Ayubu 38 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 38:1-41

Sehemu Ya Nne: Mungu Anazungumza

(Ayubu 38–41)

Bwana Anamjibu Ayubu

138:1 1Sam 2:10; Eze 1:4; Kut 19:16-18; Ay 11:5; 40:6; Isa 21:1Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:

238:2 Mk 10:38; 1Tim 1:7“Nani huyu atiaye mashauri yangu giza

kwa maneno yasiyo na maarifa?

338:3 Ay 40:7; 42:4; Mk 11:29; 1Fal 18:46Jikaze kama mwanaume;

nitakuuliza swali,

nawe unijibu.

438:4 Mwa 1:1; Mit 8:29; Za 104:5“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia?

Niambie, kama unafahamu.

538:5 Za 102:25; Yer 31:37Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake?

Hakika wewe unajua!

Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

638:6 Mit 8:25; Ay 26:7Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini,

au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni,

738:7 Mwa 1:16; Za 19:1-4; 148:2-3; 1Fal 22:19; Kum 16:15wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,

na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha?

838:8 Za 33:7; Yer 5:22; Mwa 1:9-10“Ni nani aliyeifungia bahari milango

ilipopasuka kutoka tumbo,

938:9 Mwa 1:2nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake,

na kuyafungia katika giza nene,

1038:10 Za 33:7; Neh 3:3; Isa 40:12; Ay 7:12nilipoamuru mipaka yake,

na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

1138:11 Za 65:7; 89:9; 104:6-9niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi;

hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?

1238:12 Za 57:8; 74:16; Amo 5:8“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke,

au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,

13yapate kushika miisho ya dunia,

na kuwakungʼuta waovu waliomo?

1438:14 Kut 28:11Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri;

sura yake hukaa kama ile ya vazi.

1538:15 Kum 28:29; Ay 15:22; Mwa 17:14; Za 10:15Waovu huzuiliwa nuru yao,

nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.

1638:16 Mwa 1:7; Ay 9:8“Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari?

Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi?

1738:17 Za 9:13; Mt 16:18Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti?

Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti?

1838:18 Ay 28:24; Isa 40:12; Ay 38:4Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia?

Niambie kama unajua haya yote.

1938:19 Mwa 1:4; Ay 28:3; Za 139:11-12“Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi?

Nako maskani mwa giza ni wapi?

2038:20 Ay 24:13Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake?

Unajua njia za kufika maskani mwake?

2138:21 Ay 15:7Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa!

Kwani umeishi miaka mingi!

2238:22 Ay 37:6; Kum 28:12; Za 105:32; 147:17“Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji,

au kuona ghala za mvua ya mawe,

2338:23 Za 27:5; Isa 28:17; Eze 13:13; Ufu 16:21; Kut 9:18; Za 9:13ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu,

na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano?

2438:24 Ay 28:24; 27:21; Yer 10:13; 51:16Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa,

au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia?

2538:25 Ay 28:26Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi

na njia ya umeme wa radi,

2638:26 Ay 36:27; Za 84:6; 107:35; Isa 41:18ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu,

jangwa lisilo na yeyote ndani yake,

2738:27 Ay 28:26; 37:13; Za 104:14ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa,

na majani yaanze kumea ndani yake?

2838:28 2Sam 1:21; Yer 14:22Je, mvua ina baba?

Ni nani baba azaaye matone ya umande?

2938:29 Za 147:16-17Barafu inatoka tumbo la nani?

Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni,

3038:30 Ay 37:10wakati maji yawapo magumu kama jiwe,

wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda?

3138:31 Ay 9:9; Amo 5:8“Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia?

Waweza kulegeza kamba za Orioni?

3238:32 2Fal 23:5; Isa 13:10; 40:26; 45:12; Yer 19:13; Mwa 1:16Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake,

au kuongoza Dubu na watoto wake?

3338:33 Za 148:6; Yer 31:38Je, unajua sheria zinazotawala mbingu?

Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani?

3438:34 Ay 5:10; 22:11“Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni,

na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji?

3538:35 Ay 36:32Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake?

Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’?

3638:36 Ay 34:32; Yak 1:5; Za 51:6; Mhu 2:26Ni nani aliyeujalia moyo hekima

au kuzipa akili ufahamu?

3738:37 Yos 3:16; Ay 22:11Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu?

Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni

3838:38 Law 26:19wakati mavumbi yawapo magumu,

na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?

3938:39 Mwa 49:9; Za 104:21“Je, utamwindia simba jike mawindo,

na kuwashibisha simba wenye njaa

4038:40 Ay 37:8; Mwa 49:9wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao,

au wakivizia kichakani?

4138:41 Mwa 8:7; Lk 12:24; Za 147:9; Mt 6:26Ni nani ampaye kunguru chakula

wakati makinda yake yanamlilia Mungu,

yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula?