Luka 1:57-80 NEN

Luka 1:57-80

Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji

Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto mwanaume. 1:58 Lk 1:14Majirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye.

1:59 Law 12:3; Flp 3:5Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake. 1:60 Lk 1:13, 63; Mt 3:1Lakini mama yake akakataa na kusema, “Hapana! Jina lake ataitwa Yohana.”

Wakamwambia, “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.”

1:62 Lk 1:22Basi wakamfanyia Zekaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. 1:63 Lk 1:13, 60; Mt 3:1Akaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yohana.” 1:64 Lk 1:20; Eze 24:27Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake ukaachiwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote. 1:66 Mwa 39:2; Mdo 11:21Kila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.

Unabii Wa Zekaria

1:67 Yoe 2:28Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema:

1:68 Mwa 24:27; 1Fal 8:15; Za 111:9; Lk 7:16“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli,

kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.

1:69 2Sam 22:23; Za 132:17Naye ametusimamishia pembe1:69 Pembe hapa inamaanisha nguvu. ya wokovu

katika nyumba ya Daudi mtumishi wake,

1:70 Yer 23:3; Za 132:17kama alivyonena kwa vinywa vya manabii

wake watakatifu tangu zamani,

1:71 Za 106:10kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu,

na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao:

1:72 Mik 7:20; Za 106:45; Eze 16:60ili kuonyesha rehema kwa baba zetu

na kukumbuka Agano lake takatifu,

1:73 Mwa 22:16-18kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu:

1:74 Ebr 9:14kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu,

tupate kumtumikia yeye pasipo hofu

1:75 Efe 4:24katika utakatifu na haki mbele zake,

siku zetu zote.

1:76 Mt 11:9; Mk 5:7; Mal 3:1; Mt 3:3“Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana;

kwa kuwa utamtangulia Bwana

na kuandaa njia kwa ajili yake,

1:77 Yer 31:34; Mt 1:21kuwajulisha watu wake juu ya wokovu

utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

1:78 Mal 4:2kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu,

nuru itokayo juu itatuzukia

1:79 Za 107:14; Mdo 26:18ili kuwaangazia wale waishio gizani

na katika uvuli wa mauti,

kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”

1:80 Lk 2:40, 52Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli.

Read More of Luka 1