出埃及记 18 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 18:1-27

叶特罗看望摩西

1摩西的岳父米甸的祭司叶特罗,听说上帝为摩西和祂的子民以色列人所做的一切事及如何带他们出埃及后, 2就带着女儿西坡拉和两个外孙去见摩西西坡拉摩西的妻子,摩西曾让她回娘家暂时居住。 3摩西的两个儿子一个叫革舜,因为摩西说:“我成了在异乡寄居的人”; 4一个叫以利以谢,因为摩西说:“我父亲的上帝帮助我,从法老的刀下拯救了我。” 5摩西的岳父叶特罗带着摩西的妻子和两个儿子来到上帝的山见摩西,就是摩西在旷野安营的地方。 6叶特罗事先差人把他带着摩西的妻子和两个儿子要来的消息通知摩西7摩西出去迎接岳父,向他下拜,与他亲吻,彼此问安,然后大家都进了帐篷。 8摩西把耶和华为拯救以色列人而向法老和埃及人所行的事,以及怎样救百姓脱离路上遇见的种种困难,都告诉了叶特罗9叶特罗为耶和华恩待以色列人、把他们救出埃及而高兴, 10便说:“耶和华当受称颂,因为祂从埃及人和法老手中拯救了你们,把这百姓从埃及人手中拯救了出来。 11我现在知道,耶和华比一切神明都伟大,因为祂惩治了虐待这些百姓的狂妄之徒。”

12摩西的岳父叶特罗说完,便向上帝献燔祭及其他祭物。亚伦以色列的长老都来与他一起在上帝面前吃饭。

13第二天,摩西坐着审理百姓的纠纷,百姓从早到晚都站在摩西周围。 14摩西的岳父叶特罗看见摩西对百姓所行的一切,就对摩西说:“你为什么这样处理百姓的事?为什么你独自坐着,众百姓从早到晚都站在你周围?” 15摩西对岳父说:“因为他们来我这里求问上帝。 16他们有纠纷就来我这里,我为双方定夺是非,教他们认识上帝的律例和法度。” 17摩西的岳父叶特罗摩西说:“这不是好方法, 18你和这些百姓都会疲惫不堪,你一个人无法担当如此繁重的工作。 19你要听我的劝告,愿上帝与你同在。你要做百姓的代表,把案件奏明上帝, 20又要教导他们律例和法度,指示他们当行的道、当做的事。 21此外,你要在民中挑选一些敬畏上帝、有才干、诚实、正直、憎恶不义之财的人,派他们做千夫长、百夫长、五十夫长和十夫长,管理百姓。 22让他们随时为百姓判案,处理小纠纷,遇到大事才由你审理。有他们分担你的责任,你会更轻省。 23如果你这样做,并且上帝也这样吩咐你,你就能承受得住,百姓也可以平安地回家。”

24于是,摩西接纳了岳父的建议,依言而行, 25从百姓中挑选有才干的人,委派他们做百姓的领袖,担任千夫长、百夫长、五十夫长和十夫长。 26他们负责随时审理百姓的事,遇到难断的案件就呈到摩西那里,自己则审理普通的事。 27之后,摩西为岳父送行,叶特罗就返回了家乡。

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 18:1-27

Yethro Amtembelea Mose

118:1 Kut 12:16-18; 6:6Basi Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wa Mose, akawa amesikia kila kitu Mungu alichomfanyia Mose na watu wake wa Israeli, pia jinsi Bwana alivyowatoa Israeli Misri.

218:2 Kut 2:21Baada ya Mose kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea 318:3 Kut 4:20; Mdo 7:29; Kut 2:22pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershomu, kwa kuwa Mose alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” 418:4 1Nya 23:15; Mwa 49:25; Kum 33:29Mwingine aliitwa Eliezeri, kwa kuwa alisema, “Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa kutoka upanga wa Farao.”

