Luka 1:26-38 NEN

Luka 1:26-38

Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa

1:26 Lk 1:62; Mt 2:23Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 1:27 Mt 1:16-20; Lk 2:4kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 1:28 Amu 5:24Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”

1:29 Lk 1:12Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 1:30 Mt 14:27Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata kibali kwa Mungu. 1:31 Isa 7:14; Mt 1:21-25Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu. 1:32 Mk 5:7Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 1:33 Mt 28:18; 2Sam 7:16; Ebr 1:8Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”

Maria akamuuliza huyo malaika, “Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?”

1:35 Mt 1:18; 4:3; Mk 1:24Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 1:36 Lk 1:24Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 1:37 Mt 19:26; Mwa 18:14; Zek 8:6; Mt 18:26; Mk 10:27; Rum 4:21Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”

Maria akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha.

Read More of Luka 1