Wokovu Mkuu
12:1 Rum 11:22Kwa hiyo, imetupasa kuwa waangalifu sana kuhusu kile tulichosikia, ili tusije tukakiacha. 22:2 Ebr 1:1; Kum 33:2; Mdo 7:53; Gal 3:19; Ebr 10:28Kwa kuwa kama ujumbe ulionenwa na malaika ulikuwa imara, na kila uasi na kutokutii kulipata adhabu ya haki, 32:3 Ebr 10:29; 12:25; 1:2; Lk 1:2je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana, ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia. 42:4 Mk 16:20; Yn 4:48; 1Kor 12:4; Efe 1:5Pia Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake.
Yesu Alifananishwa Na Ndugu Zake
52:5 Ebr 6:5; 2Pet 3:13Mungu hakuuweka ulimwengu ujao ambao tunanena habari zake chini ya malaika. 62:6 Ebr 4:4; Ay 7:17; Za 144:3; 8:4-6Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema:
“Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,
binadamu ni nani hata unamjali?
7Umemfanya chini kidogo kuliko malaika;
ukamvika taji ya utukufu na heshima,
82:8 Za 8:4-6; Mt 22:44; 28:18; 1Kor 15:27; Efe 1:22; Ebr 1:13; 1Kor 15:2nawe umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.”
Kwa kuweka vitu vyote chini yake, Mungu hakuacha kitu chochote ambacho hakukiweka chini ya mwanadamu. Lakini kwa sasa, hatuoni kwamba kila kitu kiko chini yake. 92:9 Ebr 2:7; Mdo 3:13; Flp 2:7-9; 2Kor 5:15; Mdo 2:33; Yn 3:16; 12:32; Rum 5:18; 8:32; 2Kor 5:15; 1Tim 2:6; 1Yn 2:2; Ufu 5:9Lakini twamwona Yesu, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.
102:10 Rum 11:36; Lk 24:26; Ebr 5:8, 9; 7:28; Lk 24:46; Mdo 3:15; 5:31; Ebr 12:2; Lk 13:32; Ebr 5:9Ili kuwaleta wana wengi katika utukufu, ilifaa kwamba Mungu, ambaye ni kwa ajili yake na kupitia kwake kila kitu kimekuwepo, amkamilishe mwanzilishi wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 112:11 Ebr 10:10; Mdo 17:26; Mt 28:10; Yn 20:17; Rum 8:29; Efe 5:26; Ebr 13:12Yeye awafanyaye watu kuwa watakatifu, pamoja na hao ambao hufanywa watakatifu, wote hutoka katika jamaa moja. Hivyo Yesu haoni aibu kuwaita ndugu zake. 122:12 Za 22:22, 25; 68:26Yeye husema,
“Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu;
mbele ya kusanyiko nitaimba sifa zako.”
132:13 Isa 8:17, 18; Yn 10:29; Za 18:2; Isa 12:2; Yn 20:17; 17:6, 9, 11, 12Tena,
“Nitaweka tumaini langu kwake.”
Tena anasema,
“Niko hapa, pamoja na watoto ambao Mungu amenipa.”
142:14 Yn 1:14; Rum 8:3Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi, 152:15 2Tim 1:7; Lk 1:74; Rum 8:15na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti. 162:16 Isa 41:8, 9; Lk 3:8Kwa kuwa ni dhahiri kwamba hakuja kusaidia malaika, bali uzao wa Abrahamu. 172:17 Ebr 2:14; 5:1; 5:2; 3:1; 4:14, 15; Flp 2:7; Rum 3:25; Za 22:22Kwa sababu hii ilibidi afanane na ndugu zake kwa kila hali, ili apate kuwa Kuhani Mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika kumtumikia Mungu, ili pia apate kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu. 182:18 Ebr 4:15, 16; 5:2; 7:2; 4:15Kwa kuwa yeye mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wale wanaojaribiwa.