但以理书 6 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

但以理书 6:1-28

但以理在狮子坑

1大流士决定设立一百二十个总督治理全国。 2总督之上设三个总长,负责管理总督,以维护王的统治,但以理是其中之一。 3因为但以理有非凡的心智,远超过其他总长和总督,王便考虑让他治理全国。 4于是,其他总长和总督想在但以理的政务中找把柄控告他,却找不到任何把柄或过失,因为他诚实可靠,毫无过失。 5最后他们说:“除非我们从但以理上帝的律法下手,否则找不到指控他的把柄。”

6于是,这些总长和总督齐来见王,说:“愿大流士王万岁! 7所有总长、行政官、总督、谋士和省长都认为王应该颁布诏书并实施一道禁令,三十天内,任何人不得向王以外的神明或人祷告,违者必被扔进狮子坑。 8王啊,求你颁布并签署这道禁令,使之不可更改,正如玛代人和波斯人的律令是不可更改的。” 9于是大流士王签署了这道禁令。

10但以理知道王签署禁令后,就回到家里,他楼上房间的窗户朝向耶路撒冷。他像往常一样每日三次跪下向上帝祷告、感恩。 11那些官员一同来了,发现但以理向他的上帝祷告、祈求, 12便去见王,提及王的禁令,说:“王啊,你不是签署禁令,三十天内,任何人不得向王以外的神明或人祷告,违者必被扔进狮子坑吗?”王说:“确有此事,按照玛代人和波斯人的律令,这禁令不可更改。” 13他们对王说:“王啊,被掳来的犹大但以理不理会你和你的禁令,仍一日三次向他的上帝祈祷。” 14王听了这些话,十分愁烦,一心想救但以理,直到日落都在筹划解救之道。 15那些人齐来见王,说:“王啊,要知道按照玛代人和波斯人的律令,王颁布的禁令和律例是不可更改的。”

16王便下令把但以理带来扔进狮子坑。他对但以理说:“愿你一直事奉的上帝拯救你!” 17有人搬来一块石头封住坑口,王用他和大臣的印加封,使惩办但以理的事不可更改。 18王回宫后,整夜禁食,拒绝娱乐,无法入睡。

19次日黎明,王起来匆忙赶往狮子坑, 20到了坑边,凄声呼喊但以理:“永活上帝的仆人但以理啊,你一直事奉的上帝有没有救你脱离狮子的口?” 21但以理对王说:“愿王万岁! 22我的上帝差遣天使封住了狮子的口,不让它们伤害我,因为我在上帝面前是清白的。王啊,我在你面前也没有过错。” 23王非常高兴,便命人把但以理从坑中拉上来。于是,但以理从坑中被拉了上来,他因为信靠他的上帝,身上毫无损伤。 24王下令把那些恶意控告但以理的人及其儿女妻子都带来,扔进狮子坑。他们还没到坑底,狮子便扑上去,咬碎了他们的骨头。

25后来,大流士王传谕境内的各族、各邦、各语种的人,说:“愿你们大享平安! 26我下令,我统治的国民都要敬畏但以理的上帝,

“因为祂是永活长存的上帝,

祂的国度永不灭亡,

祂的统治直到永远。

27祂庇护、拯救,

在天上地下行神迹奇事,

但以理脱离狮子的口。”

28因此,在大流士波斯塞鲁士执政期间,但以理凡事亨通。

Kiswahili Contemporary Version

Danieli 6:1-28

Danieli Katika Tundu La Simba

16:1 Dan 5:31; Es 1:1Ilimpendeza Dario kuteua wakuu 120 kutawala katika ufalme wake wote, 26:2 Dan 2:48-49; Mit 3:35; Dan 5:12-14; 1:20pamoja na wasimamizi watatu juu yao, ambao mmoja wao alikuwa Danieli. Wakuu walitoa hesabu kwa hao wasimamizi ili mfalme asipate hasara. 36:3 Es 10:3; Mwa 41:41; Mit 3:35; Dan 5:12-14; 1:20Basi Danieli alijidhihirisha, miongoni mwa wasimamizi na wakuu kwa sifa zake za kipekee hata mfalme akapanga kumweka juu ya ufalme wote. 46:4 Yer 20:10Walipofahamu hilo, wakuu na wasimamizi wakajaribu kutafuta sababu za kumshtaki Danieli kuhusu usimamizi wake wa shughuli za serikali, lakini hawakuweza kufanikiwa. Hawakuweza kupata kosa kwake, kwa sababu alikuwa mwaminifu, wala hakupatikana na upotovu au uzembe. 56:5 Mdo 24:13-16Mwishoni watu hawa walisema, “Kamwe hatutapata msingi wa mashtaka dhidi ya huyu Danieli isipokuwa iwe inahusiana na sheria ya Mungu wake.”

