1Kwa kuwa watu wengi wamekaa ili kuandika habari za mambo yaliyotukia katikati yetu, 21:2 Mk 1:1; Mdo 1:21-22; 2Pet 1:16; 1Yn 1:1; Mk 4:14kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale waliokuwa mashahidi walioyaona na watumishi wa Bwana, 31:3 Mdo 11:4; 24:3; 26:25; 1:1mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo, ewe mtukufu Theofilo, 41:4 Yn 20:31; Mdo 2:42ili upate kujua ukweli kuhusu yale uliyofundishwa.
Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji Kwatabiriwa
51:5 1Nya 24:10; Mt 2:1Wakati wa Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zekaria, ambaye alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Aroni. 61:6 Kum 5:33; Lk 2:25Zekaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Bwana na maagizo yote bila lawama. 7Lakini walikuwa hawana watoto, kwa sababu Elizabeti alikuwa tasa; nao wote wawili walikuwa wazee sana.
81:8 1Nya 24:19; 2Nya 8:14Siku moja ilipokuwa zamu ya kikundi cha Zekaria, yeye akifanya kazi ya ukuhani Hekaluni mbele za Mungu, 91:9 2Nya 29:11; Za 141:2alichaguliwa kwa kura kwa kufuata desturi za ukuhani, kuingia Hekaluni mwa Bwana ili kufukiza uvumba. 101:10 Law 16:17Nao wakati wa kufukiza uvumba ulipowadia, wale wote waliokuwa wamekusanyika ili kuabudu walikuwa nje wakiomba.
111:11 Mdo 5:19; Kut 30:1-10Ndipo malaika wa Bwana, akiwa amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia uvumba, akamtokea Zekaria. 121:12 Amu 6:22-23; 13:22Zekaria alipomwona huyo malaika, akafadhaika sana, akajawa na hofu. 131:13 Mt 14:27; 3:1; Lk 1:60-63Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yohana. 141:14 Lk 1:58Yeye atakuwa furaha na shangwe kwako, nao watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. 151:15 Law 10:9; Lk 7:33; Yer 1:5; Gal 1:15Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Bwana, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji chochote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake. 161:16 Mal 4:5, 6Naye atawageuza wengi wa wana wa Israeli warudi kwa Bwana Mungu wao. 171:17 Mt 11:14; Mal 4:4-6Naye atatangulia mbele za Bwana katika roho na nguvu ya Eliya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao, na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki, ili kuliweka tayari taifa lililoandaliwa kwa ajili ya Bwana.”
181:18 Mwa 17:17Zekaria akamuuliza malaika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa.”
191:19 Mt 18:10; Lk 1:26Malaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu, nami nimetumwa kwako ili nikuambie habari hizi njema. 201:20 Kut 4:11; Eze 3:26Basi sasa kwa kuwa hujaamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati wake, utakuwa bubu hadi siku ile mambo haya yatakapotukia.”
21Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zekaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni. 221:22 Lk 1:62Alipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono.
231:23 2Fal 11:5Muda wake wa kuhudumu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. 24Baada ya muda usio mrefu, Elizabeti mkewe akapata mimba, naye akajitenga kwa miezi mitano.
251:25 Mwa 30:23; Isa 4:1Akasema, “Hili ndilo Bwana alilonitendea aliponiangalia kwa upendeleo na kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.”
Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa
261:26 Lk 1:62; Mt 2:23Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 271:27 Mt 1:16-20; Lk 2:4kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 281:28 Amu 5:24Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”
291:29 Lk 1:12Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 301:30 Mt 14:27Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata kibali kwa Mungu. 311:31 Isa 7:14; Mt 1:21-25Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu. 321:32 Mk 5:7Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 331:33 Mt 28:18; 2Sam 7:16; Ebr 1:8Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”
34Maria akamuuliza huyo malaika, “Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?”
351:35 Mt 1:18; 4:3; Mk 1:24Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 361:36 Lk 1:24Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 371:37 Mt 19:26; Mwa 18:14; Zek 8:6; Mt 18:26; Mk 10:27; Rum 4:21Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”
38Maria akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha.
