以西结书 38 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 38:1-23

对歌革的预言

1耶和华对我说: 2“人子啊,你要面向玛各地区的歌革,就是米设土巴的首领,说预言斥责他, 3告诉他,主耶和华这样说,‘米设土巴的首领歌革啊,我要与你为敌。 4我要把你调转过来,用钩子钩住你的腮,把你和你那些全副武装、拿着大小盾牌、挥动刀剑的军队、马匹和骑兵都拖出来。 5你的军队中有拿着盾牌、戴着头盔的波斯人、古实人和人, 6还有歌篾及其全军和从遥远的北方来的陀迦玛及其全军。许多国家的军队都与你在一起。

7“‘你和聚集到你那里的联军都要时刻预备好,你要做他们的统帅。 8再过多日,你必被征召出战。在以后的岁月,你将去攻打一片已从战争中恢复的土地,以色列久已荒凉的山上有从各国招聚回来的百姓。他们从列国中被领回来,如今都在那里安然居住。 9你和你的军队以及各国的联军一起上来,如暴风来临,又如密云覆盖大地。’

10“‘主耶和华说:那时你必心起歹念,筹划恶谋。 11你必说,我要攻打那没有围墙保护的乡村,毁灭那毫无戒备、在无墙无门无闩之地安然居住的百姓。 12我要抢掠他们的财物,下手攻击那曾是废墟的城邑和从列国归来的百姓。他们住在世界的中心,牲畜货物甚多。 13示巴人、底但人以及他施的客商和首领都必问:你是来抢掠吗?你聚集军队是来抢夺金银财宝,掳掠牲畜和货物吗?’

14“因此,人子啊,你要说预言告诉歌革,主耶和华这样说,‘当我的以色列子民安然居住的时候,难道你会不知道吗? 15你召集各国联军,组成庞大的军队,骑着马从遥远的北方来。 16歌革啊,你必如密云一样遮天蔽日,前来攻击我的以色列子民。将来,我要领你来攻击我的土地,我要在列国面前借着你彰显我的圣洁,使他们认识我。’

17“主耶和华说,‘歌革啊,我从前借我的仆人——以色列的先知所预言的那位就是你,那时他们曾多年预言我要领你上来攻击以色列18歌革上来攻击以色列的时候,我必发烈怒。这是主耶和华说的。 19我要在义愤和烈怒中宣告,那天在以色列必有大地震。 20海里的鱼,空中的鸟,田野的走兽,地上的一切爬虫和人类都要在我面前战栗。山岭必倒塌,悬崖必崩裂,墙垣必坍塌。 21我要在我的山岭上叫刀剑攻击歌革,使他们自相残杀。这是主耶和华说的。 22我要用瘟疫和杀戮惩罚他,将暴雨、冰雹、烈火和硫磺倾倒在他及其军队和随从的列邦身上。 23我要彰显我的伟大和圣洁,使列国的人都认识我。这样他们就知道我是耶和华。’

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 38:1-23

Unabii Dhidi Ya Gogu

1Neno la Bwana likanijia kusema: 238:2 Mwa 10:2; Eze 27:13; Ufu 20:8; Eze 39:11“Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali, tabiri dhidi yake 338:3 Eze 39:1na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali. 438:4 2Fal 19:28; Isa 43:17; Dan 11:40; Eze 23:12; 29:4; 39:2Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao. 538:5 Eze 27:10-14; Mwa 10:6Uajemi, Kushi38:5 Kushi ni Ethiopia. na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma, 638:6 Mwa 10:2-3; Eze 32:30pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe.

738:7 Isa 8:9; 8:10; Yer 46:3, 4, 14; 51:12“ ‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe. 838:8 Isa 11:11; 24:22; Kum 4:30; Yer 23:6; Yoe 3:1; Eze 28:26Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo, utaivamia nchi ile ambayo imepona kutoka vita, ambayo watu wake walikusanywa kutoka mataifa mengi kuja katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama. 938:9 Isa 25:4; 28:2; Yer 4:13; Yoe 2:2; Ufu 20:8Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu.

1038:10 Yer 17:10; Za 36:4; Mik 2:1“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya. 1138:11 Yer 49:31; Zek 2:4; Amu 18:7-27; Mwa 34:25Utasema, “Nitapigana vita na nchi ambayo vijiji vyake havina maboma. Nitawashambulia watu wanaoishi kwa amani na wasiotarajia vita: wote wanaishi bila maboma na bila malango na makomeo. 12Nitateka mateka na kuchukua nyara mali za wale waliorudi kuishi katika mahame na wale watu waliokusanywa kutoka kwa mataifa, ambao sasa wana mifugo na mali nyingi, wanaoishi katikati ya nchi.” 1338:13 Mwa 10:7; Eze 27:22; Isa 33:23; Yer 15:13; Mwa 25:3; Isa 10:6Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyangʼanya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’

1438:14 Law 25:18; Yer 16:15; Zek 2:5“Kwa hiyo, mwanadamu, tabiri na umwambie Gogu: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile, watu wangu Israeli watakapokuwa wanaishi salama, Je, wewe mwenyewe hutalijua hilo? 1538:15 Eze 39:2; Ufu 20:8; Eze 32:30Utakuja kutoka kwako huko kaskazini ya mbali, ukiwa pamoja na mataifa mengi, wote wakiwa wamepanda farasi, kundi kubwa, jeshi kuu. 1638:16 Eze 38:9; 38:8; Kut 14:4; Eze 36:23; 39:21Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.

17“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, wewe si yule niliyenena juu yako katika siku za zamani kwa kupitia kwa watumishi wangu manabii wa Israeli? Wakati ule walitabiri kwa miaka mingi kwamba ningekuleta upigane nao. 18Hili ndilo litakalotokea katika siku ile: Gogu atakaposhambulia nchi ya Israeli, hasira yangu kali itaamka, asema Bwana Mwenyezi. 1938:19 Za 18:7; Hag 2:6, 21; Isa 29:23; Yoe 3:11; Law 10:3Katika wivu wangu na ghadhabu yangu kali ninasema kuwa wakati ule patakuwepo tetemeko kuu katika nchi ya Israeli. 2038:20 Za 76:8; Yer 4:24; Kut 15:14; Isa 42:15; Ay 14:18; Hos 4:3Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini. 2138:21 Isa 66:16; Kut 9:18; Ufu 16:21; Yer 25:31; Amu 7:22; 1Sam 14:20; Hag 2:22Nitaita upanga vita dhidi ya Gogu juu ya milima yangu yote, asema Bwana Mwenyezi. Upanga wa kila mtu utakuwa dhidi ya ndugu yake. 2238:22 Yer 25:31; Eze 36:5; 14:19; Kut 9:18; Za 18:12; Ufu 16:21Nitatekeleza hukumu juu yake kwa tauni na kwa umwagaji wa damu. Nitaifanya mvua ya mafuriko kunyesha, mvua ya mawe na moto wa kiberiti juu yake na juu ya vikosi vyake na juu ya mataifa mengi walio pamoja naye. 2338:23 Eze 20:42; 36:23; 37:6Nami hivyo ndivyo nitakavyoonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’