以赛亚书 28 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以赛亚书 28:1-29

北国必遭审判

1以法莲酒徒引以为荣的华冠有祸了!

它坐落在醉酒者肥美的山谷顶上,

它的荣美如将残之花。

2看啊,主有一位强壮有力的人,

他像冰雹和带来毁灭的暴风,

又像汹涌泛滥的洪水,

他必把华冠摔在地上。

3以法莲酒徒引以为荣的华冠必被践踏在脚下。

4那荣美的将残之花在肥沃的山谷之巅,

它必像夏季到来之前早熟的无花果,

人一看见它就把它摘下吞掉。

5到那日,万军之耶和华必作祂余民的荣冠和华冕,

6祂必使审判官公正断案,

赐力量给守城退敌之人。

7但祭司和先知也因醉酒而摇摇晃晃,

因烈酒而东倒西歪。

他们因烈酒而摇摇晃晃、

酩酊大醉,东倒西歪,

他们错解异象,糊涂判案。

8桌子上到处都是呕吐之物,

一片狼藉。

9他们抱怨说:

“祂想教导谁知识呢?

祂想把信息解释给谁呢?

是刚刚断奶、离开母怀的婴孩吗?

10因为祂的教导只是命命令令、命命令令、律律例例、律律例例、这里一点、那里一点。”

11因此,耶和华必用外族人的口和陌生的语言来教训他们。

12耶和华曾对他们说:

“这是安歇之地,

让疲乏的人安歇吧。

这是安歇之地。”

他们却不肯听。

13所以,对他们来说,

耶和华的话成了命命令令、命命令令、律律例例、律律例例、这里一点、那里一点,

以致他们走路时仰面跌倒,摔伤,落网,被捉。

14因此,你们这些好讥讽、在耶路撒冷统管百姓的人啊,

要听耶和华的话。

15你们说:

“我们已经和死亡立约,

与阴间结盟。

势不可挡的灾难席卷而来时,

我们会安然无恙,

因为我们以谎言为庇护所,

以诡诈为藏身处。”

16所以主耶和华说:

“看啊,我要在锡安放一块基石,

一块经过考验的石头,

一块根基稳固的宝贵房角石,

信靠的人必不会恐慌。

17我必以公平为准绳,

以公义作线锤。

冰雹必砸碎你们虚谎的庇护所,

洪水必淹没你们的藏身处。

18你们和死亡所立的约必被废弃,

与阴间的结盟必不能长久。

势不可挡的灾难席卷而来时,

你们必遭践踏。

19灾难必不分昼夜、日复一日地袭来,

每次袭来都必掳掠你们。”

明白这信息的人都必惊恐万分。

20你们的床太小,不能舒身;

你们的被子太窄,不足裹身。28:20 此处的床和被子象征他们虚假的安全感。

21耶和华必像在毗拉心山一样挺身而出,

像在基遍谷一样发怒,

要完成祂奇异的作为,

成就祂不寻常的工作。

22现在你们不要再讥讽了,

以免你们的捆索更沉重,

因为我已从主——万军之耶和华那里听到毁灭全国的谕旨。

23你们要侧耳听我的声音,

留心听我的话语。

24难道农夫会一直耕地而不撒种吗?

难道他会一直犁地、耙地吗?

25他整平土地之后,

难道不种小茴香、大茴香,

按行种小麦,

在合适的地方种大麦,

在田边种粗麦吗?

26因为他的上帝指点他,教导他耕种之道。

27打小茴香不用大槌,用木棍;

打大茴香不用石磙,用木棒。

28做饼的粮食要磨碎,

没有人会不停地在场上碾压粮食。

马拉着石磙在场上轧过,

也不会把粮食磨碎。

29这些知识都是万军之耶和华所赐的,

祂有奇妙的谋略和伟大的智慧。

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 28:1-29

Ole Wa Efraimu

128:1 Isa 7:2; Law 10:9; Amo 6:6; Isa 10:5; 9:9; Hos 7:5; Isa 5:11; 8:7Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,

kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:

kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!

228:2 Isa 30:30; 40:10; Yos 10:11; Eze 13:11; Isa 29:6; 8:7; Dan 9:26Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.

Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,

kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,

atakiangusha chini kwa nguvu.

328:3 Ay 40:12; Isa 5:5Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,

kitakanyagwa chini ya nyayo.

428:4 Wim 2:13; Nah 3:12; Hos 9:10Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,

litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:

mara mtu aionapo, huichuma na kuila.

528:5 Zek 9:16; Eze 21:26; Isa 10:20; 1:9; 29:18; Yer 13:18; Eze 16:12; Isa 62:3Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote

atakuwa taji la utukufu,

taji zuri la maua

kwa mabaki ya watu wake.

