Wafilipi 1:27-30, Wafilipi 2:1-11 NEN

Wafilipi 1:27-30

Kuenenda Ipasavyo Injili

1:27 Efe 4:1; 1Kor 16:13; Yud 3Lakini lolote litakalotukia, mwenende kama ipasavyo Injili ya Kristo, ili kwamba nikija na kuwaona au ikiwa sipo, nipate kusikia haya juu yenu: Kuwa mnasimama imara katika roho moja, mkiishindania imani ya Injili kwa umoja, 1:28 2The 1:5; Rum 8:17; 2Tim 2:11wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa, na hii ni kazi ya Mungu. 1:29 Mt 5:11, 12; Mdo 5:41; 14:22Kwa maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali pia kuteswa kwa ajili yake, 1:30 Kol 2:1; Ebr 10:32; Mdo 16:19-40kwa kuwa mnashiriki mashindano yale yale mliyoyaona nikiwa nayo na ambayo hata sasa mnasikia kuwa bado ninayo.

Read More of Wafilipi 1

Wafilipi 2:1-11

Kuiga Unyenyekevu Wa Kristo

2:1 2Kor 13:14; Kol 3:12Kama kukiwa na jambo lolote la kutia moyo katika kuunganishwa na Kristo, kukiwa faraja yoyote katika upendo wake, kukiwa na ushirika wowote na Roho, kukiwa na wema wowote na huruma, 2:2 Yn 3:29; Flp 4:2; Rum 12:16; 15:15basi ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, mkiwa na upendo huo moja, mkiwa wa roho na kusudi moja. 2:3 Gal 5:26; Rum 12:10; 1Pet 5:5Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake. 2:4 1Kor 10:24, 33; 13:5Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.

2:5 Mt 11:29; Yn 13:15; 1Pet 2:21; 1Yn 2:6Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu:

2:6 Yn 1:1; 5:18Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa,

hakuona kule kuwa sawa na Mungu

kuwa kitu cha kushikilia,

2:7 Mt 20:28; Rum 8:3; Ebr 5:8bali alijifanya si kitu,

akachukua hali hasa na mtumwa,

naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

2:8 Rum 5:19; Ebr 5:8Naye akiwa na umbo la mwanadamu,

alijinyenyekeza, akatii hata mauti:

naam, mauti ya msalaba!

2:9 Dan 7:14; Mdo 2:33; Efe 1:20Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana,

na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina,

2:10 Rum 14:11; Efe 1:10ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe,

la vitu vya mbinguni, na vya duniani,

na vya chini ya nchi,

2:11 Yn 13:13; Mdo 2:36; Rum 14:9; 1Kor 8:6; 12:3na kila ulimi ukiri ya kwamba

Yesu Kristo ni Bwana,

kwa utukufu wa Mungu Baba.

Read More of Wafilipi 2