马可福音 3 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马可福音 3:1-35

治好手枯的人

1耶稣又进了会堂,那里有个人一只手是萎缩的。 2当时有好些人监视耶稣,看祂会不会在安息日医治这个人,好控告祂。

3耶稣对那一只手萎缩的人说:“起来,站在中间。” 4然后问众人:“在安息日应该行善还是作恶?救人还是害人?”他们都不吭声。

5耶稣生气地看着四周这些人,为他们心里刚硬而深感难过。祂对那人说:“把手伸出来!”那人一伸手,手就复原了。 6法利赛人立刻出去,跟希律党的人策划怎样除掉耶稣。

群众跟随耶稣

7耶稣和门徒退到湖边,有一大群人从加利利来跟随祂。 8还有很多人听见耶稣的一切作为,就从犹太耶路撒冷以土买约旦河东,甚至泰尔西顿一带来找祂。 9耶稣见人多,就吩咐门徒为祂预备一条小船,以免人群拥挤祂。 10因为祂医治了很多人,凡有疾病的人都想挤过来摸祂。 11污鬼一看见祂,就俯伏在祂面前,大喊:“你是上帝的儿子!” 12耶稣却严厉地警告它们不要泄露祂的身份。

选立十二使徒

13耶稣上了山,把自己想要的人召来,他们就来到祂面前。 14祂从中选出十二人立为使徒,让他们跟随自己,并且差遣他们出去传道, 15赐他们赶鬼的权柄。

16祂设立的十二位使徒是:西门——耶稣给他取名叫彼得17西庇太的儿子雅各雅各的兄弟约翰——耶稣给他们取名叫“半尼其”,就是“雷霆之子”的意思、 18安得烈腓力巴多罗买马太多马亚勒腓的儿子雅各达太、激进党人西门19及后来出卖耶稣的加略犹大

耶稣和别西卜

20耶稣刚进家门,人群又聚集起来,以致祂和门徒都无暇吃饭。 21祂的亲属听见这个消息,就出来要制止祂,因为他们说祂疯了。

22耶路撒冷下来的律法教师说:“祂被别西卜附身。”又说:“祂是靠鬼王赶鬼。”

23耶稣叫他们来,用比喻对他们说:“撒旦怎能驱逐撒旦呢? 24一个国内部自相纷争,必无法坚立。 25一个家内部自相纷争,必无法坚立。 26同样,撒旦如果与自己为敌,自相纷争,就站立不住,必然灭亡。 27没有人能进入壮汉家里抢夺财物,除非先把那壮汉捆绑起来,才能抢劫他的家。

28“我实在告诉你们,世人一切的罪和亵渎的话都可以得到赦免, 29唯有亵渎圣灵的人永远得不到赦免,他们要永远担罪。” 30耶稣这样说是因为他们诬蔑祂被污鬼附身。

谁是耶稣的亲人

31这时候,耶稣的母亲和兄弟来了,他们站在外面,托人叫耶稣。 32有许多人围坐在耶稣身边,他们告诉祂说:“看啊!你的母亲和兄弟在外面找你。”

33耶稣说:“谁是我的母亲?谁是我的兄弟?” 34然后祂望着周围坐着的人说:“看啊,我的母亲和我的兄弟! 35凡遵行上帝旨意的人都是我的弟兄、姊妹和母亲。”

Kiswahili Contemporary Version

Marko 3:1-35

Mtu Aliyepooza Mkono Aponywa

(Mathayo 12:9-14; Luka 6:6-11)

13:1 Mt 4:23; Mk 1:21Yesu akaingia tena ndani ya sinagogi, na huko palikuwa na mtu aliyepooza mkono. 23:2 Mt 12:10; Lk 14:1Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. 3Yesu akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.”

4Kisha Yesu akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza kimya.

53:5 Yn 11:33Yesu akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa kabisa! 63:6 Mt 22:16; Mk 12:13; Mt 12:14Kisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya shauri la kumuua Yesu wakiwa na Maherode.

Umati Wa Watu Wamfuata Yesu

73:7 Mt 4:25Yesu pamoja na wanafunzi wake wakaondoka huko wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya ukamfuata. 83:8 Mt 11:21Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, umati mkubwa wa watu ukamjia kutoka Uyahudi, Yerusalemu, Idumaya, na ngʼambo ya Yordani, pamoja na wale wa sehemu za karibu na Tiro na Sidoni. 9Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga. 103:10 Mt 4:23; 9:20Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa. 113:11 Mt 4:3; Mk 1:23, 24Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.” 123:12 Mt 8:4; Mdo 16:17, 18Lakini aliwaonya wasimseme yeye ni nani.

Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:1-4; Luka 6:12-16)

133:13 Mt 5:11Yesu akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia. 143:14 Mk 6:30Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri 153:15 Mt 10:1na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. 163:16 Yn 1:42Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro); 173:17 Lk 2Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); 18Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo, 19na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.

Yesu Na Beelzebuli

(Mathayo 12:22-32; Luka 11:14-23; 12:10)

203:20 Mk 6:31Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. 213:21 Yn 10:20; Mdo 26:24Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”

223:22 Mt 15:1; 12:24; Yn 10:20; Mt 9:34Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli!3:22 Beelzebuli kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu. Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!”

233:23 Mk 4:2; Mt 4:10Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani? 24Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. 25Nayo nyumba kama ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. 26Naye Shetani kama akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama bali mwisho wake umewadia. 273:27 Isa 49:24-25Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali zake. 283:28 Mt 12:31; Lk 12:10; 1Yn 5:16Amin, nawaambia, dhambi zote na makufuru yote ya wanadamu watasamehewa. 293:29 Mt 12:31-32; Lk 12:10Lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.”

303:30 Mk 3:22Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”

Mama Na Ndugu Zake Yesu

(Mathayo 12:46-50; Luka 8:19-21)

313:31 Mt 12:46; Lk 8:19Kisha wakaja ndugu zake Yesu pamoja na mama yake. Wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. 32Umati wa watu ulikuwa umeketi kumzunguka, nao wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.”

33Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni nani?”

34Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, “Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. 35Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.”