Kufufuka Kwa Yesu
(Mathayo 28:1-10; Marko 16:1-8; Yohana 20:1-10)
124:1 Lk 23:56; Mt 28:1; Mk 16; 1; Yn 20:2Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. 224:2 Mt 24:2; Mk 16:5Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, 324:3 Lk 24:23; Mk 16:5lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu. 424:4 Yn 20:12; Mdo 1:10Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayongʼaa kama umeme wakasimama karibu nao. 5Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao mpaka chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? 624:6 Mt 17:22-23; Mk 9:30-31Hayuko hapa; amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado yuko pamoja nanyi huko Galilaya kwamba: 724:7 Mt 8:20; 16:21‘Ilikuwa lazima Mwana wa Adamu atiwe mikononi mwa watu wenye dhambi na waovu ili asulubiwe, na siku ya tatu afufuke.’ ” 824:8 Yn 2:22Ndipo wakayakumbuka maneno ya Yesu.
924:9 Mt 28:8; Mk 16:10Waliporudi kutoka huko kaburini, wakawaeleza wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote mambo haya yote. 1024:10 Lk 8:1-3; Mk 6:30Basi Maria Magdalene, Yoana, na Maria mama yake Yakobo, pamoja na wanawake wengine waliofuatana nao ndio waliwaelezea mitume habari hizi. 1124:11 Mk 16:11Lakini hawakuwasadiki hao wanawake, kwa sababu maneno yao yalionekana kama upuzi. 1224:12 Yn 20:3-7; 20:10Hata hivyo, Petro akainuka na kukimbia kwenda kule kaburini. Alipoinama kuchungulia, akaona vile vitambaa vya kitani, ila hakuona kitu kingine. Naye akaenda zake akijiuliza nini kilichotokea.
Njiani Kwenda Emau
(Marko 16:12-13)
1324:13 Mk 16:12Ikawa siku iyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba24:13 Maili saba ni kama kilomita 11.2. kutoka Yerusalemu. 14Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia. 1524:15 Mt 18:20Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, 1624:16 Yn 20:14; 21:4lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.
17Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumza wakati mnatembea?”
Wakasimama, nyuso zao zikionyesha huzuni. 1824:18 Yn 19:25Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiye peke yako mgeni huku Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?”
1924:19 Mk 1:24Akawauliza, “Mambo gani?”
Wakamjibu, “Mambo ya Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote. 2024:20 Lk 23:13Viongozi wa makuhani na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa, nao wakamsulubisha. 2124:21 Lk 1:68; 2:38; Mt 16:21Lakini tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angelikomboa Israeli. Zaidi ya hayo, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 2224:22 Mt 28:8; Mk 16:10; Lk 24:9, 10; Yn 20:18Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtusha. Walikwenda kaburini leo alfajiri, 23lakini hawakuukuta mwili wake. Walirudi wakasema wameona maono ya malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. 2424:24 Lk 24:12; Yn 20:3-19Kisha baadhi ya wenzetu walikwenda kaburini wakalikuta kama vile wale wanawake walivyokuwa wamesema, lakini yeye hawakumwona.”
25Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii! 2624:26 Ebr 2:10; 1Pet 1:11Je, haikumpasa Kristo24:26 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?” 2724:27 Mwa 3:15; Hes 2:19; Mk 7:20; Mal 3:1; Yn 1:45Naye akianzia na Sheria ya Mose na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye.
2824:28 Mwa 32:26; 42:7; Mk 6:49Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea mbele. 2924:29 Mwa 19:3; Mdo 16:15Lakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao.
3024:30 Mt 14:19Alipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 3124:31 Za 39:3; Lk 24:16Ndipo macho yao yakafumbuliwa, nao wakamtambua, naye akatoweka machoni pao. Hawakumwona tena. 3224:32 Za 39:3; Lk 24:27, 28Wakaulizana wao kwa wao, “Je, mioyo yetu haikuwakawaka kwa furaha ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”
33Wakaondoka mara, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika 3424:34 1Kor 15:5wakisema, “Ni kweli! Bwana amefufuka, naye amemtokea Simoni.” 3524:35 Lk 24:30, 31Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotukia njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate.
Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
(Mathayo 28:16-20; Marko 16:14-18; Yohana 20:19-23; Matendo 1:6-8)
3624:36 Yn 20:19, 21, 26; 14:27Walipokuwa bado wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”
3724:37 Mk 6:49Wakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. 38Lakini Yesu akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? 3924:39 Yn 20:27; 1Yn 1:1Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.”
40Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. 4124:41 Mwa 45:26; Yn 21:5Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?”
42Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, 4324:43 Mdo 10:40naye akakichukua na kukila mbele yao.
4424:44 Lk 24:26; Mt 1:22; 16:21; Za 110Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Sheria ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”
4524:45 Mdo 16:14Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko. 4624:46 Lk 24:26; Isa 50:6; 53:2Akawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 4724:47 Mdo 10:43; 13:38; Mt 28:19; Mk 13:10Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu. 4824:48 Yn 15:27; 1Pet 5:1Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
Kuahidiwa Kwa Roho Mtakatifu
4924:49 Yn 14:16; Mdo 1:4“Tazama nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo utokao juu.”
Kupaa Kwa Yesu Mbinguni
(Marko 16:19-20; Matendo 1:9-11)
5024:50 Mt 21:11Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. 5124:51 2Fal 2:11Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. 5224:52 Mt 28:9, 17Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. 5324:53 Mdo 2:46Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.