2 Nyakati 4 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 4:1-22

Vifaa Vya Hekalu

(1 Wafalme 7:23-51)

14:1 Eze 43:13; Kut 27:1-2; 2Fal 16:14; 1Fal 9:25Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,4:1 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.4:1 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. 24:2 Kut 30:18; Ufu 4:6; 15:2; 1Fal 7:23Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini4:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. ingeweza kuizunguka. 34:3 1Fal 7:24Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.4:3 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.

44:4 Eze 48:30-34; Ufu 21:13Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana. 54:5 1Fal 7:26Unene wake ulikuwa nyanda nne,4:5 Nyanda nne ni sawa na sentimita 7.5. na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 3,000.4:5 Bathi 3,000 ni sawa na lita 60,000.

64:6 Kut 30:18; 1Fal 7:26; Ebr 9:9; 4:7Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.

74:7 Kut 25:31, 40; 1Fal 7:49Akatengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu kama ilivyoainishwa kwao na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini.

84:8 Kut 25:23; Hes 4:14; 1Fal 7:48-49Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli 100 ya dhahabu ya kunyunyizia.

94:9 2Fal 21:5; 2Nya 33:5Akatengeneza ukumbi wa makuhani na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba. 10Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba.

114:11 1Fal 7:14Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani:

12zile nguzo mbili;

yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo,

zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo;

134:13 Yer 52:23; Wim 4:13; Kut 28:33-34; 1Fal 7:20yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);

144:14 1Fal 7:27-30vishikio pamoja na masinia yake;

15hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;

16pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana.

Vitu vyote ambavyo Huramu-Abi alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. 174:17 Mwa 33:17; 1Fal 7:46Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.4:17 Au Sarethani. 184:18 1Fal 7:23, 47Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.

194:19 Kut 25:23, 30; 2Fal 24:13; Dan 5:2-3; Yer 28:3; 1Nya 28:6Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu:

madhabahu ya dhahabu;

meza za kuweka mikate ya Wonyesho;

204:20 Kut 27:20-21vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya sehemu takatifu ya ndani kama ilivyoelekezwa;

214:21 Kut 37:20; 1Fal 6:18-35; Kut 25:31maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa);

224:22 Hes 7:14; Law 10:1; 1Fal 6:21mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

历代志下 4:1-22

圣殿的器具

1所罗门造了一座铜坛,长九米,宽九米,高四米半。 2他又铸了一个圆形的铜海,高两米二,直径四米半,周长十三米半。 3铜海边缘下面有两圈牛的图案,每四十五厘米有十头牛,是跟铜海一起铸造的。 4有十二头铜牛驮着铜海,三头向北,三头向西,三头向南,三头向东。铜海安在牛上,牛尾向内。 5铜海厚八厘米,边如杯边,又如百合花,容量为六万六千升。 6他又造了十个盆,五个放右边,五个放左边,用来清洗献燔祭所用之物。但铜海只供祭司洗涤使用。

7他照着所定的式样,造了十个金灯台放在殿里,五个在右边,五个在左边; 8又造了十张桌子放在殿里,五张在右边,五张在左边;还造了一百个金碗。 9他又建了祭司院、大院及大院的门,门都包上铜。 10铜海放在殿的右边,就是东南方。

11户兰又造了锅、铲和碗。他为所罗门王完成了上帝殿里的工作。 12户兰所制造的有:两根柱子,两个碗状的柱冠,两个装饰柱冠的网子, 13四百个安在网子上的石榴,每个网子上两行石榴,用来装饰碗状的柱冠; 14盆座及盆座上的盆; 15铜海和铜海下面的十二头铜牛; 16锅、铲、肉叉及耶和华殿里的一切器具。这些都是巧匠户兰用磨亮的铜为所罗门王制造的。 17这些都是照王的命令,在疏割撒利但之间的约旦平原用泥模铸成的。 18所罗门制造的器具极多,铜的重量无法统计。

19所罗门又为上帝的殿造了以下器具:金坛和放供饼的桌子, 20按规定放在内殿前的纯金灯台和灯盏, 21灯台上的金花、灯盏、火钳、 22灯剪、碗、碟和火鼎。殿门和至圣所的门也是金的。