出埃及記 39 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

出埃及記 39:1-43

祭司的衣服

1比撒列等人按照耶和華對摩西的吩咐,用藍色、紫色、朱紅色毛線精工製作在聖所供職時穿的禮服,又為亞倫做聖衣。 2他們用金線、細麻及藍色、紫色、朱紅色毛線精工製作以弗得, 3把金子打成薄片,剪成細線,與細麻和藍色、紫色、朱紅色毛線巧妙地織在一起。 4他們做了兩條肩帶,固定在以弗得兩邊,用來連接以弗得。 5又按耶和華對摩西的吩咐,照以弗得的做法用金線、細麻及藍色、紫色、朱紅色毛線精工製作腰帶,縫在以弗得上。 6他們選了兩塊紅瑪瑙,用刻圖章的方法刻上以色列十二個兒子的名字,鑲在兩個金框裡, 7再縫在以弗得的兩條肩帶上,作以色列人的紀念石。這些都是照耶和華對摩西的吩咐做的。

8他們精工製作胸牌,像造以弗得一樣用金線、細麻及藍色、紫色、朱紅色毛線製作。 9胸牌是方形的,疊成兩層,長寬各二十二釐米。 10上面鑲上四行寶石:第一行是紅寶石、黃玉和翠玉; 11第二行是綠寶石、藍寶石和金剛石; 12第三行是紫瑪瑙、白瑪瑙和紫晶; 13第四行是水蒼玉、紅瑪瑙和碧玉。這些寶石都鑲在胸牌的金框上。 14他們用刻圖章的方法,在每一顆寶石上刻一個以色列兒子的名字,十二顆寶石代表以色列十二支派。

15他們用純金擰成兩條像繩子一樣的鏈子,連在胸牌上, 16又造兩個金框和兩個金環,把金環安在胸牌兩端。 17把兩條金鏈分別繫在胸牌兩端的金環上, 18又把兩條金鏈的另兩端接在兩個金框上,安在以弗得前面的肩帶上。 19又造了兩個金環,安在靠近以弗得內邊的胸牌下兩端。 20又造了兩個金環,安在以弗得前面兩條肩帶下端,靠近精緻的以弗得腰帶上方的接縫處。 21用一條藍色的帶子繫住以弗得和胸牌上面的金環,使胸牌貼在精工織成的以弗得腰帶上,不會從以弗得上鬆脫。這些都是照耶和華對摩西的吩咐做的。

22以弗得的外袍用純藍色的線織成, 23上面有領口,領口周圍織領邊,就像鎧甲上的領口,免得領口破裂。 24外袍的底邊用細麻和藍色、紫色、朱紅色毛線做成石榴狀的飾物, 25又造純金的鈴鐺掛在外袍底邊的石榴間, 26一個石榴一個金鈴鐺,相間排列,圍在外袍的底邊。這件外袍是祭司供職時穿的,正如耶和華對摩西的吩咐。

27他們用細麻布為亞倫父子們縫製內袍、 28禮冠、頭巾和褲子, 29還用細麻和藍色、紫色、朱紅色毛線繡製腰帶。這是照耶和華對摩西的吩咐做的。 30又用純金造了牌子,就是聖冠,上面用刻印章的方法刻上「耶和華的聖物」的字樣, 31然後用一條藍色帶子把它繫在禮冠上。這些都是照耶和華對摩西的吩咐做的。

聖幕完工

32聖幕,就是會幕的工作就這樣全部完成了,都是以色列人照耶和華對摩西的吩咐做的。 33他們把聖幕和聖幕的各樣器具都送到摩西那裡,即鉤子、木板、橫閂、柱子和帶凹槽的底座; 34海狗皮頂蓋、遮掩約櫃的幔子、染成紅色的公羊皮蓋; 35約櫃、抬約櫃的橫槓、施恩座; 36桌子、桌上的一切器具和供餅; 37純金的燈臺、燈盞、燈臺的一切器具、燈油; 38金壇、膏油、芬芳的香;會幕的門簾; 39銅祭壇、祭壇的銅網、抬祭壇的橫槓、祭壇用的一切器具、洗濯盆和盆座; 40院子的帷幔、柱子、帶凹槽的底座、院子入口的門簾、繩子、橛子和會幕,即聖幕所需的一切器具; 41在聖所供職時穿的精製禮服、亞倫祭司的聖衣及其眾子供祭司之職時穿的衣服。 42這一切都是以色列人照耶和華對摩西的吩咐做的。 43摩西察看這一切工作,見他們都是按照耶和華的吩咐做的,就給他們祝福。

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 39:1-43

Mavazi Ya Kikuhani

(Kutoka 28:1-14)

139:1 Kut 35:19-23; 28:2; Za 93:5; Eze 43Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Aroni mavazi matakatifu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Kisibau

239:2 Kut 28:6; Law 8:7Akatengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kitani iliyosokotwa vizuri. 3Akafua vipande vyembamba vya dhahabu kwa nyundo na kutengeneza nyuzi nyembamba ili kuzifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi, kazi ya fundi stadi. 439:4 Law 24:7; Yos 4:7Akatengeneza vipande vya mabegani vya kisibau, vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kukifungia kisibau. 539:5 Isa 11:5; Ufu 1:13Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

639:6 Kut 28:9; Ay 28:16; Isa 49:16; Ufu 1:17Akatengeneza vito vya shohamu vilivyowekwa katika vijalizo vya dhahabu, navyo vilichorwa na majina ya wana wa Israeli kama vile muhuri huchorwa. 739:7 Law 24:7; Yos 4:7; Kut 28:12; Yos 4:7; Neh 2:20Kisha akavifungia kwenye vipande vya mabega ya kisibau kuwa vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Kifuko Cha Kifuani

