2 Wakorintho 11 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

2 Wakorintho 11:1-33

Paulo Na Mitume Wa Uongo

111:1 Mt 17:17; 2Kor 5:13Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo. 211:2 Hos 2:19; Efe 5:26-27Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Kristo kama mabikira safi. 311:3 Mwa 3:1-6; 1Tim 2:14; Ufu 12:5Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo. 411:4 1Kor 3:11; Rum 8:15; Gal 1:6-9Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi. 511:5 2Kor 12:11; Gal 2:6Lakini sidhani ya kuwa mimi ni dhalili sana kuliko hao “mitume wakuu.” 611:6 1Kor 1:17; 2Kor 9:7; Efe 3:4Inawezekana mimi nikawa si mnenaji hodari, lakini ni hodari katika elimu. Jambo hili tumelifanya liwe dhahiri kwenu kwa njia zote.

711:7 2Kor 12:13; Rum 1:1; 1Kor 9:18Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo? 811:8 Flp 4:15-18Niliyanyangʼanya makanisa mengine kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi. 911:9 Flp 4:15; 2Kor 12:13-16Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nikipungukiwa na chochote, sikuwa mzigo kwa mtu yeyote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walinipatia mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yoyote, nami nitaendelea kujizuia. 1011:10 Rum 9:1; Mdo 18:12; 1Kor 9:15Kwa hakika kama vile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu yeyote katika Akaya nzima atakayenizuia kujivunia jambo hili. 1111:11 Rum 1:9; 2Kor 12:15Kwa nini? Je, ni kwa sababu siwapendi? Mungu anajua ya kuwa nawapenda! 1211:12 2Kor 9:12Nami nitaendelea kufanya lile ninalofanya sasa ili nisiwape nafasi wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia.

1311:13 Mt 7:15; Tit 1:10; Ufu 2:2Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Kristo. 1411:14 Mt 4:10Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. 1511:15 Mt 16:27; Flp 3:19Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.

Paulo Anajivunia Mateso Yake

1611:16 2Kor 11:1; 12:6, 11Nasema tena, mtu yeyote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata kama mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. 1711:17 1Kor 7:12, 25; 2Kor 11:21; 1Kor 7:6Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi kama vile ambavyo Bwana angesema, bali kama mjinga. 1811:18 2Kor 5:16; 10:4; Flp 3:3-4Kwa kuwa wengi wanajisifu kama vile ulimwengu ufanyavyo, mimi nami nitajisifu. 1911:19 1Kor 4:10; 2Kor 11:1Ninyi mwachukuliana na wajinga kwa sababu mna hekima sana! 2011:20 2Kor 11:1Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida au akiwanyangʼanya au akijitukuza mwenyewe au akiwadanganya. 2111:21 2Kor 10:1; Flp 3:4Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo!

Lakini chochote ambacho mtu mwingine yeyote angethubutu kujisifia, nanena kama mjinga, nami nathubutu kujisifu juu ya hilo. 2211:22 Flp 3:5; Rum 9:4; 11:1; Lk 3:8Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Je, wao ni Waisraeli? Mimi pia ni Mwisraeli. Je, wao ni wazao wa Abrahamu? Mimi pia ni mzao wa Abrahamu. 2311:23 1Kor 3:5; 15:10; Mdo 16:23; 2Kor 6:4-5; Rum 8:36Je, wao ni watumishi wa Kristo? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii kuwaliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi. 2411:24 Kum 25:3Mara tano nimechapwa na Wayahudi viboko arobaini kasoro kimoja. 2511:25 Mdo 16:22; 14:19; 27:1-44Mara tatu nilichapwa kwa fimbo, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa, 2611:26 Mdo 20:3; 21:31; Gal 2:4katika safari za mara kwa mara. Nimekabiliwa na hatari za kwenye mito, hatari za wanyangʼanyi, hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, hatari kutoka kwa watu wa Mataifa; hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini; na hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 2711:27 Mdo 18:3; Kol 1:29; 1Kor 4:11-12; 2Kor 6:5Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi; ninajua kukaa njaa na kuona kiu; nimefunga kula chakula mara nyingi; nimehisi baridi na kuwa uchi. 2811:28 1Kor 7:17Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa na mzigo wa wajibu wangu kwa makanisa yote. 2911:29 Rum 14:1; 1Kor 2:3; Mt 5:29Je, ni nani aliye mdhaifu, nami nisijisikie mdhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike?

