Ezra 1 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Ezra 1:1-11

Koreshi Asaidia Watu Kurudi Kutoka Uhamishoni

11:1 Yer 29:10-14; Zek 1:12-16; 2Nya 36:22-23; Ezr 5:13; 7:27; Yer 25:12; Law 26:42Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Bwana lililosemwa na nabii Yeremia, Bwana aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:

21:2 Amu 4:10; Isa 44:28; Ezr 5:13; Za 72:11“Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. 31:3 Kum 3:24; 2Sam 22:32; Za 86:10; Dan 6:26; 1Kor 8:6; Isa 37:16; Mk 12:32Yeyote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu la Bwana, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu. 41:4 Isa 10:20-22; Hes 15:3; Za 116:17; Ezr 3:7; 4:3Nao watu wa mahali popote wale walionusurika wanapoishi sasa, watu hao wampe fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, mbali na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”

51:5 2Nya 34:9; Neh 12:34; Hag 1:4; Flp 2:13; Mit 16:1Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba ya Bwana huko Yerusalemu. 6Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari. 71:7 2Fal 24:13; Ezr 5:14; 6:5; 2Nya 36:7; Yer 52:17-19Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu la Bwana, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalu la mungu wake. 81:8 Ezr 5:14; Hag 1:1; 1Nya 3:18Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda.

9Hii ilikuwa ndio orodha ya vifaa:

masinia ya dhahabu yalikuwa 30masinia ya fedha yalikuwa 1,000vyetezo vya fedha vilikuwa 2910mabakuli ya dhahabu yalikuwa 30mabakuli ya fedha yanayofanana yalikuwa 410vifaa vingine vilikuwa 1,000.

11Kwa ujumla, kulikuwa na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.