2 Wafalme 2 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

2 Wafalme 2:1-25

Eliya Achukuliwa Mbinguni

12:1 Mwa 5:24; 1Fal 19:16Wakati Bwana alipokuwa karibu kumchukua Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya na Elisha walikuwa njiani wakitoka Gilgali. 22:2 Rut 1:16Eliya akamwambia Elisha, “Kaa hapa. Bwana amenituma Betheli.”

Lakini Elisha akasema, “Kwa hakika, kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo wakaenda Betheli pamoja.

32:3 1Sam 10:5Wana wa manabii waliokuwako huko Betheli wakamjia Elisha na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?”

Elisha akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”

42:4 Yos 3:16Kisha Eliya akamwambia, “Baki hapa, Elisha. Bwana amenituma Yeriko.”

Naye akajibu, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.

52:5 2Fal 2:3Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba Bwana atakuondolea bwana wako leo?”

Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”

62:6 Yos 3:15Kisha Eliya akamwambia, “Kaa hapa. Bwana amenituma kwenda Yordani.”

Naye akamjibu, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja.

7Wana hamsini wa manabii wakaenda na kusimama kwa mbali, kuelekea mahali ambapo Eliya na Elisha walikuwa wamesimama kando ya Mto Yordani. 82:8 Kut 14:21Eliya akachukua vazi lake, akalisokota na kupiga nalo maji. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.

92:9 Kum 21:17; Hes 11:17Walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?”

Elisha akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”

10Eliya akasema, “Umeomba jambo gumu. Lakini kama utaniona wakati ninapoondolewa kutoka kwako litakuwa lako. La sivyo, hautalipata.”

112:11 2Fal 6:17; Za 104:3, 4Walipokuwa wakitembea pamoja na kuzungumza, ghafula gari la moto na farasi wa moto vilitokea na kuwatenganisha wao wawili, naye Eliya akapanda mbinguni katika upepo wa kisulisuli. 122:12 2Fal 13:14; Mwa 37:29Elisha aliona hili, naye akapaza sauti, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya Israeli na wapanda farasi wake!” Naye Elisha hakumwona tena. Kisha akazishika nguo zake mwenyewe na kuzirarua.

13Akaliokota lile vazi lililoanguka kutoka kwa Eliya, kisha akarudi na kusimama ukingoni mwa Yordani. 142:14 1Fal 19:19Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Eliya, naye akayapiga yale maji nalo. Akauliza, “Yuko wapi sasa Bwana, Mungu wa Eliya?” Elisha alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.

152:15 1Sam 10:5; Hes 11:17Wale wana wa manabii kutoka Yeriko waliokuwa wakitazama wakasema, “Roho wa Eliya inamkalia Elisha.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi nchi mbele yake. 162:16 1Fal 18:12; Mdo 8:39Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho wa Bwana amemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.”

Elisha akajibu, “Hapana, msiwatume.”

172:17 Amu 3:25Lakini wakasisitiza, mpaka akaona aibu kuwakatalia. Hivyo akasema, “Watumeni.” Nao wakawatuma watu hamsini, wakamtafuta kwa siku tatu, lakini hawakumpata. 18Walipomrudia Elisha, ambaye alikuwa akingojea huko Yeriko, akawaambia, “Je, sikuwaambia msiende?”

Kuponywa Kwa Maji

19Watu wa mji wakamwambia Elisha, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake ni mabaya, na nchi haizai.”

20Akasema, “Nileteeni bakuli mpya, mweke chumvi ndani yake.” Kwa hiyo wakamletea.

212:21 Kut 15:25; 2Fal 4:41; 6:6Kisha akaenda kwenye chemchemi na kuitupa ile chumvi ndani yake, akisema, “Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Nimeyaponya maji haya. Kamwe hayatasababisha mauti tena wala kutozaa.’ ” 222:22 Kut 15:22Nayo yale maji yakaponywa mpaka leo, sawasawa na neno la Elisha alilokuwa amesema.

