1 Wafalme 5 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 5:1-18

Maandalio Ya Ujenzi Wa Hekalu

(2 Nyakati 2:1-18)

15:1 Ezr 6:14; Hag 1:14; Zek 8:9Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Solomoni ametiwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Solomoni, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi. 25:2 1Nya 3:19; Ezr 6:14; Mhu 12:11; Zek 4:6-10; Hag 1:2-15; 2:2-5Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu:

35:3 Ezr 6:6“Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wake, hadi Bwana alipowaweka adui zake chini ya miguu yake. 4Lakini sasa Bwana Mungu wangu amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa. 55:5 2Fal 25:28; 1Pet 3:12; 2Nya 16:9; Ezr 7:6, 28; Za 33:18; Isa 41:10Kwa hiyo, ninakusudia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia baba yangu Daudi, wakati aliposema, ‘Mwanao nitakayemweka kwenye kiti cha ufalme mahali pako, ndiye atajenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

65:6 Ezr 4:9“Hivyo toa amri ili mierezi ya Lebanoni ikatwe kwa ajili yangu. Watu wangu watafanya kazi na watu wako, nami nitawalipa watu wako kwa ujira wowote utakaoupanga. Unajua kwamba hatuna mtu yeyote mwenye ustadi katika kukata miti kama Wasidoni.”

7Hiramu aliposikia ujumbe wa Solomoni, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Bwana leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima kutawala juu ya taifa hili kubwa.”

8Hiramu akatuma neno kwa Solomoni:

“Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mierezi na misunobari. 95:9 Ezr 4:12Watu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga mafungu mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.”

10Kwa njia hii Hiramu akampa Solomoni miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji, 115:11 1Fal 6:1; Yos 24:15; Za 119:46; Yn 1:9; Mt 10:32; Lk 12:8; Mdo 27:23; 2Nya 3:1, 2naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,0005:11 Kori 20,000 ni sawa na madebe 240,000. za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000.5:11 Bathi 20,000 ni sawa na madebe 200. Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. 125:12 2Nya 34:24-25; 36:16, 17; Yer 39:1; 2Fal 24:2Bwana akampa Solomoni hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Solomoni, na wote wawili wakafanya mkataba.

135:13 Ezr 1:1Mfalme Solomoni akakusanya wafanyakazi 30,000 kutoka Israeli yote. 145:14 Ezr 6:5; Dan 5:2; 1Nya 3:18; Hag 1:4Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu 10,000 kwa mwezi, hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja na miezi miwili nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa. 15Solomoni alikuwa na wachukuzi wa mizigo 70,000 na wachonga mawe 80,000 huko vilimani, 165:16 Ezr 3:10; 6:15; 4:15; 6:1-2pamoja na wasimamizi 3,300 ambao walisimamia kazi hiyo na kuwaongoza wafanyakazi. 175:17 Ezr 6:1, 2; Mit 25:2Kwa amri ya mfalme walitoa kwenye machimbo ya mawe, mawe makubwa, yaliyo bora kwa kujengea msingi wa nyumba yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu. 18Mafundi wa Solomoni, wa Hiramu na watu wa Gebali5:18 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

列王纪上 5:1-18

预备建造圣殿

1泰尔希兰素来与大卫修好,他听说以色列人膏立了所罗门继承大卫的王位,就遣使者来见所罗门2所罗门也派人去见希兰,说: 3“你知道,我父大卫因周围战事连连,未能为他的上帝耶和华建殿,要等到耶和华使仇敌伏在他脚下后再建。 4现在我的上帝耶和华使我四境太平,内外无忧, 5我想为我的上帝耶和华建殿,因为耶和华曾对我父大卫说,‘我必使你的儿子继承你的王位,他必为我的名建殿。’ 6请你命人为我砍伐黎巴嫩的香柏木。我会派人帮助你的人,并按你的要求付你的人工钱。因为你知道,我们没有人像西顿人那样善于砍伐树木。”

7希兰听了所罗门的话后,非常高兴,说:“今天当赞美耶和华!祂赐给大卫一个有智慧的儿子治理这伟大的民族。” 8他派人回复所罗门说:“我已收到你派人带来的口信。我一定会照你的心愿提供香柏木和松木。 9我的工人会将这些木料从黎巴嫩扎成木筏,经海道运到你指定的地点。木筏拆散以后,你就可以点收了。你也要成全我的心愿,供应我家食粮。” 10于是,希兰供应所罗门需用的香柏木和松木, 11所罗门每年供应希兰四百四十万升麦子和四千四百升橄榄油。 12耶和华照着应许赐给所罗门智慧。他跟希兰修好,缔结盟约。

13所罗门王从以色列征集了三万劳工, 14派他们每月轮班到黎巴嫩工作,每班一万人,在黎巴嫩一个月,在家两个月。亚多尼兰做他们的总管。 15所罗门又征用了七万名搬运工,八万名在山上凿石的匠人。 16此外,他还派了三千三百名监工,监督工人做工。 17他们按照王的命令在山上凿出珍贵的巨石,用来作殿的根基。 18于是,所罗门希兰的工匠及迦巴勒人凿好石头,备好木料,准备建殿。