628:6 Amu 9:44-45; 2Sam 14:20; 2Nya 32:8; Yn 5:30; Isa 11:2-4Atakuwa roho ya haki

kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,

chanzo cha nguvu

kwa wale wazuiao vita langoni.

728:7 Law 10:9; Isa 56:10-12; Efe 5:18; Za 107:27; Isa 24:2; 3:12; 22:13; 9:15Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,

wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:

Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,

wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;

wanapepesuka wanapoona maono,

wanajikwaa wanapotoa maamuzi.

828:8 Yer 48:26Meza zote zimejawa na matapishi

wala hakuna sehemu hata ndogo

isiyokuwa na uchafu.

928:9 Yer 6:10; 1Pet 2:2; Za 32:8; Ebr 5:12-13; Yer 31:34; Isa 30:20; 48:17; 54:13“Yeye anajaribu kumfundisha nani?

Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?

Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?

Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini?

1028:10 Isa 29:13Kwa maana ni:

Amri juu ya amri, amri juu ya amri,

kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;

hapa kidogo, kule kidogo.”

1128:11 Yer 5:15; 1Kor 14:21; Mwa 11:7; Eze 3:5; Isa 33:19Sawa kabisa, kwa midomo migeni

na kwa lugha ngeni,

Mungu atasema na watu hawa,

1228:12 Yos 1:13; Mt 11:28-29; 2Nya 14:7; Kut 14:14; Ay 11:18; Isa 11:10wale ambao aliwaambia,

“Hapa ni mahali pa kupumzika,

waliochoka na wapumzike,”

na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,”

lakini hawakutaka kusikiliza.

1328:13 Mt 21:44; Isa 8:14-15Hivyo basi, neno la Bwana kwao litakuwa:

Amri juu ya amri, amri juu ya amri,

kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni,

hapa kidogo, kule kidogo:

ili waende na kuanguka chali,

wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.

1428:14 Isa 1:10; 2Nya 36:16Kwa hiyo sikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau

mnaotawala watu hawa wa Yerusalemu.

1528:15 Dan 11:22; Isa 9:15; 10:26; Ay 5:23; Isa 8:19; Amu 9:35; Isa 29:15; Yer 23:24Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,

tumefanya mapatano na kuzimu.

Wakati pigo lifurikalo litakapopita,

haliwezi kutugusa sisi,

kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu

na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”

1628:16 Zek 12:3; Efe 2:20; Rum 9:33; 1Pet 2:6; Isa 54:4; 14:32; Za 118:22; Isa 8:14-15; Dan 2:34-45; Mdo 4:11; Yer 51:26; 1Kor 3:11Kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo:

“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,

jiwe lililojaribiwa,

jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti.

Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.

1728:17 Isa 5:16; Za 11:7; 2Fal 21:13; Yos 10:11Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia

na uadilifu kuwa timazi;

mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,

nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha.

1828:18 Isa 63:18; Dan 8:13; Isa 7:7Agano lenu na kifo litabatilishwa,

patano lenu na kuzimu halitasimama.

Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,

litawaangusha chini.

1928:19 2Fal 24:2; Ay 18:11; Za 5:3Kila mara lijapo litawachukua,

asubuhi baada ya asubuhi,

wakati wa mchana na wakati wa usiku,

litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.”

Kuuelewa ujumbe huu

utaleta hofu tupu.

2028:20 Isa 59:6Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake,

nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno

mtu hawezi kujifunikia.

2128:21 2Sam 5:20; Mwa 38:29; 1Nya 14:11-16; Lk 19:41-44; Yos 9:3; Isa 65:7Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu,

ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni:

ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu,

ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni.

2228:22 Isa 10:22; Yer 29:18; 2Nya 36:16; Mao 2:15; Sef 2:15Sasa acheni dharau zenu,

la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi.

Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia

habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.

2328:23 Isa 32:9Sikilizeni msikie sauti yangu,

tegeni masikio na msikie niyasemayo.

2428:24 Mhu 3:2Wakati mkulima alimapo ili apande,

je, hulima siku zote?

Je, huendelea kubomoa ardhi

na kusawazisha udongo?

2528:25 Kut 9:32; Mt 23:23; Eze 4:9Akiisha kusawazisha shamba,

je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira?

Je, hapandi ngano katika sehemu yake,

shayiri katika eneo lake,

na nafaka nyingine katika shamba lake?

2628:26 Za 94:10Mungu wake humwelekeza

na kumfundisha njia iliyo sahihi.

2728:27 Isa 21:10; Ay 41:30; Isa 10:5Iliki haipurwi kwa nyundo,

wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira;

iliki hupurwa kwa fimbo,

na jira kwa ufito.

2828:28 Isa 21:10Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate,

kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima.

Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake,

farasi wake hawasagi.

2928:29 Yer 32:19; Za 92:5; Rum 11:33; Isa 9:5Haya yote pia hutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,

mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.