3011:30 Gal 6:14; 2Kor 12:5-9; 1Kor 2:3Kama ni lazima nijisifu, basi nitajisifia yale mambo yanayoonyesha udhaifu wangu. 3111:31 Rum 1:25; 9:5Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye anahimidiwa milele, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. 3211:32 Mdo 9:24; 9:25Huko Dameski, mtawala aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliulinda mji wa Dameski ili kunikamata. 33Lakini nilishushwa kwa kapu kubwa kupitia katika dirisha ukutani, nikatoroka kutoka mikononi mwake.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

哥林多後書 11:1-33

保羅與假使徒

1請你們包容我的這點愚妄吧!我知道你們一定會包容我。 2我以上帝痛恨不貞的愛愛你們。因為我曾把你們當作貞潔的少女許配給一位丈夫——基督。 3但我真怕你們會像被狡猾的蛇欺騙的夏娃一樣,思想受迷惑,失去了對基督純真專一的心。 4有人來傳另一位耶穌——與我們所傳的不同,或要你們接受另一個靈——與你們所接受的不同,或要你們相信另一種福音——與你們所相信的不同,你們竟欣然容忍。 5我想,我一點也不比那些「超級使徒」差。 6我雖然不善辭令,但我認識真理。這一點,我們在各方面已經向你們證明了。

7我為了把上帝的福音白白地傳給你們,甘願卑微,以提升你們,我這樣做有罪嗎? 8我「搶奪」其他教會,拿了他們的資助,來服侍你們。 9我在你們那裡經濟拮据的時候,沒有拖累過你們任何人,因為馬其頓來的弟兄補足了我的缺乏。我沒有在任何方面成為你們的負擔,將來也不會成為你們的負擔。 10我憑我心中基督的真理說,亞該亞地區無人會阻止我這樣誇口。 11為什麼呢?難道我不愛你們嗎?上帝知道我愛你們!

12我現在所做的,將來還會繼續做下去,為了要斷絕那些投機分子的機會,使他們無法在所誇耀的事上被認為與我們一樣。 13其實這些人是假使徒,為人詭詐,冒充基督的使徒。 14這不足為奇,因為連撒旦都裝成光明的天使, 15牠的爪牙若冒充公義的僕人,又何足為奇呢?他們最終必得到應得的報應。

保羅的諸多苦難

16我再說,誰也別把我當作傻瓜。你們如果真這麼想,那就把我當傻瓜看待吧!好讓我也能說幾句自誇的話。 17我這樣說,並不是主的意思,而是像一個傻瓜一樣誇口。 18既然許多人憑血氣誇口,我當然也可以誇口。 19因為你們這些聰明人竟然甘願忍受那些傻瓜, 20就算有人奴役、剝削、利用、侮辱你們,打你們耳光,你們都能逆來順受! 21慚愧得很,我必須說,我們太軟弱了,做不出那樣的事!

然而,別人敢誇口的,我再講一句傻話,我也敢。 22他們是希伯來人,我也是。他們是以色列人,我也是。他們是亞伯拉罕的子孫,我也是。 23他們自稱是基督的僕人,我說句狂話,我更是!我比他們更辛苦,坐牢更多,身受更重的鞭打,經常出生入死。 24我被猶太同胞鞭打了五次,每次三十九鞭11·24 「三十九鞭」希臘文是「四十鞭減一鞭」。25被人用棍打了三次,用石頭打了一次,遇到船難三次,曾在大海上漂浮了一天一夜。 26我常常四處奔波,遭遇江河的危險、盜賊的威脅、同胞的威脅、外族的威脅、城中的危險、曠野的危險、海上的危險和假信徒的威脅。 27我勞碌困苦,不得安眠,又饑又渴,挨餓受凍,赤身露體。 28此外,我還掛慮眾教會的事,天天承受著壓力。 29有誰軟弱,我不感同身受呢?有誰失足犯罪,我不心急如焚呢?

30如果一定要誇耀,我情願誇耀自己的軟弱。 31主耶穌的父上帝永受稱頌,祂知道我不撒謊。 32大馬士革的時候,亞哩達王手下的總督吩咐人把守城門,要逮捕我。 33我被人用筐子從城牆上的窗戶縋下去,才逃出他的手掌。