(Kutoka 28:15-30)

839:8 Law 8:8; Kut 28:15; Isa 59:17Akafanyiza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. 9Kifuko hicho kilikuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja39:9 Shibiri moja ni sawa na sentimita 22. na upana wa shibiri moja, nacho kilikunjwa mara mbili. 1039:10 Kut 28:17; Eze 28:13; Ufu 21:19, 20; Isa 54:12Kifuko hicho kilipambwa kwa safu nne za vito vya thamani. Safu ya kwanza ilikuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 1139:11 Ufu 4:3; Isa 54:11; Yer 17:1safu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 12safu ya tatu ilikuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 1339:13 Dan 10:6; Ay 28:16; Ufu 21:11katika safu ya nne ilikuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Vito hivyo vilitiwa kwenye vijalizo vya dhahabu. 1439:14 Ufu 21:12Palikuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kikiwa na jina mojawapo la wana wa Israeli; kila kimoja kilichorwa kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.

15Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani akakitengenezea mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. 16Akatengeneza vijalizo viwili vya dhahabu na pete mbili za dhahabu, na kuzifungia pete hizo kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. 17Akafunga hiyo mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, 18nazo zile ncha nyingine za mkufu akazifunga kwenye vile vijalizo viwili, na kuzishikamanisha na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. 19Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuzishikamanisha kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. 20Kisha akatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuzishikamanisha sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. 21Akafunga pete za hicho kifuko cha kifuani kwenye pete za kisibau kwa kamba ya buluu, wakiziunganisha na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Mavazi Mengine Ya Kikuhani

(Kutoka 28:31-43)

2239:22 Kut 28:31; Law 8:7; 1Sam 2:18; 2Sam 6:14Akashona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, kazi ya mfumaji, 23na lilikuwa na nafasi ya shingo katikati ya joho lile iliyofanana na ukosi, na utepe ulioshonwa kuizunguka nafasi hiyo ili isichanike. 24Akatengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na ya kitani iliyosokotwa vizuri kuzunguka pindo la hilo joho. 2539:25 Kut 28:33Kisha akatengeneza vikengele vya dhahabu safi na kuvishikamanisha kuzunguka pindo hilo kati ya hayo makomamanga. 26Hivyo vikengele na makomamanga vilipishana kuzunguka upindo wa joho ili livaliwe kwa kuhudumu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

2739:27 Kut 28:39, 40; 39:27; Law 8:13; Kut 28:4; Isa 61:10; Rum 3:22; Gal 3:27Pia akamtengenezea Aroni na wanawe makoti ya kitani safi, kazi ya mfumaji, 2839:28 Law 6:10; 8:2; Kut 28:39, 42; Eze 44:17, 18na kilemba cha kitani safi, tepe za kichwani za kitani, na nguo za ndani za kitani iliyosokotwa vizuri. 29Mshipi ulikuwa wa kitani iliyosokotwa vizuri ya rangi ya buluu, na zambarau, na nyekundu, kazi ya mtarizi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

3039:30 Isa 23:18; Zek 14:20; Za 93:5; Isa 23:18Kisha akatengeneza lile bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana. 31Kisha wakalifunga kwa kamba ya rangi ya buluu ili kulishikamanisha na kile kilemba kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Mose Akagua Maskani Ya Mungu

(Kutoka 35:10-19)

3239:32 Kut 25:9; 25:40Kwa hiyo kazi yote ya maskani, Hema la Kukutania ikakamilika. Waisraeli wakafanya kila kitu sawasawa kama vile Bwana alivyomwagiza Mose. 3339:33 Kut 25:8-40; 36:10-16; Ebr 9:1-28Ndipo wakaleta maskani kwa Mose: hema pamoja na vifaa vyake vyote, vibanio vyake, mihimili yake, mataruma yake, nguzo na vitako vyake; 34kifuniko cha ngozi za kondoo dume kilichotiwa rangi nyekundu, kifuniko cha ngozi za pomboo,39:34 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. pazia la kufunikia; 3539:35 Kut 30:6; 37:1Sanduku la Ushuhuda pamoja na mipiko yake na kiti cha rehema, 3639:36 Kut 25:23-30; 37:10-16meza pamoja na vyombo vyake vyote na mikate ya Wonyesho; 3739:37 Kut 25:31-39; 25:6; Ufu 1:13-20; Mt 5:14; Flp 2:15kinara cha taa cha dhahabu safi, safu zake za taa pamoja na vifaa vyake vyote pamoja na mafuta kwa ajili ya taa; 3839:38 Kut 31:1-10; 37:25-28; 30:22-32; 37:29; 30:34-38; 36:35madhabahu ya dhahabu, mafuta ya upako, uvumba wenye harufu nzuri na pazia la ingilio la hema; 3939:39 Kut 37:1-8; 38:1-7; 30:18madhabahu ya shaba, pamoja na wavu wa shaba, nguzo zake na vyombo vyake vyote, sinia, na tako lake; 4039:40 Kut 27:9-19; 38:9-20; Ufu 3:12mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania; 41na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.

4239:42 Kut 25:9Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose. 4339:43 Kut 25:9; 35:10; Mwa 31:55; Law 9:22-23; Hes 6:23-27; Kum 26:15; 2Sam 6:18; 1Fal 8:14, 55; 1Nya 16:2; 2Nya 30:27Mose akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Mose akawabariki.