Ezra 1:1-11, Ezra 2:1-67 NEN

Ezra 1:1-11

Koreshi Asaidia Watu Kurudi Kutoka Uhamishoni

1:1 Yer 29:10-14; Zek 1:12-16; 2Nya 36:22-23; Ezr 5:13; 7:27; Yer 25:12; Law 26:42Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Bwana lililosemwa na nabii Yeremia, Bwana aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:

1:2 Amu 4:10; Isa 44:28; Ezr 5:13; Za 72:11“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. 1:3 Kum 3:24; 2Sam 22:32; Za 86:10; Dan 6:26; 1Kor 8:6; Isa 37:16; Mk 12:32Yeyote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Bwana, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu. 1:4 Isa 10:20-22; Hes 15:3; Za 116:17; Ezr 3:7; 4:3Nao watu wa mahali popote wale walionusurika wanapoishi sasa, watu hao wampe fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, mbali na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”

1:5 2Nya 34:9; Neh 12:34; Hag 1:4; Flp 2:13; Mit 16:1Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu. Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari. 1:7 2Fal 24:13; Ezr 5:14; 6:5; 2Nya 36:7; Yer 52:17-19Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la Bwana, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalu la mungu wake. 1:8 Ezr 5:14; Hag 1:1; 1Nya 3:18Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda.

Hii ilikuwa ndio orodha ya vifaa:

masinia ya dhahabu yalikuwa 30masinia ya fedha yalikuwa 1,000vyetezo vya fedha vilikuwa 29mabakuli ya dhahabu yalikuwa 30mabakuli ya fedha yanayofanana yalikuwa 410vifaa vingine vilikuwa 1,000.

Kwa ujumla, kulikuwa na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.

Read More of Ezra 1

Ezra 2:1-67

Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni

(Nehemia 7:4-73)

2:1 2Nya 36:20; Neh 7:6; 11:3; 2Fal 24:16; 25:12; Ezr 5:8; 6:2; Es 1:1; 8:9Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2:2 1Nya 3:19; 6:14; Hag 2:4; Zek 3:1-10wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):

Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:

2:3 Ezr 10:25; Neh 3:25wazao wa Paroshi 2,172wazao wa Shefatia 3722:5 Neh 6:18wazao wa Ara 775wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812wazao wa Elamu 1,254wazao wa Zatu 945wazao wa Zakai 760wazao wa Bani 642wazao wa Bebai 623wazao wa Azgadi 1,2222:13 Ezr 8:13; 7:18wazao wa Adonikamu 666wazao wa Bigwai 2,056wazao wa Adini 454wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98wazao wa Besai 323wazao wa Yora 112wazao wa Hashumu 2232:20 Yos 9:17wazao wa Gibari 95

2:21 Mik 5:2; 1Nya 2:51; Rut 1:19; Mt 2:6; 2Sam 21:2; Mwa 35:19watu wa Bethlehemu 123watu wa Netofa 56watu wa Anathothi 128watu wa Azmawethi 42wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 7432:26 Yos 18:25; 1Sam 7:17; Yer 31:15wazao wa Rama na Geba 621watu wa Mikmashi 1222:28 Mwa 12:8watu wa Betheli na Ai 223wazao wa Nebo 52wazao wa Magbishi 1562:31 Ezr 2:7wazao wa Elamu ile ingine 1,254wazao wa Harimu 320wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 7252:34 Kum 34:3; 2Nya 28:15; 1Fal 16:34wazao wa Yeriko 345wazao wa Senaa 3,630

2:36 1Nya 9:10; 24:7Makuhani:

wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 9732:37 1Nya 24:14; Ezr 10:20wazao wa Imeri 1,0522:38 1Nya 9:12; Ezr 10:22wazao wa Pashuri 1,2472:39 1Nya 24:8wazao wa Harimu 1,017

2:40 Mwa 29:34; Hes 3:9; Ezr 3:9Walawi:

wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74

2:41 1Nya 15:16Waimbaji:

wazao wa Asafu 128

2:42 1Sam 3:15; 1Nya 9:17Mabawabu wa lango la Hekalu:

wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 139

2:43 1Nya 9:2Watumishi wa Hekalu:2:43 Yaani Wanethini (pia 2:58, 70).

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,

wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,

wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,

wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,

wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,

wazao wa Uza, Pasea, Besai,

wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,

wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

wazao wa Nesia na Hatifa.

2:55 1Fal 9:21Wazao wa watumishi wa Solomoni:

wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,

wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.

2:58 1Fal 9:21; Ezr 7:7; Yos 9:21-27; 1Nya 9:2Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392

2:59 Hes 1:18Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 652

2:61 2Sam 17:27; 1Fal 2:7Kutoka miongoni mwa makuhani:

Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

2:62 Hes 16:39-40; 3:10Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 2:63 Neh 8:9; Hes 18:9-11; Kut 28:30; Law 2:3-10Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 2:65 2Sam 19:35tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 2:66 Isa 66:20Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, ngamia 435 na punda 6,720.

Read More of Ezra 2