1 Wafalme 4 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version

1 Wafalme 4:1-34

Maafisa Wa Solomoni Na Watawala

1Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote. 24:2 Es 8:17; 2Fal 17:24, 41; 19:37Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu:

Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki;

34:3 Yn 4:9; 2Nya 36:22-23; Ezr 1:1-4; 6:3; Isa 44:28; Neh 2:20; Mdo 8:21Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi;

Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani;

44:4 Ezr 3:3; Yer 38:4; Isa 35:3-4Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi;

Sadoki na Abiathari: makuhani;

5Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya;

Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme;

64:6 Es 3:13; 9:5; Dan 9:1Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme;

Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha.

74:7 Ezr 7:1; Isa 36:11; Neh 2:1Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka. 84:8 Za 112:6; Zek 1:14; Rum 8:28Majina yao ni haya:

Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;

94:9 Ezr 5:6; 2Fal 17:30, 31Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani;

104:10 Neh 4:2; Ezr 7:12Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);

11Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni);

124:12 Amo 7:10; Lk 23:2; Mdo 24:5Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;

134:13 Ezr 7:24; Neh 5:4; Mt 9:9Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);

14Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;

154:15 Ezr 5:17; Es 3:8; Mdo 17:6-7Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);

16Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;

17Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;

18Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;

194:19 2Fal 18:7Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.

Mahitaji Ya Solomoni Ya Kila Siku

204:20 Mwa 15:18-21; Kut 23:31; Za 72:8; 1Nya 18:3Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi. 21Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.

224:22 Dan 6:2Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini4:22 Kori 30 ni sawa na madebe 360. za unga laini, kori sitini4:22 Kori 60 ni sawa na madebe 720. za unga wa kawaida. 234:23 Mit 4:16Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana. 244:24 Dan 9:25; Ay 20:5Kwa kuwa Solomoni alitawala falme zote magharibi ya mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote. 25Wakati wa maisha ya Solomoni Yuda na Israeli, kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba, wakaishi salama kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake.

26Solomoni alikuwa na mabanda 4,0004:26 Waandishi wengine wanasema 40,000 (angalia 2Nya 9:25). ya magari ya vita, na farasi 12,000.

27Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua. 28Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili.

Hekima Ya Solomoni

29Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari. 30Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri. 31Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka. 32Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005. 33Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki. 34Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

列王纪上 4:1-34

所罗门的臣仆

1所罗门王统治以色列2以下是他的众臣仆:撒督的儿子亚撒利雅做祭司; 3示沙的儿子以利何烈亚希亚做书记;亚希律的儿子约沙法做史官; 4耶何耶大的儿子比拿雅做元帅;撒督亚比亚他做祭司长; 5拿单的儿子亚撒利雅掌管吏部;拿单的儿子撒布得祭司做所罗门王的顾问; 6亚希煞总管宫廷事务;亚比大的儿子亚多尼兰总管做劳役的。

7所罗门以色列全国设立了十二个地方官,负责供给王及王室的需用,每年每人负责一个月。 8这十二个地方官是:便·户珥,负责以法莲山区; 9便·底甲,负责玛迦斯沙宾伯·示麦以伦·伯·哈南10便·希悉,负责亚鲁泊,包括梭哥希弗全境; 11所罗门女儿她法的丈夫便·亚比拿达,负责多珥高原; 12亚希律的儿子巴拿,负责他纳米吉多,靠近撒拉他拿耶斯列下边的伯·善全境,以及从伯·善亚伯·米何拉,远至约缅13便·基别,负责基列拉末玛拿西子孙雅珥基列的城邑,以及巴珊亚珥歌伯地区有城墙和铜闩的大城六十座; 14易多的儿子亚希拿达,负责玛哈念15所罗门的另一个女儿巴实抹的丈夫亚希玛斯,负责拿弗他利16户筛的儿子巴拿,负责亚设亚禄17帕路亚的儿子约沙法,负责以萨迦18以拉的儿子示每,负责便雅悯19乌利的儿子基别,独自负责从前属亚摩利西宏巴珊基列地区。

所罗门的财富和智慧

20犹大人和以色列人多如海沙,丰衣足食,生活幸福。 21所罗门统管列国,从幼发拉底河至非利士,直到埃及边界。所罗门在世的日子,列国都年年进贡称臣。

22所罗门每天的膳食用三千公斤细面粉、六千公斤粗面粉、 23十头肥牛、二十头草场的牛、一百只羊,此外还有鹿、羚羊、狍子及肥禽。 24所罗门统治幼发拉底河西面所有的国家,从提弗萨直到迦萨,四境安宁。 25所罗门在世的时候,从别示巴犹大人和以色列人都在自己的葡萄树和无花果树下安居。

26所罗门有四万个安置拉战车马匹的马厩和一万二千名骑兵。 27十二个地方官按月供给所罗门王及王室的需用,使他们一无所缺。 28他们也各按其份提供喂战车马等马匹用的大麦和干草。

29上帝赐予所罗门极大的智慧和悟性,以及如海边的沙一样浩博的学识。 30他的智慧高过东方人和埃及人的一切智慧, 31无人能比,胜过以斯拉以探玛曷的儿子希幔甲各达大的智慧。他名扬四周列国。 32所罗门写下箴言三千句,作诗歌一千零五首。 33他对飞禽走兽、草木鱼虫,从黎巴嫩的香柏树到长在墙上的牛膝草,都无所不知。 34天下列王风闻所罗门的智慧,都纷纷遣使来求教。