Zaburi 90:1-10
KITABU CHA NNE
(Zaburi 90–106)
Zaburi 90
Umilele Wa Mungu Na Udhaifu Wa Mwanadamu
Maombi ya Mose, mtu wa Mungu.
90:1 Kum 33:27; Efe 2:22; Ufu 21:3Bwana, wewe umekuwa makao yetu
katika vizazi vyote.
90:2 Ay 38:4, 5; 10:5; 15:7; Mwa 21:33; Isa 9:6; 57:15; Za 102:24-27; Mit 8:23-26Kabla ya kuzaliwa milima
au hujaumba dunia na ulimwengu,
wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
90:3 Mwa 2:7; 3:9; Ay 7:21; 34:15; 1Kor 15:47; Mhu 12:7Huwarudisha watu mavumbini,
ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”
90:4 Ebr 13:8; 2Pet 3:8; Ay 10:5Kwa maana kwako miaka elfu
ni kama siku moja iliyokwisha pita,
au kama kesha la usiku.
90:5 Mwa 19:15; Isa 40:6Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo,
nao ni kama majani machanga ya asubuhi:
90:6 Isa 40:6-8; Ay 14:2; Za 92:7ingawa asubuhi yanachipua,
ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka.
Tumeangamizwa kwa hasira yako
na tumetishwa kwa ghadhabu yako.
90:8 2Kor 4:2; Efe 5:12; Ebr 4:13; 4:12, 13; Za 19:12; 50:21; Yer 16:17; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1Kor 4:5Umeyaweka maovu yetu mbele yako,
dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako.
90:9 Za 78:33Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako,
tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza.
90:10 Isa 23:15, 17; 2Sam 19:35; Ay 5:7; 20:8; 34:15; Yer 25:11Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,
au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,
lakini yote ni ya shida na taabu,
nazo zapita haraka, nasi twatoweka.