Elisha Anafanyiwa Mzaha

232:23 2Nya 30:10; Za 31:18Kutoka huko Elisha akakwea kwenda Betheli. Ikawa alipokuwa akitembea barabarani, baadhi ya vijana wakatoka mjini na kumfanyia mzaha. Wakasema, “Paa, wewe mwenye upaa! Paa, wewe mwenye upaa!” 242:24 Mwa 4:11; Kum 18:19Akageuka, akawatazama na kuwalaani kwa Jina la Bwana. Kisha dubu wawili wa kike wakatokea mwituni na kuwararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao. 25Naye akaondoka huko, akaenda Mlima Karmeli, na kutoka huko akarudi Samaria.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

列王纪下 2:1-25

以利亚被接到天上

1耶和华用旋风接以利亚升天之前,以利亚以利沙正离开吉甲2以利亚以利沙说:“你留在这里吧,耶和华差遣我去伯特利。”以利沙说:“我凭永活的耶和华和你的性命起誓,我决不离开你。”于是二人前往伯特利3伯特利的众先知出来见以利沙,问他:“你知道耶和华今天要接走你师傅吗?”他说:“我知道,请不要作声。”

4以利亚以利沙说:“你留在这里吧,耶和华差遣我去耶利哥。”以利沙说:“我凭永活的耶和华和你的性命起誓,我决不离开你。”于是二人前往耶利哥5耶利哥的众先知来见以利沙,问他:“你知道耶和华今天要接走你师傅吗?”他说:“我知道,请不要作声。”

6以利亚以利沙说:“你留在这里吧,耶和华差遣我去约旦河。”以利沙说:“我凭永活的耶和华和你的性命起誓,我决不离开你。”于是二人继续前行。 7先知中有五十人跟他们来到约旦河,远远地站着,他们二人则站在河边。 8以利亚脱下外衣卷起来,用它击打河水,水立即左右分开,二人脚踏干地而过。

9到对岸后,以利亚以利沙说:“在我被接走之前,你要我为你做什么?”以利沙说:“请将你的灵加倍给我。” 10以利亚说:“这是个很难的要求。不过,我被接走的时候,你若看得见我,就可以得到,否则就得不到。” 11他们边走边谈,忽然有火马拉的火车把他们二人隔开,以利亚乘着旋风升上了天。 12以利沙见此情景,便喊道:“我父啊!我父啊!以色列的战车和骑兵啊!”以利沙以利亚消失在天空中,就悲伤地把自己的衣服撕成两半。

13他拿起以利亚身上掉下来的外衣,回到约旦河边, 14用它击打河水,说:“以利亚的上帝耶和华在哪里呢?”河水就左右分开,以利沙便过了河。

15耶利哥的先知们从远处看见他,就说:“以利亚的灵降在以利沙身上了。”他们就上前迎接,俯伏在他面前, 16说:“仆人们这里有五十个壮士,请让他们去寻找你师傅吧,也许耶和华的灵把他提走,放在某座山上或某个山谷里了。”以利沙说:“你们不要派人去找了。” 17他们再三恳求,以利沙难以推辞,就让他们派人去了。他们派去了五十人,找了三天也没有找到。 18他们回来的时候,以利沙仍在耶利哥。他对他们说:“我不是早就告诉你们不要去吗?”

以利沙行神迹

19耶利哥城的人对以利沙说:“我主,你看这城地势很好,只是水不好,地里长不出庄稼。” 20以利沙说:“拿一个新碗装些盐给我。”他们就去照办。 21以利沙走到水源那里,把盐倒在水中说:“耶和华说,‘我洁净了这水,从此它不会再使人死亡,也不会再使土地贫瘠。’” 22果然如以利沙所说,那里的水变好了,直到如今。

23以利沙从那里去伯特利,正在赶路的时候,从城里出来一群少年讥笑他说:“秃头,上去吧!秃头,上去吧!” 24以利沙转身看着他们,奉耶和华的名咒诅他们。林中随即走出来两只母熊,咬死了其中的四十二个少年。 25以利沙伯特利上了迦密山,又从迦密山回到撒玛利亚