出埃及记 27 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 27:1-21

造燔祭坛的条例

1“要用皂荚木造一个方形的祭坛,长宽各两米二,高一米三。 2要在坛的四角造四个凸起的角,与坛连成一体,坛外面要包上铜。 3用铜造盛坛灰的盆和其他祭坛用具,即铲、碗、肉叉、火鼎。 4要造一个铜网,在铜网的四角造四个铜环。 5铜网在祭坛围边的下方,向下伸展到祭坛的腰部。 6要用皂荚木为祭坛造两根横杠,包上铜。 7要将两根横杠穿在坛两旁的铜环里,以便抬坛。 8整座坛都用木板制作,坛是中空的。一切都要照我在山上给你的指示去做。

圣幕院子的规划

9“要为圣幕围出一个院子。院子南面的帷幔要用细麻织成,长四十五米, 10帷幔有二十根柱子,二十个带凹槽的铜底座,柱子上的钩和箍都是银的。 11北面的帷幔也是长四十五米,柱子、铜底座、钩和箍的样式都与南面的一样。 12院子西面的帷幔宽二十二米半,有十根柱子和十个带凹槽的底座。 13院子东面的帷幔也是宽二十二米半。 14-15入口两边的帷幔都是宽七米,各有三根柱子和三个带凹槽的底座。 16院子的入口要有门帘,长九米,用细麻和蓝色、紫色、朱红色毛线绣制,还有四根柱子和四个带凹槽的底座。 17院子四围的柱子都要有银箍,所有的钩子都要用银制作,带凹槽的底座要用铜制作。 18整个院子长四十五米,宽二十二米半,高两米二,所有的帷幔都要用细麻精工制作,带凹槽的底座要用铜制作。 19圣幕里其他一切器具以及圣幕、院子所用的橛子都要用铜制作。

20“你要吩咐以色列人把榨的纯橄榄油给你拿来点灯,使灯常明。 21亚伦和他的子孙要负责照看会幕内遮掩约柜的幔子外的灯,使灯从晚上到早晨一直在耶和华面前亮着。这是以色列百姓世代当守的永久律例。

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 27:1-21

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

(Kutoka 38:1-7)

127:1 Kut 20:24; 40:6; 1Fal 8:64“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu;27:1 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35. itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano,27:1 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. na upana wake dhiraa tano. 227:2 Kut 29:12; 30:2; 37:25; Law 4:7; 1Fal 1:50; 2:28; Za 118:27; Yer 17:1; Eze 43:15; Amo 3:14; Zek 9:15Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. 327:3 Hes 7:13; 1Fal 7:40-45; 2Fal 12:13; Hes 4:14; 1Nya 28:17; Yer 52:18Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. 4Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu. 5Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 627:6 Kut 25:13-14, 28Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. 727:7 Hes 4:15; Isa 52:11Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. 827:8 Kut 25:9, 40; Ebr 8:5; Mdo 7:44Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.

Ua Wa Kukutania

(Kutoka 38:9-20)

927:9 Kut 35:17; 40:8, 33; Law 6:16, 26; Eze 40:14; 42:1“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,27:9 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

12“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,27:12 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. 13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano27:15 Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75. kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.

1627:16 Kut 40:33; 36:37“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini27:16 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. 17Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. 18Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. 19Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba.

Mafuta Ya Kinara Cha Taa

(Walawi 24:1-4)

2027:20 Kut 25:6; Law 24:2“Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. 2127:21 Kut 28:43; 29:42; 30:36; 33:7; Law 6:26; 8:3, 31; Hes 31:54; Yos 18:1; 1Fal 1:38-39; Kut 16:34; 25:37; 29:9; 30:21; Law 3:17; 16:34; 17:7; Hes 18:23; 19:21; 1Sam 30:25Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za Bwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.