their hypocrisy even Barnabas was led astray.

14When I saw that they were not acting in line with the truth of the gospel, I said to Cephas in front of them all, “You are a Jew, yet you live like a Gentile and not like a Jew. How is it, then, that you force Gentiles to follow Jewish customs?

15“We who are Jews by birth and not sinful Gentiles 16know that a person is not justified by the works of the law, but by faith in Jesus Christ. So we, too, have put our faith in Christ Jesus that we may be justified by faith in2:16 Or but through the faithfulness of… justified on the basis of the faithfulness of Christ and not by the works of the law, because by the works of the law no one will be justified.

17“But if, in seeking to be justified in Christ, we Jews find ourselves also among the sinners, doesn’t that mean that Christ promotes sin? Absolutely not! 18If I rebuild what I destroyed, then I really would be a lawbreaker.

19“For through the law I died to the law so that I might live for God. 20I have been crucified with Christ and I no longer live, but Christ lives in me. The life I now live in the body, I live by faith in the Son of God, who loved me and gave himself for me. 21I do not set aside the grace of God, for if righteousness could be gained through the law, Christ died for nothing!”2:21 Some interpreters end the quotation after verse 14.