66:6 Neh 2:3; Dan 2:4Basi wasimamizi na wakuu wakaingia kwa mfalme kama kikundi wakasema, “Ee Mfalme Dario, uishi milele! 76:7 Dan 3:2; Za 59:3; 64:2-6; Dan 3:6Wasimamizi wa ufalme, wasaidizi, wakuu, washauri na watawala wote wamekubaliana kwamba mfalme atoe sheria na kukazia amri kuwa yeyote atakayetoa dua kwa mungu au mwanadamu yeyote katika muda huu wa siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, ee mfalme, atupwe ndani ya tundu la simba. 86:8 Es 1:19Sasa, ee mfalme, toa amri na uiandike ili isiweze kubadilishwa: kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.” 96:9 Dan 9:23; Eze 2:1; Dan 9:23Hivyo Mfalme Dario akaiweka amri hiyo katika maandishi.

106:10 1Fal 8:29; Mdo 5:29; Za 95:6; Mt 6:6Basi Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alikwenda nyumbani kwenye chumba chake cha ghorofani ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Akapiga magoti na kuomba mara tatu kwa siku, akimshukuru Mungu wake kama alivyokuwa akifanya mwanzoni. 116:11 1Fal 8:48-50; Za 55:17; 1The 5:17-18Ndipo watu hawa wakaenda kama kikundi na kumkuta Danieli akiomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya msaada. 126:12 Es 1:19; Dan 3:8-12Basi wakaenda kwa mfalme na kusema naye kuhusu amri ya mfalme: “Je, hukutangaza amri kwamba kwa muda huu wa siku thelathini zijazo mtu yeyote ambaye atamwomba mungu au mwanadamu yeyote isipokuwa wewe, ee mfalme, angetupwa ndani ya tundu la simba?”

Mfalme akajibu, “Amri ndivyo ilivyo, kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi, ambazo haziwezi kubatilishwa.”

136:13 Eze 14:14; Dan 2:25; Es 3:8; Dan 3:12Ndipo wakamwambia mfalme, “Danieli, ambaye ni mmoja wa mahamisho kutoka Yuda, hakuheshimu, ee mfalme, wala hajali amri uliyoiweka kwa maandishi. Bado anaomba mara tatu kwa siku.” 146:14 Dan 3:13; Mk 6:26Wakati mfalme aliposikia hili, akahuzunika mno. Akakusudia kumwokoa Danieli, hivyo akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua.

156:15 Es 8:8Ndipo wale watu wakamwendea mfalme kama kikundi na kumwambia, “Ee mfalme, kumbuka kwamba kulingana na sheria ya Wamedi na Waajemi, hakuna amri wala sheria ambayo mfalme ameitoa inayoweza kubadilishwa.”

166:16 Ay 5:19; 2Kor 1:10; Za 97:10; 37:39-40Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, na wakamtupa ndani ya tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako unayemtumikia daima na akuokoe!”

176:17 Mt 27:66; Mao 3:536:17 Dan 4:3; 3:29Jiwe likaletwa na kuwekwa kwenye mdomo wa tundu, naye mfalme akalitia muhuri kwa pete yake mwenyewe pamoja na kwa pete za wakuu wake, ili hali ya Danieli isiweze kubadilishwa. 186:18 2Sam 12:17; Dan 3:10; Es 6:1; Dan 2:1Kisha mfalme akarudi kwenye jumba lake la kifalme, naye usiku kucha hakula chakula wala kutumia viburudisho alivyoletewa. Lakini hakuweza kulala.

19Asubuhi na mapema, mfalme akaondoka na kuharakisha kwenda kwenye tundu la simba. 206:20 Dan 3:17; Yer 32:17; Mwa 18:14Wakati alipokaribia lile tundu, akamwita Danieli kwa sauti ya uchungu, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa kwa simba?”

216:21 Neh 2:3; Dan 2:4; 3:9Danieli akajibu, “Ee mfalme, uishi milele! 226:22 Dan 3:23-28; Mwa 32:1; Za 91:11-13; Ebr 11:33; Mdo 12:11; 2Tim 4:17Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.”

236:23 Dan 3:27; Mk 16:18; Isa 12:2; 1Nya 5:20Mfalme akafurahi mno, naye akatoa amri Danieli atolewe kutoka kwa lile tundu. Danieli alipotolewa kutoka kwa lile tundu, hakukutwa na jeraha lolote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake.

246:24 Kum 19:18-19; Es 7:9-10; 2Fal 14:6; Isa 38:13; Kum 24:16; 2Fal 14:6Kwa amri ya mfalme, wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote.

256:25 Dan 3:4; 4:1Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa, na watu wa kila lugha katika nchi yote:

“Ninyi na mstawi sana!

266:26 Dan 4:34; Es 8:17; Dan 2:44; Za 99:1-3; Yos 2:11; 3:10; Dan 12:7; Za 5:7; Dan 3:26; Yer 10:10; Ufu 1:18“Natoa amri hii, kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu, lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli.

“Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai,

naye hudumu milele,

ufalme wake hautaangamizwa,

nao utawala wake hauna mwisho.

27Huponya na kuokoa;

hufanya ishara na maajabu

mbinguni na duniani.

Amemwokoa Danieli

kutoka nguvu za simba.”

286:28 2Nya 36:22; Dan 1:21; 5:1, 28Hivyo Danieli akastawi wakati wa utawala wa Dario, na utawala wa Koreshi Mwajemi.