Isaya 60 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 60:1-22

Utukufu Wa Sayuni

160:1 Isa 52:2; Yn 8:12; Mal 4:2; Za 36:9; Efe 5:14; Za 118:27; Ufu 21:11; Kut 16:7“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja

na utukufu wa Bwana umezuka juu yako.

260:2 Yer 13:16; Kol 1:13; 1Sam 2:9; Za 82:5; Isa 8:20; Za 107:14Tazama, giza litaifunika dunia

na giza kuu litayafunika mataifa,

lakini Bwana atazuka juu yako

na utukufu wake utaonekana juu yako.

360:3 Mt 2:1-11; Isa 49:23; Ufu 21:24; Isa 44:5; 45:14; 42:6Mataifa watakuja kwenye nuru yako

na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.

460:4 Isa 11:12; 43:6; 49:20-22; Yer 30:10; Isa 43:6“Inua macho yako na utazame pande zote:

Wote wanakusanyika na kukujia,

wana wako wanakuja toka mbali,

nao binti zako wanabebwa mikononi.

560:5 Rum 11:25; Kut 34:29; Isa 35:2; 65:13; 66:14; Zek 10:7; Kum 33:19; Amu 3:15; Ufu 21; 6Ndipo utatazama na kutiwa nuru,

moyo wako utasisimka na kujaa furaha,

mali zilizo baharini zitaletwa kwako,

utajiri wa mataifa utakujilia.

660:6 Mwa 25:2-4; Yer 6:20; Za 72:10; Mt 2:11; Amu 6:5; Isa 42:10Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako,

ngamia vijana wa Midiani na Efa.

Nao wote watokao Sheba watakuja,

wakichukua dhahabu na uvumba

na kutangaza sifa za Bwana.

760:7 Mwa 25:13; Hag 2:3-9; Isa 18:7; Sef 3:10; Eze 20:40; 43:27; Isa 19:21Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,

kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia,

watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu,

nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.

860:8 Isa 49:21; 19:1“Ni nani hawa warukao kama mawingu,

kama hua kuelekea kwenye viota vyao?

960:9 Mwa 10:4; Isa 2:16; 14:2; Yer 30:19; Isa 43:6; Gal 4:26; 1Fal 10:22Hakika visiwa vinanitazama,

merikebu za Tarshishi60:9 Au: za biashara (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16). ndizo zinazotangulia,

zikiwaleta wana wenu kutoka mbali,

wakiwa na fedha na dhahabu zao,

kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwa maana amekujalia utukufu.

1060:10 Ezr 1:2; Ufu 21:24; Za 102:13; Isa 54:8; Kut 1:11; Isa 14:1-2; 56:6“Wageni watazijenga upya kuta zako,

na wafalme wao watakutumikia.

Ingawa katika hasira nilikupiga,

lakini katika upendeleo wangu

nitakuonyesha huruma.

1160:11 Mik 2:13; Ufu 21:25-26; Isa 2:12; 61:6; Za 24:7Malango yako yatakuwa wazi siku zote,

kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku,

ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa:

wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi.

1260:12 Isa 11:14; Zek 14:17; Za 2:12; Dan 2:34; Mwa 27:29Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia;

utaharibiwa kabisa.

1360:13 Isa 35:2; Ezr 3:7; 1Nya 28:2; Isa 41:19“Utukufu wa Lebanoni utakujilia,

msunobari, mvinje pamoja na mteashuri,

ili kupapamba mahali pangu patakatifu,

nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.

1460:14 Mwa 27:29; Ufu 3:9; Ebr 12:22; Isa 14:9; 1:12Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako,

wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako,

nao watakuita Mji wa Bwana,

Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.

1560:15 Isa 6:12; 54:6; Za 126:5; Isa 65:18; 1:7-9; Kut 14:30; Isa 33:8“Ingawa umeachwa na kuchukiwa,

bila yeyote anayesafiri ndani yako,

nitakufanya kuwa fahari ya milele,

na furaha ya vizazi vyote.

1660:16 Eze 34:30; Kut 6:2; Isa 66:11-12; Ay 19:25; Isa 59:20; Kut 14:30Utanyonya maziwa ya mataifa,

na kunyonyeshwa matiti ya wafalme.

Ndipo utakapojua kwamba Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako,

Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.

1760:17 1Fal 10:21; Za 85:8; Isa 66:12; 9:7; Hag 2:9Badala ya shaba nitakuletea dhahabu,

na fedha badala ya chuma.

Badala ya mti nitakuletea shaba,

na chuma badala ya mawe.

Nitafanya amani kuwa mtawala wako,

na haki kuwa mfalme wako.

1860:18 Law 26:6; 2Sam 7:10; Yer 33:9; Sef 3:20; Isa 9:4; 49:19; 33:6; 61:11; 62:7Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako,

wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako,

lakini utaita kuta zako Wokovu,

na malango yako Sifa.

1960:19 Zek 2:5; Za 36:9; Ufu 21:23; 22:5; Za 118:27Jua halitakuwa tena nuru yako mchana,

wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia,

kwa maana Bwana atakuwa nuru yako ya milele,

naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.

2060:20 Amo 8:9; Isa 30:19, 26; Ufu 7:17; Isa 35:10Jua lako halitazama tena,

nao mwezi wako hautafifia tena;

Bwana atakuwa nuru yako milele,

nazo siku zako za huzuni zitakoma.

2160:21 Efe 2:10; Law 10:3; Za 37:11, 22; Zek 8:12; Amo 9:15; Isa 4:3; Yer 32:41; Mt 15:13Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu,

nao wataimiliki nchi milele.

Wao ni chipukizi nililolipanda,

kazi ya mikono yangu,

ili kuonyesha utukufu wangu.

2260:22 Mwa 12:2; Kum 1:10; Isa 5:19Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu,

mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu.

Mimi ndimi Bwana;

katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

以賽亞書 60:1-22

錫安將來的榮耀

1起來,發光吧!因為你的光已經來到,

耶和華的榮耀光照你。

2看啊,黑暗遮蓋大地,

幽暗籠罩萬民,

但耶和華必光照你,

祂的榮耀必顯在你身上。

3萬國要來就你的光,

君王要來就你的曙光。

4耶和華說:「舉目四望吧,

眾人正聚到你面前,

你的兒子們從遠方來,

你的女兒們被護送回來。

5你看見後就容光煥發,心花怒放,

因為海上的貨物要歸給你,

列國的財富都要歸給你。

6米甸以法的駱駝必成群結隊而來,

佈滿你的地面;

示巴人都必帶著黃金和乳香來頌讚耶和華。

7基達的羊群必聚集到你那裡,

尼拜約的公羊必供你使用,

牠們在我的壇上必蒙悅納。

我要使我榮美的殿更榮美。

8「這些好像雲彩飛來,

又像鴿子飛回巢穴的是誰?

9眾海島都等候我,

他施的船隻領航,

從遠處把你的兒子和他們的金銀一同帶來,

以尊崇你的上帝耶和華——以色列的聖者,

因為祂已經使你得到榮耀。

10「外族人要為你建造城牆,

他們的君王要服侍你。

我曾發怒擊打你,

如今我要施恩憐憫你。

11你的城門要一直敞開,

晝夜不關,

好讓列國的君王帶著百姓和財物前來向你朝貢。

12不事奉你的邦國都必滅亡,

被徹底摧毀。

13黎巴嫩引以為榮的松樹、杉樹和黃楊樹都要運到你這裡,

用來裝飾我的聖所;

我要使我腳踏之處充滿榮耀。

14欺壓你之人的子孫要來向你下拜,

藐視你的人要在你腳前跪拜。

他們要稱你為耶和華的城,

以色列聖者的錫安

15「雖然你曾被撇棄、被厭惡,

無人從你那裡經過,

但我要使你永遠尊貴,

世世代代都充滿歡樂。

16你必吸各國的乳汁,

吃列王的奶水。

那時,你就知道我耶和華是你的救主,

雅各的大能者是你的救贖主。

17「我要帶給你金子,而非銅;

帶給你銀子,而非鐵;

帶給你銅,而非木頭;

帶給你鐵,而非石頭。

我要使和平做你的官長,

使公義做你的首領。

18你國中再沒有暴力,

境內再沒有破壞和毀滅的事;

你必給你的城牆取名叫『拯救』,

給你的城門取名叫『讚美』。

19「太陽不再作你白晝的光,

月亮也不再給你光輝,

因為耶和華要作你永遠的光,

你的上帝要成為你的榮耀。

20你的太陽不再落下,

你的月亮也不再消失,

因為耶和華要作你永遠的光,

你悲哀的日子將要結束。

21你的人民都必成為義人,

永遠擁有這土地。

他們是我栽種的樹苗,是我手中的工作,

以彰顯我的榮耀。

22最小的家族要變成千人大族,

最弱的一國要成為強國。

時候一到,我耶和華必迅速成就這些事。」