以西结书 1 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 1:1-28

以西结的异象

1第三十年四月五日,我正在迦巴鲁河畔被掳的人当中,那时天开了,我看见了上帝的异象。 2那是约雅斤王被掳第五年的四月五日, 3就在迦勒底人境内的迦巴鲁河畔,耶和华的话传给了布西的儿子以西结祭司,耶和华的手按在他身上。

4在异象中,我看见一阵狂风从北方刮来,有一大朵云闪耀着火光,四周环绕着灿烂的光芒,火的中心像发光的金属。 5火中有四个像人形的活物, 6每个活物有四张脸和四个翅膀。 7他们的腿是直的,脚如同牛犊的蹄,都亮如磨光的铜。 8四面的翅膀下都有人的手,四个活物都有脸和翅膀, 9翅膀彼此相连。他们移动时不必转身,各朝前面移动。 10四个活物的脸是这样的:正面是人的脸,右面是狮子的脸,左面是牛的脸,后面是鹰的脸。 11他们的翅膀向上展开,每个活物的一对翅膀与两侧活物的翅膀相连,另外一对翅膀遮蔽身体。 12每个活物都往前直行,耶和华的灵往哪里去,他们也往哪里去,移动时不用转身。 13四个活物的形象如燃烧的火炭,又像火把。活物之间有火上下移动,非常明亮,从火中发出闪电。 14这些活物像闪电一样往来飞驰。

15当我观看这些活物的时候,发现每个活物旁边的地上都有一个轮子。 16四个轮子的形状和结构都一样,好像轮套轮,如同闪耀的绿宝石。 17他们可以向四面移动,移动时轮子不必转向。 18轮圈高而可畏,周围布满了眼睛。 19活物行走,轮子也在旁边行走;活物上升,轮子也上升。 20灵往哪里去,活物也往哪里去,轮子也跟着往哪里去,因为活物的灵在轮子里。 21活物行走,轮子也行走;活物站立不动,轮子也站立不动;活物上升,轮子也跟着上升,因为活物的灵在轮子里。

22活物的头上好像铺展着茫茫的穹苍,如同顶着耀眼的水晶。 23穹苍下四个活物伸展翅膀,彼此相对,各用另两个翅膀遮蔽身体。 24他们移动时,我听见他们翅膀发出的响声如洪涛之声,既像全能者的声音,又像军队的呐喊。活物站住的时候,便将翅膀垂下。 25他们站立垂下翅膀时,有声音从他们头顶的穹苍之上传来。

26在他们头顶的穹苍之上仿佛有蓝宝石的宝座,有一位形状像人的高坐在宝座上。 27我看到祂的腰部以上好像烧红发亮的金属,好像有火四面环绕。腰部以下如同火焰。祂周围有耀眼的光辉, 28仿佛雨天云中的彩虹。

这是耶和华荣耀的形象。我一看见,便俯伏在地,随后听见有说话的声音。

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 1:1-28

Viumbe Hai Na Utukufu Wa Bwana

11:1 Kum 21:10; Mt 3:16; Eze 11:24-25; Mdo 7:56; Kut 24:10Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, wakati nilipokuwa miongoni mwa hao waliokuwa uhamishoni kando ya Mto Kebari, mbingu zilifunguka nami nikaona maono ya Mungu.

21:2 2Fal 24:15; 24:15; 24:12Katika siku ya tano ya mwezi, ilikuwa mwaka wa tano wa kuhamishwa kwa Mfalme Yehayakini, 31:3 2Fal 3:15; Isa 8:11; 2Pet 1:21; Eze 24:24; 3:14, 22; 33:22neno la Bwana lilimjia Ezekieli kuhani, mwana wa Buzi, kando ya Mto Kebari, katika nchi ya Wakaldayo. Huko mkono wa Bwana ulikuwa juu yake.

41:4 Yer 1:14; 23:19; Eze 8:2; Ay 38:1Nilitazama, nikaona dhoruba kubwa ikitoka kaskazini, wingu kubwa sana pamoja likiwa na umeme wa radi likiwa limezungukwa na mwanga mkali. Katikati ya huo moto kulikuwa kama rangi ya manjano ya chuma kinapokuwa ndani ya moto. 51:5 Isa 6:2; Ufu 4:6; Dan 7:13Katika ule moto kulikuwa na kitu kinachofanana na viumbe vinne vyenye uhai. Katika kuonekana kwake vilikuwa na umbo mfano wa mwanadamu, 61:6 Eze 10:14lakini kila kimoja kilikuwa na nyuso nne na mabawa manne. 71:7 Dan 10:6; Ufu 1:15; Eze 40:3Miguu yao ilikuwa imenyooka, nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za miguu ya ndama, nazo zilimetameta kama shaba iliyosuguliwa. 81:8 Eze 10:8; 10:18, 21Chini ya mabawa yao katika pande zao nne walikuwa na mikono ya mwanadamu. Wote wanne walikuwa na nyuso na mabawa, 91:9 Eze 10:22; 10:11; 1:11nayo mabawa yao yaligusana. Kila mmoja alikwenda kuelekea mbele moja kwa moja, hawakugeuka walipokuwa wanatembea.