518:5 Kut 3:1Yethro, baba mkwe wa Mose, pamoja na wana wawili wa Mose na mkewe, wakamjia Mose huko jangwani, mahali alipokuwa amepiga kambi karibu na mlima wa Mungu. 6Yethro alikuwa ametuma ujumbe kwake Mose, kusema, “Mimi Yethro baba mkwe wako ninakuja kwako pamoja na mke wako na wanao wawili.”

718:7 Mwa 17:3; 43:8; 29:13Kwa hiyo Mose akatoka kumlaki baba mkwe wake, akainama na kumbusu. Wakasalimiana, kisha wakaingia hemani. 818:8 Hes 20:14; Neh 9:32; Kut 15:5, 16; Za 81:7Mose akamwambia baba mkwe wake kuhusu kila kitu Bwana alichomfanyia Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na pia kuhusu shida zote walizokutana nazo njiani na jinsi Bwana alivyowaokoa.

918:9 Yos 21:45; 1Fal 8:66; Neh 9:25; Isa 63:7Yethro akafurahishwa sana kusikia juu ya mambo yote mazuri Bwana aliyowatendea Waisraeli kuwaokoa kutoka mkono wa Wamisri. 1018:10 Mwa 9:26; 24:27Yethro akasema, “Sifa na ziwe kwa Bwana, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri. 1118:11 Kut 12:12; 1Nya 16:25; Kut 1:10; Lk 1:51Sasa najua ya kuwa Bwana ni mkuu kuliko miungu mingine yote, kwa kuwa amewatendea hivi wale waliowatenda Israeli kwa ujeuri.” 1218:12 Kut 3:1; 10:25; 20:24; Law 1:2-9; Mwa 31:54; Kut 24:5; Mwa 26:30; Kum 12:7Kisha Yethro, baba mkwe wa Mose, akaleta sadaka ya kuteketezwa na dhabihu nyingine kwa Mungu, naye Aroni pamoja na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula pamoja na baba mkwe wa Mose mbele za Mungu.

Ushauri Wa Yethro

(Kumbukumbu 1:9-18)

13Siku iliyofuata, Mose akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. 14Baba mkwe wake alipoona yote Mose anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi mpaka jioni?”

1518:15 Mwa 25:22; Hes 9:6-8Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. 1618:16 Kut 24:14; Law 24:12; Hes 15:34; Kum 1:17; 2Nya 19:7; Mit 24:23; Mt 2:9Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake na kuwajulisha juu ya amri na sheria za Mungu.”

17Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri. 1818:18 Hes 11:11, 14, 17; Kum 1:9-12Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe. 1918:19 Kut 3:12; Hes 27:5Sasa nisikilize mimi, nitakupa shauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake. 2018:20 Kum 4:1-4; 5:1; Za 119:12, 26, 68; 143:8; Mwa 39:11Uwafundishe amri na sheria, tena uwaonyeshe namna ya kuishi na kazi zinazowapasa wao kufanya. 2118:21 Mwa 47:6; Mdo 6:3; Mwa 22:12; Kut 23:8; Kum 16:19; 1Sam 12:3; Za 15:5; Mit 17:23; 28:8; Mhu 7:7; Eze 18:8; 22:12; Hes 1:16; 7:2; 10:4; Kum 16:18; Ezr 7:25Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. 2218:22 Law 24:11; Kum 17:18; Hes 11:17; Kum 1:9Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe. 23Kama ukifanya hivi, na ikiwa Mungu ameagiza hivyo, utaweza kushinda uchovu, nao watu hawa wote watarudi nyumbani wameridhika.”

Kuchaguliwa Kwa Waamuzi

24Mose akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. 2518:25 Hes 1:16; 7:2; 11:16; Kum 16:18; 1:13-15Mose akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. 2618:26 Kum 16:18; 2Nya 19:5; Ezr 7:25; Kum 1:17Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Mose, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe.

2718:27 Hes 10:29-30Kisha Mose akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake.