Wafilipi 1 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wafilipi 1:1-30

Salamu

11:1 Mdo 16:1; 2Kor 1:1; Mdo 9:13; 16:12; 1Tim 3:1; 3:8Waraka wa Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu:

Kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu walioko Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi:

21:2 Rum 1:7; 1Kor 1:2; 1Pet 1:2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

Shukrani Na Maombi

31:3 Rum 1:8; 1Kor 1:6, 8; Efe 1:15, 16; 1Kor 1:4; Kol 1:3; 1The 1:2Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. 41:4 Rum 1:10Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, 51:5 Mdo 2:42; Flp 4:15; Mdo 16:12-40kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. 61:6 Flp 2:13; 1Kor 16:8; Za 138:8Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Kristo Yesu.

71:7 2Pet 1:13; 2Kor 7:3; Flp 1:13, 14, 17; Mdo 21:33Ni haki na ni wajibu wangu kufikiri hivi juu yenu nyote, kwa sababu ninyi mko moyoni mwangu. Ikiwa nimefungwa au nikiwa ninaitetea na kuithibitisha Injili, ninyi nyote mnashiriki neema ya Mungu pamoja nami. 81:8 Rum 1:9; 2Kor 1:23; 1The 2:5Mungu ni shahidi wangu jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote kwa huruma ya Kristo Yesu.

91:9 1The 3:12Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, 101:10 1Kor 1:8; Rum 2:18; Efe 5:10; Mdo 24:16; 1The 3:13; 5:23ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo, 111:11 Yak 3:18; Yn 15:4; Efe 2:10; Kol 1:16; Yn 15:8; Efe 1:12, 14mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu.

Kufungwa Kwa Paulo Kwaieneza Injili

121:12 2Tim 2:9Basi, ndugu zangu, nataka mjue kwamba mambo yale yaliyonipata kwa kweli yamesaidia sana kueneza Injili. 131:13 Mdo 21:33Matokeo yake ni kwamba imejulikana wazi kwa walinzi wote wa jumba la kifalme na kwa wengine wote kuwa nimefungwa kwa ajili ya Kristo. 141:14 Mdo 21:33Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga.

151:15 Flp 2:3Ni kweli kwamba wengine wanamhubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana, lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema. 161:16 Flp 1:7, 12Hawa wa mwisho wanamhubiri Kristo kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba nimo humu gerezani kwa ajili ya kuitetea Injili. 171:17 Flp 2:3; Mdo 21:33Hao wa kwanza wanamtangaza Kristo kutokana na tamaa zao wenyewe wala si kwa moyo mweupe, bali wanakusudia kuongeza mateso yangu katika huku kufungwa kwangu. 181:18 Flp 2:17, 18Lakini inadhuru nini? Jambo la muhimu ni kwamba kwa kila njia, ikiwa ni kwa nia mbaya au njema, Kristo anahubiriwa. Nami kwa ajili ya jambo hilo ninafurahi.

Naam, nami nitaendelea kufurahi, 191:19 2Kor 1:11; Mdo 16:7; 16:23kwa maana ninajua kwamba kwa maombi yenu na kwa msaada unaotolewa na Roho wa Yesu Kristo, yale yaliyonipata mimi yatageuka kuwa wokovu wangu. 201:20 Rum 8:19; 1Kor 6:20; Rum 14:8Ninatarajia kwa shauku kubwa na kutumaini kwamba sitaaibika kwa njia yoyote, bali nitakuwa na ujasiri wa kutosha ili sasa kama wakati mwingine wowote, Kristo atukuzwe katika mwili wangu, ikiwa ni kwa kuishi au kwa kufa. 211:21 Gal 2:20Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. 221:22 Rum 1:13Kama nitaendelea kuishi katika mwili, kwangu hili ni kwa ajili ya matunda ya kazi. Lakini sijui nichague lipi? Mimi sijui! 231:23 2Tim 4:6; Yn 12:26; 2Kor 5:8Ninavutwa kati ya mambo mawili: Ninatamani kuondoka nikakae pamoja na Kristo, jambo hilo ni bora zaidi. 24Lakini kwa sababu yenu ni muhimu zaidi mimi nikiendelea kuishi katika mwili. 251:25 Flp 2:24Kwa kuwa nina matumaini haya, ninajua kwamba nitaendelea kuwepo na kuwa pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani. 261:26 2Kor 1:14; 5:12Ili kwamba furaha yenu iwe nyingi katika Kristo Yesu kwa ajili yangu kwa kule kuja kwangu kwenu tena.

Kuenenda Ipasavyo Injili

271:27 Efe 4:1; 1Kor 16:13; Yud 3Lakini lolote litakalotukia, mwenende kama ipasavyo Injili ya Kristo, ili kwamba nikija na kuwaona au ikiwa sipo, nipate kusikia haya juu yenu: Kuwa mnasimama imara katika roho moja, mkiishindania imani ya Injili kwa umoja, 281:28 2The 1:5; Rum 8:17; 2Tim 2:11wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa, na hii ni kazi ya Mungu. 291:29 Mt 5:11, 12; Mdo 5:41; 14:22Kwa maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali pia kuteswa kwa ajili yake, 301:30 Kol 2:1; Ebr 10:32; Mdo 16:19-40kwa kuwa mnashiriki mashindano yale yale mliyoyaona nikiwa nayo na ambayo hata sasa mnasikia kuwa bado ninayo.