Ayubu 38:1-41, Ayubu 39:1-30, Ayubu 40:1-2 NEN

Ayubu 38:1-41

Sehemu Ya Nne: Mungu Anazungumza

(Ayubu 38–41)

Bwana Anamjibu Ayubu

38:1 1Sam 2:10; Eze 1:4; Kut 19:16-18; Ay 11:5; 40:6; Isa 21:1Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:

38:2 Mk 10:38; 1Tim 1:7“Nani huyu atiaye mashauri yangu giza

kwa maneno yasiyo na maarifa?

38:3 Ay 40:7; 42:4; Mk 11:29; 1Fal 18:46Jikaze kama mwanaume;

nitakuuliza swali,

nawe unijibu.

38:4 Mwa 1:1; Mit 8:29; Za 104:5“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?

Niambie, kama unafahamu.

38:5 Za 102:25; Yer 31:37Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake?

Hakika wewe unajua!

Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

38:6 Mit 8:25; Ay 26:7Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini,

au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,

38:7 Mwa 1:16; Za 19:1-4; 148:2-3; 1Fal 22:19; Kum 16:15wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,

na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?

38:8 Za 33:7; Yer 5:22; Mwa 1:9-10“Ni nani aliyeifungia bahari milango

ilipopasuka kutoka tumbo,

38:9 Mwa 1:2nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,

na kuyafungia katika giza nene,

38:10 Za 33:7; Neh 3:3; Isa 40:12; Ay 7:12nilipoamuru mipaka yake,

na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

38:11 Za 65:7; 89:9; 104:6-9niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;

hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?

38:12 Za 57:8; 74:16; Amo 5:8“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,

au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,

yapate kushika miisho ya dunia,

na kuwakungʼuta waovu waliomo?

38:14 Kut 28:11Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri;

sura yake hukaa kama ile ya vazi.

38:15 Kum 28:29; Ay 15:22; Mwa 17:14; Za 10:15Waovu huzuiliwa nuru yao,

nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.

38:16 Mwa 1:7; Ay 9:8“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?

Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?

38:17 Za 9:13; Mt 16:18Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti?

Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?

38:18 Ay 28:24; Isa 40:12; Ay 38:4Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia?

Niambie kama unajua haya yote.

38:19 Mwa 1:4; Ay 28:3; Za 139:11-12“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi?

Nako maskani mwa giza ni wapi?

38:20 Ay 24:13Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake?

Unajua njia za kufika maskani mwake?

38:21 Ay 15:7Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa!

Kwani umeishi miaka mingi!

38:22 Ay 37:6; Kum 28:12; Za 105:32; 147:17“Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji,

au kuona ghala za mvua ya mawe,

38:23 Za 27:5; Isa 28:17; Eze 13:13; Ufu 16:21; Kut 9:18; Za 9:13ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu,

na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?

38:24 Ay 28:24; 27:21; Yer 10:13; 51:16Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa,

au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia?

38:25 Ay 28:26Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi

na njia ya umeme wa radi,

38:26 Ay 36:27; Za 84:6; 107:35; Isa 41:18ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu,

jangwa lisilo na yeyote ndani yake,

38:27 Ay 28:26; 37:13; Za 104:14ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa,

na majani yaanze kumea ndani yake?

38:28 2Sam 1:21; Yer 14:22Je, mvua ina baba?

Ni nani baba azaaye matone ya umande?

38:29 Za 147:16-17Barafu inatoka tumbo la nani?

Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni,

38:30 Ay 37:10wakati maji yawapo magumu kama jiwe,

wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda?

38:31 Ay 9:9; Amo 5:8“Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia?

Waweza kulegeza kamba za Orioni?

38:32 2Fal 23:5; Isa 13:10; 40:26; 45:12; Yer 19:13; Mwa 1:16Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake,

au kuongoza Dubu na watoto wake?

38:33 Za 148:6; Yer 31:38Je, unajua sheria zinazotawala mbingu?

Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?

38:34 Ay 5:10; 22:11“Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,

na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji?

38:35 Ay 36:32Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake?

Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’?

38:36 Ay 34:32; Yak 1:5; Za 51:6; Mhu 2:26Ni nani aliyeujalia moyo hekima

au kuzipa akili ufahamu?

