马可福音 2 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马可福音 2:1-28

治好瘫痪的人

1几天后,耶稣回到迦百农。祂在家的消息一传开, 2许多人便蜂拥而来,连门外也挤满了人。耶稣正给他们讲道的时候, 3有四个人抬着一个瘫痪的人来见祂。 4可是人太多了,他们无法抬到耶稣跟前,就拆掉耶稣所在房间的屋顶,将那人连垫子一起缒下去。 5耶稣看见他们的信心,就对瘫痪的人说:“孩子,你的罪得到赦免了!” 6有几个律法教师坐在那里,心里议论说: 7“这是什么话?祂是在亵渎上帝!除了上帝以外,谁能赦罪呢?”

8耶稣立刻看透了他们的心思,就说:“你们为什么这样心里议论呢? 9对瘫痪的人说‘你的罪被赦免了’容易呢,还是说‘起来,收拾你的垫子走吧’容易呢? 10但我要让你们知道人子在世上有赦罪的权柄。”于是祂对那人说: 11“我吩咐你起来拿上你的垫子回家去吧。” 12那人就站起来,马上拿起垫子,当着众人的面走了出去。众人都十分惊奇,赞美上帝说:“我们从来没见过这样的事!”

呼召利未

13耶稣又出去到了湖边。有一大群人围拢过来,祂就教导他们。 14耶稣往前走的时候,看见亚勒腓的儿子利未坐在收税站里,就对他说:“跟从我!”利未就起来跟从了耶稣。

15后来,利未请耶稣和祂的门徒到家里坐席,同席的还有很多已经跟随耶稣的税吏和罪人。 16有几位法利赛人的律法教师看见耶稣跟税吏和罪人同席,就问耶稣的门徒:“祂为何跟税吏和罪人一起吃饭?”

17耶稣听见后,就对他们说:“健康的人不需要医生,有病的人才需要。我来不是召义人,而是召罪人。”

论禁食

18约翰的门徒和法利赛人都在禁食的时候,有人来问耶稣:“约翰的门徒和法利赛人的门徒禁食,为什么你的门徒不禁食呢?”

19耶稣对他们说:“新郎和宾客还在一起的时候,宾客岂能禁食?新郎还跟他们在一起的时候,他们不能禁食。 20但有一天新郎将被带走,那时他们就要禁食了。

21“没有人会用新布来补旧衣服,否则新布会把旧衣服扯破,破洞会更大; 22也没有人把新酒装在旧皮囊里,否则新酒会把旧皮囊胀破,酒和皮囊都毁了。所以,新酒一定要装在新皮囊里。”

安息日的主

23有一个安息日,耶稣经过一片麦田,同行的门徒一边走一边掐麦穗。 24法利赛人对耶稣说:“看啊,他们为什么做安息日不准做的事?”

25耶稣回答说:“你们没有读过大卫的事迹吗?当时他和随从饥饿匮乏, 26他进入上帝的殿吃了献给上帝的供饼,还给他的随从吃,这饼只有祭司才可以吃。这事在发生在亚比亚他做大祭司的时候。”

27然后,耶稣对他们说:“安息日是为人设立的,人不是为安息日设立的。 28所以,人子也是安息日的主。”

Kiswahili Contemporary Version

Marko 2:1-28

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

(Mathayo 9:1-8; Luka 5:17-26)

12:1 Mt 9:4Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani. 22:2 Mk 1:45; 2:13Hivyo watu wengi wakakusanyika kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. 32:3 Mt 4:24Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa Yesu kwa ajili ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa mahali pale alipokuwa Yesu, wakamshusha yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia. 52:5 Lk 7:48Yesu alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”

6Basi baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wameketi huko wakawaza mioyoni mwao, 72:7 Isa 43:25“Kwa nini mtu huyu anasema hivi? Huyu anakufuru! Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”

82:8 Mt 9:4Mara moja Yesu akatambua rohoni mwake kile walichokuwa wanawaza mioyoni mwao, naye akawaambia, “Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? 9Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’? 102:10 Mt 8:20Lakini ili mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Yesu akamwambia yule aliyepooza, 11“Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.” 122:12 Mt 9:8; 9:33Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!”

Yesu Amwita Lawi

(Mathayo 9:9-13; Luka 5:27-32)

132:13 Lk 5:15; Yn 6:2Yesu akaenda tena kandokando ya Bahari ya Galilaya. Umati mkubwa wa watu ukamfuata, naye akaanza kuwafundisha. 142:14 Mt 4:19Alipokuwa akitembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru, akamwambia, “Nifuate.” Lawi akaondoka, akamfuata Yesu.

152:15 Mt 9:10Yesu alipokuwa akila chakula nyumbani mwa Lawi, watoza ushuru wengi pamoja na “wenye dhambi” walikuwa wakila pamoja naye na wanafunzi wake, kwa maana kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakimfuata. 162:16 Mdo 23:9; 9:11Baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa Mafarisayo walipomwona akila pamoja na watoza ushuru na “wenye dhambi,” wakawauliza wanafunzi wake: “Mbona Yesu anakula pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”

172:17 Lk 19:10; 1Tim 1:15Yesu aliposikia haya akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Mathayo 9:14-17; Luka 5:33-39)

182:18 Mt 6:16-18; Mdo 1; Mt 9Basi wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Baadhi ya watu wakamjia Yesu na kumuuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?”

19Yesu akawajibu, “Wageni wa bwana arusi wawezaje kufunga wakati angali pamoja nao? Wakati bwana arusi bado yuko pamoja nao, hawawezi kufunga. 202:20 Lk 17:22Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kwao. Siku hiyo ndipo watakapofunga.

21“Hakuna mtu ashoneaye kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, kile kiraka kipya kitachanika kutoka ile nguo iliyochakaa, nayo itachanika zaidi. 222:22 Lk 5:33-38Wala hakuna mtu awekaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, nayo hiyo divai itamwagika na viriba vitaharibika. Lakini divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.”

Bwana Wa Sabato

(Mathayo 12:1-8; Luka 6:1-5)

232:23 Kum 23:25; Mt 12:1; Lk 6:1Siku moja ya Sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke. 242:24 Mt 12:2Mafarisayo wakamwambia, “Tazama, mbona wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato?”

25Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa, wakahitaji chakula? 262:26 1Nya 24:6; 2Sam 8:17; Law 24:5-9; 1Sam 21:1-6Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.”

272:27 Kut 23:12; Kum 5:14; Kol 2:16Kisha Yesu akawaambia, “Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, lakini si mwanadamu kwa ajili ya Sabato. 282:28 Mt 8:20Hivyo, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”