但以理书 1 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

但以理书 1:1-21

但以理被掳到巴比伦

1犹大约雅敬执政第三年,巴比伦尼布甲尼撒前来围攻耶路撒冷2主将犹大约雅敬及上帝殿中的部分器具交在他手中。他把器具掳到巴比伦1:2 巴比伦”希伯来文是“示拿”,巴比伦的别称。的神庙,放在他神明的库房里。

3王吩咐太监长亚施毗拿以色列的王室贵族中选一些人, 4即毫无残疾、相貌英俊、学问渊博、知识丰富、聪慧善学、能在王宫服侍的青年,教他们迦勒底的语言和文字。 5王安排他们每日享用一份御用的膳食和酒。他们要受教养三年,期满后好在王身边供职。 6被选的人中有犹大族的但以理哈拿尼雅米沙利亚撒利雅7太监长给他们起了名字:称但以理伯提沙撒哈拿尼雅沙得拉米沙利米煞亚撒利雅亚伯尼歌

8然而,但以理决心不用王的膳食和酒,以免玷污自己。他请求太监长准许他不玷污自己。 9上帝使但以理得到太监长的恩待和同情。 10不过,太监长对但以理说:“我惧怕我主我王,因为这是他安排给你们的饮食。如果他看见你们比同龄的青年瘦弱,如何是好?你们会使我在王面前人头难保。” 11但以理便对太监长派来监管他、哈拿尼雅米沙利亚撒利雅的人说: 12“求你试试看,十天内只让仆人们吃素菜、喝清水, 13然后比较一下我们的面貌和那些用御膳的青年的面貌,看了之后再作决定。” 14监管同意试他们十天。 15十天后,但以理和他三个朋友看上去比那些用御膳的青年更俊美健康。 16于是,监管撤去了安排给他们的膳食和酒,只给他们素菜。

17上帝使这四个青年精通各样学问和知识。但以理能明白各种异象和梦兆。 18到了尼布甲尼撒王规定青年们进宫的日子,太监长便带他们去见王。 19王与他们谈话,发现无人比得上但以理哈拿尼雅米沙利亚撒利雅,便把他们留在身边供职。 20王询问他们各样的事,发现他们的智慧和聪明比全国的术士和巫师高十倍。 21直到塞鲁士王元年,但以理仍在那里供职。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Danieli 1:1-21

Mafunzo Ya Danieli Huko Babeli

11:1 Yer 28:4; 35:11; 46:2; 2Nya 36:6; 2Fal 24:1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja akazingira Yerusalemu kwa jeshi. 21:2 2Nya 36:7; Yer 27:19; Zek 5:5-11; 2Fal 24:13Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza, pamoja na baadhi ya vyombo kutoka Hekalu la Mungu. Hivi akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari, naye akaviweka nyumbani ya hazina ya mungu wake.

31:3 2Fal 20:18; Isa 39:7; Amu 8:18; Mdo 7:20-22; Mwa 39:6; Ezr 4:7Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa mfalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya mfalme na kutoka jamaa kuu, 4vijana wanaume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonyesha kipaji katika kila aina ya elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo. 51:5 Es 2:5-6, 9Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, na hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme.

61:6 Eze 14:14; Dan 2:17-25Baadhi ya hawa vijana walitoka Yuda: nao ni Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. 71:7 Dan 5:12; 10:1; Isa 39:7; Dan 3:12; 2:49; 2:26Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya: Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki, na Azaria akamwita Abednego.

81:8 Mwa 39:21; Mit 16:7; 1Fal 8:50; Eze 4:13-14Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii. 91:9 Mwa 39:21; Mit 16:7; 1Fal 8:50Basi Mungu alikuwa amemfanya huyo mkuu wa maafisa kuonyesha upendeleo na huruma kwa Danieli, 101:10 Ufu 2:10lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”

11Ndipo Danieli akamwambia mlinzi aliyeteuliwa na huyo mkuu wa maafisa kuwasimamia Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria, 121:12 Ufu 2:10“Tafadhali wajaribu watumishi wako kwa siku kumi. Usitupe chochote ila nafaka na mboga za majani1:12 Nafaka na mboga za majani, yaani zeroimu kwa Kiebrania, ina maana ya aina za ngano na shayiri, na jamii ya kunde kama maharagwe, dengu, choroko, n.k. tule, na maji ya kunywa. 13Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.” 141:14 Mhu 2:26; Yak 1:5; Dan 2:19, 30; 7:1; 8:1Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi.

151:15 Kut 23:25Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko yeyote kati ya wale vijana waliokula chakula cha mfalme. 16Hivyo mlinzi wao akaondoa chakula chao na divai yao waliopangiwa kula na kunywa, akawapa nafaka na mboga za majani badala yake.

171:17 1Fal 3:12; Ay 12:13; Mhu 2:26; Dan 2:23; Kol 1:9; Dan 5:11; Mdo 7:22Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.

18Mwisho wa muda uliowekwa na mfalme kuwaingiza kwake, mkuu wa maafisa akawaleta mbele ya Mfalme Nebukadneza. 191:19 Mwa 41:46Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme. 201:20 Es 2:15; Eze 28:3; Mwa 41:8; 1Fal 4:30; Dan 4:18; 2:13; 6:3Katika kila jambo la hekima na ufahamu kuhusu kile mfalme alichowauliza, aliwaona bora mara kumi zaidi kuliko waganga na wasihiri wote katika ufalme wake wote.

211:21 Dan 6:28; 2Nya 36:22; Dan 10:1Naye Danieli akabaki huko mpaka mwaka wa kwanza wa utawala wa Mfalme Koreshi.