38:37 Yos 3:16; Ay 22:11Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu?

Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni

38:38 Law 26:19wakati mavumbi yawapo magumu,

na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?

38:39 Mwa 49:9; Za 104:21“Je, utamwindia simba jike mawindo,

na kuwashibisha simba wenye njaa

38:40 Ay 37:8; Mwa 49:9wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao,

au wakivizia kichakani?

38:41 Mwa 8:7; Lk 12:24; Za 147:9; Mt 6:26Ni nani ampaye kunguru chakula

wakati makinda yake yanamlilia Mungu,

yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?

Read More of Ayubu 38

Ayubu 39:1-30

39:1 Kum 14:5“Je, wajua ni wakati gani mbuzi wa mlimani wanapozaa?

Je, watambua ni wakati gani kulungu jike azaapo mtoto wake?

39:2 Mwa 31:7-9Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo?

Je, unajua majira yao ya kuzaa?

Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao;

utungu wa kuzaa unakoma.

Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani;

huenda zao wala hawarudi tena.

39:5 Mwa 16:12; Ay 6:5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru?

Ni nani aliyezifungua kamba zake?

39:6 Za 107:34; Yer 2:24; 14:6; Hos 8:9Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake,

nchi ya chumvi kuwa makao yake.

39:7 Ay 5:22; 3:18Huzicheka ghasia za mji,

wala hasikii kelele za mwendesha gari.

39:8 Isa 32:20Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho

na kutafuta kila kitu kibichi.

39:9 Hes 23:22; Kum 33:17“Je, nyati atakubali kukutumikia?

Atakaa karibu na hori lako usiku?

39:10 Ay 41:13; Za 32:9Je, waweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba?

Je, atalima mabonde nyuma yako?

39:11 Ay 40:16; 41:12, 22; Za 147:10Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi?

Utamwachia yeye kazi zako nzito?

Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbani

kutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria?

39:13 Zek 5:9“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha,

lakini hayawezi kulinganishwa

na mabawa na manyoya ya korongo.

Huyataga mayai yake juu ya ardhi,

na kuyaacha yapate joto mchangani,

39:15 2Fal 14:9bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda,

kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.

39:16 Ay 39:17; Mao 4:3Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake;

hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,

39:17 Ay 21:22; 39:16kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima,

wala hakumpa fungu la akili njema.

39:18 Ay 5:22Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia,

humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.

39:19 Ay 39:11“Je, wewe humpa farasi nguvu

au kuivika shingo yake manyoya marefu?

39:20 Yoe 2:4-5; Ufu 9:7; Yer 8:16Je, wewe humfanya farasi aruke kama nzige,

akistaajabisha kwa tishio la mlio wake wa majivuno?

39:21 Yer 8:6Huparapara bila woga, akizifurahia nguvu zake,

husonga mbele kukabiliana na silaha.

39:22 Ay 5:22Huicheka hofu, haogopi chochote,

wala haukimbii upanga.

39:23 Isa 5:28; Yer 5:16; Nah 3:3Podo hutoa sauti kando yake,

pamoja na mkuki unaongʼaa na fumo.

39:24 Hes 10:9; Eze 7:14Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi,

wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama.

39:25 Yos 6:5; Yer 8:6; Amo 2:2Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’

Hunusa harufu ya vita toka mbali,

sauti ya mtoa amri na ukelele wa vita.

“Je, mwewe huruka kwa hekima yako

na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini?

Je, tai hupaa juu kwa amri yako

na kujenga kiota chake mahali pa juu?

Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku;

majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake.

Kutoka huko hutafuta chakula chake;

macho yake hukiona kutoka mbali.

39:30 Mt 24:28; Lk 17:37Makinda yake hujilisha damu,

na pale palipo na machinjo, ndipo yeye alipo.”

Read More of Ayubu 39

Ayubu 40:1-2

40:1 Ay 5:8; 13:3; 13:3; 9:15; 9:3; 11:8; 33:13Bwana akamwambia Ayubu:

40:2 Rum 9:20“Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?

Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”

Read More of Ayubu 40