101:10 Eze 10:4; Ufu 4:7; Hes 2:10Kuonekana kwa nyuso zao kulikuwa hivi: Kila mmoja wa wale wanne alikuwa na uso wa mwanadamu na kwa upande wa kulia kila mmoja alikuwa na uso wa simba, upande wa kushoto alikuwa na uso wa ngʼombe pia kila mmoja alikuwa na uso wa tai. 111:11 Isa 6:2Hivyo ndivyo zilivyokuwa nyuso zao. Mabawa yao yalikunjuliwa kuelekea juu, kila mmoja alikuwa na mabawa mawili ambayo kila moja liligusa bawa la mwenzake kila upande na mabawa mengine mawili yakifunika mwili wake. 121:12 Eze 10:16-19; 10:22Kila mmoja alikwenda kuelekea mbele moja kwa moja. Popote roho alipotaka kwenda, ndipo walipokwenda pasipo kugeuka. 131:13 Ufu 4:5; Mt 28:3; 2Sam 22:9Kuonekana kwa vile viumbe hai katikati kulikuwa kama makaa ya mawe yanayowaka au kama mienge. Moto ule ulikuwa ukienda mbele na nyuma katikati ya vile viumbe, ulikuwa na mwangaza mkali na katikati ya ule moto kulitoka kimulimuli kama umeme wa radi. 141:14 Zek 4:10; Za 29:7; Amu 13:20Vile viumbe vilipiga mbio kwenda na kurudi, kama vimulimuli vya umeme wa radi.

151:15 Eze 3:13; 10:2; Dan 7:9Nilipokuwa nikitazama vile viumbe hai, niliona gurudumu moja juu ya ardhi kando ya kila kiumbe kikiwa na nyuso zake nne. 161:16 Dan 10:6; Kut 28:20Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa hayo magurudumu na muundo wake: yalingʼaa kama zabarajadi, nayo yote manne yalifanana. Kila gurudumu lilikuwa na gurudumu jingine ndani yake. 171:17 Eze 1:12; 1:19Yalipokwenda yalielekea upande wowote wa pande nne walipoelekea wale viumbe, magurudumu hayakuzunguka wakati viumbe vile vilipokwenda. 181:18 Mit 15:3; Eze 10:12; Ufu 4:6Kingo zake zilikuwa ndefu kwenda juu na za kutisha, nazo zote nne zilijawa na macho pande zote.

191:19 Eze 1:16, 17Vile viumbe hai vilipokwenda, magurudumu yaliyokuwa kando yao yalisogea na wakati hivyo viumbe hai vilipoinuka kutoka ardhini magurudumu nayo yaliinuka. 201:20 Eze 1:12; 10:17Mahali popote roho alipokwenda wale viumbe nao walikwenda, nayo magurudumu yaliinuka pamoja navyo, kwa sababu roho ya vile viumbe hai alikuwa ndani ya hayo magurudumu. 211:21 Eze 10:9, 12, 17Wakati viumbe vile viliposogea, nayo magurudumu yalisogea, viumbe viliposimama kimya, nayo pia yalisimama kimya, viumbe vilipoinuka juu ya nchi magurudumu yaliinuliwa pamoja navyo kwa kuwa roho ya hivyo viumbe hai alikuwa ndani ya hayo magurudumu.

221:22 Eze 10:1, 5Juu ya vichwa vya hao viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa eneo lililokuwa wazi, lililokuwa angavu kabisa na lenye kutisha. 23Chini ya hiyo nafasi mabawa yao yalitanda moja kuelekea jingine, kila mmoja alikuwa na mabawa mengine mawili yaliyofunika mwili wake. 241:24 2Fal 7:6; Ufu 14:2; Dan 10:6; Za 18:13; 46:3; Eze 10:5; 43:2; Ufu 19:6Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi,1:24 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao.

25Ndipo ikaja sauti toka juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, waliposimama mabawa yao yakiwa yameshushwa. 261:26 Kut 24:10; Eze 10:1; Ufu 1:13; Isa 6:1; 1Fal 22:19; Yer 3:17Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu. 271:27 Eze 8:2Nikaona kwamba kutokana na kile nilichoona kama kiuno chake kuelekea juu alionekana kama chuma inayowaka kana kwamba imejaa moto na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto na mwanga mkali ulimzunguka. 281:28 Mwa 9:13; Ufu 10:1; 4:2; 1:17; Hes 12:8; Kut 24:16; Dan 8:17; Hes 14:5; Lk 2:9; Kut 16:7Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mngʼao uliomzunguka.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa utukufu wa Bwana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.