Luka 24:36-53 NEN

Luka 24:36-53

Yesu Awatokea Wanafunzi Wake

(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)

24:36 Yn 20:19, 21, 26; 14:27Walipokuwa bado wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”

24:37 Mk 6:49Wakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. Lakini Yesu akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? 24:39 Yn 20:27; 1Yn 1:1Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”

Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. 24:41 Mwa 45:26; Yn 21:5Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?”

Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 24:43 Mdo 10:40naye akakichukua na kukila mbele yao.

24:44 Lk 24:26; Mt 1:22; 16:21; Za 110Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Sheria ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”

24:45 Mdo 16:14Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko. 24:46 Lk 24:26; Isa 50:6; 53:2Akawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 24:47 Mdo 10:43; 13:38; Mt 28:19; Mk 13:10Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu. 24:48 Yn 15:27; 1Pet 5:1Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.

Kuahidiwa Kwa Roho Mtakatifu

24:49 Yn 14:16; Mdo 1:4“Tazama nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo utokao juu.”

Kupaa Kwa Yesu Mbinguni

(Marko 16:19-20; Matendo 1:9-11)

24:50 Mt 21:11Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. 24:51 2Fal 2:11Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. 24:52 Mt 28:9, 17Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. 24:53 Mdo 2:46Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.

Read More of Luka 24