Maria Aenda Kumtembelea Elizabeti
391:39 Lk 1:65; Yos 21:9, 10, 11Wakati huo Maria akajiandaa, akaharakisha kwenda katika mji mmoja kwenye vilima vya Uyahudi. 40Akaingia nyumbani kwa Zekaria na kumsalimu Elizabeti. 411:41 Lk 1:15; Mwa 25; 22Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 421:42 Amu 5:24akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. 431:43 Yn 13:13Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 451:45 Lk 1:20; 11:28Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.”
Wimbo Wa Maria Wa Sifa
461:46 Za 34:2-3Naye Maria akasema:
“Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
471:47 Za 18:46; 1Tim 4:10nayo roho yangu inamfurahia
Mungu Mwokozi wangu,
481:48 Za 138:5; Lk 11:27kwa kuwa ameangalia kwa fadhili
unyonge wa mtumishi wake.
Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa,
491:49 Za 71:19; 111:9kwa maana yeye Mwenye Nguvu
amenitendea mambo ya ajabu:
jina lake ni takatifu.
501:50 Kut 20:6; Za 103:17Rehema zake huwaendea wale wamchao,
kutoka kizazi hadi kizazi.
511:51 Za 98:1; Isa 40:10Kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake;
amewatawanya wale wenye kiburi
ndani ya mioyo yao.
521:52 Mt 23:12; 1Sam 2:6; Ay 5:11; Za 11:3, 6Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi,
lakini amewainua wanyenyekevu.
531:53 Za 107:9; 1Sam 3:5Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri,
bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
541:54 Za 98:3Amemsaidia mtumishi wake Israeli,
kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu
551:55 Za 132:11; Gal 3:16Abrahamu na uzao wake milele,
kama alivyowaahidi baba zetu.”
56Maria akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.
Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji
57Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto mwanaume. 581:58 Lk 1:14Majirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye.
591:59 Law 12:3; Flp 3:5Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake. 601:60 Lk 1:13, 63; Mt 3:1Lakini mama yake akakataa na kusema, “Hapana! Jina lake ataitwa Yohana.”
61Wakamwambia, “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.”
621:62 Lk 1:22Basi wakamfanyia Zekaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. 631:63 Lk 1:13, 60; Mt 3:1Akaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yohana.” 641:64 Lk 1:20; Eze 24:27Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake ukaachiwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. 65Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote. 661:66 Mwa 39:2; Mdo 11:21Kila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Unabii Wa Zekaria
671:67 Yoe 2:28Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema:
681:68 Mwa 24:27; 1Fal 8:15; Za 111:9; Lk 7:16“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli,
kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.
691:69 2Sam 22:23; Za 132:17Naye ametusimamishia pembe1:69 Pembe hapa inamaanisha nguvu. ya wokovu
katika nyumba ya Daudi mtumishi wake,
701:70 Yer 23:3; Za 132:17kama alivyonena kwa vinywa vya manabii
wake watakatifu tangu zamani,
711:71 Za 106:10kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu,
na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao:
721:72 Mik 7:20; Za 106:45; Eze 16:60ili kuonyesha rehema kwa baba zetu
na kukumbuka Agano lake takatifu,
731:73 Mwa 22:16-18kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu:
741:74 Ebr 9:14kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu,
tupate kumtumikia yeye pasipo hofu
751:75 Efe 4:24katika utakatifu na haki mbele zake,
siku zetu zote.
761:76 Mt 11:9; Mk 5:7; Mal 3:1; Mt 3:3“Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana;
kwa kuwa utamtangulia Bwana
na kuandaa njia kwa ajili yake,
771:77 Yer 31:34; Mt 1:21kuwajulisha watu wake juu ya wokovu
utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,
781:78 Mal 4:2kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu,
nuru itokayo juu itatuzukia
791:79 Za 107:14; Mdo 26:18ili kuwaangazia wale waishio gizani
na katika uvuli wa mauti,
kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”
801:80 Lk 2:40, 52Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli.