Isaya 5:8-30, Isaya 6:1-13, Isaya 7:1-25, Isaya 8:1-10 NEN

Isaya 5:8-30

Ole Na Hukumu

5:8 Yer 22:13; Isa 24:16; 6:5; 10:1; Hab 2:9-12; Ay 20:19; Mik 2:2Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba

na kuunganisha mashamba baada ya mashamba

hadi hakuna nafasi iliyobaki,

nanyi mnaishi peke yenu katika nchi.

5:9 Isa 6:11-12; Mt 23:38; Yer 44:11; Isa 22:14; Mt 23:38Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia:

“Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa,

nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa.

5:10 Law 27:16; Kum 28:38; Zek 8:10; Law 26:26; 27:16Shamba la mizabibu la eka kumi

litatoa bathi5:10 Bathi moja ni sawa na lita 22. moja ya divai,

na homeri5:10 Homeri moja ni sawa na lita 220. ya mbegu zilizopandwa

itatoa efa5:10 Efa moja ni sawa na lita 22. moja tu ya nafaka.”

5:11 1Sam 25:36; Mit 23:29-30Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema

wakikimbilia kunywa vileo,

wale wakawiao sana mpaka usiku,

mpaka wamewaka kwa mvinyo.

5:12 1Sam 12:24; Ay 34:27; Eze 26:13; Amo 6:5-6; Isa 24:8; Ay 21:12; Za 28:5; 68:25Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao,

matari, filimbi na mvinyo,

lakini hawayajali matendo ya Bwana,

wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake.

5:13 Isa 49:21; 1:3; 3:3; Mit 10:21; Hos 4:6; Rum 1:28; Ay 22:8Kwa hiyo watu wangu watakwenda uhamishoni

kwa sababu ya kukosa ufahamu,

watu wao wenye vyeo watakufa kwa njaa

na watu wao wengi watakauka kwa kiu.

5:14 Mit 30:16; Hes 16:30; Isa 22:13; 23:7; 24:8Kwa hiyo kaburi5:14 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. limeongeza hamu yake

na kupanua mdomo wake bila kikomo,

ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu,

pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote.

5:15 Isa 2:9-11; 10:33Hivyo mwanadamu atashushwa,

na binadamu kunyenyekezwa,

macho ya wenye majivuno yatanyenyekezwa.

5:16 Isa 61:8; Law 10:3; Eze 36:23; Za 97:6; Isa 33:10; 28:17; 30:18; 29:23Lakini Bwana Mwenye Nguvu Zote atatukuzwa

kwa ajili ya haki yake,

naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewe

kuwa mtakatifu kwa haki yake.

5:17 Sef 2:6, 14; Isa 32:14; 7:25; 17:2Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe,

wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri.

5:18 Isa 59:4-8; 5:8; Amo 5:8; Yer 17:5; 23:14; Hos 11:4Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu

na uovu kama kwa kamba za mkokoteni,

5:19 2Pet 3:3-4; Eze 12:22; Yer 17:15; Isa 30:11-12; 29:23; 1:4; 60:22kwa wale wanaosema, “Mungu na afanye haraka,

aharakishe kazi yake ili tupate kuiona.

Huo mpango wa Aliye Mtakatifu wa Israeli na ukamilike,

tena udhihirike ili tupate kuujua.”

5:20 Ay 24:13; Amo 5:7; Mwa 18:25; 1Fal 22:8; Za 94:21; Isa 5:8; Mt 6:22-23; Lk 11:22, 34-35Ole wao wanaoita ubaya ni wema,

na wema ni ubaya,

wawekao giza badala ya nuru,

na nuru badala ya giza,

wawekao uchungu badala ya utamu,

na utamu badala ya uchungu.

5:21 Mit 3:7; Rum 12:16; Isa 47:10; 1Kor 3:18-20Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe,

na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe.

5:22 1Sam 25:36; Mit 23:20; Isa 22:13; Mit 31:4; Yer 7:18Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo,

nao walio hodari katika kuchanganya vileo,

5:23 Kut 23:8; Amo 5:12; Yak 5:6; Eze 22:12; Isa 1:17; 29:21; 59:13-15; Za 94:21wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo,

lakini huwanyima haki wasio na hatia.

5:24 2Fal 19:20; Za 107:11; Ay 18:16; Isa 47:14; Ay 24:24; 40:8; 6:10; Isa 1:31; Nah 1:10; 2Fal 19:30Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi,

na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto,

ndivyo mizizi yao itakavyooza

na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi;

kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote

na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.

5:25 2Fal 22:13; Yer 6:12; 2Fal 9:37; Dan 9:16; Ay 40:11; Kut 19:18; Isa 26:11; 10:17; Ay 40:11; Yer 6:12Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake,

mkono wake umeinuliwa na anawapiga.

Milima inatetemeka,

maiti ni kama takataka kwenye barabara.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

5:26 Za 20:5; Isa 7:18; Zek 10:8; Kum 28:4-9; Isa 13:5; 18:2Yeye anainua bendera kwa ajili ya mataifa yaliyo mbali,

anapiga filimbi kwa ajili ya wale walio kwenye miisho ya dunia.

Tazama wamekuja,

kwa kasi na kwa haraka!

5:27 Yoe 2:7-8; Eze 23:15; Isa 22:21; 40:29-31; 14:31; Ay 12:18Hakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa,

hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala,

hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni,

hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika.

5:28 Ay 39:23; Za 45:6; 7:12; Eze 26:11; Ay 1:19; Za 25:5; 2Fal 2:1Mishale yao ni mikali,

pinde zao zote zimevutwa,

kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume,

magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.

5:29 Isa 42:22; 49:24-25; 2Fal 17:25; Mik 5:8; Yer 51:38; Zek 11:3; Sef 3:3; Isa 10:6Ngurumo yao ni kama ile ya simba,

wananguruma kama wana simba,

wanakoroma wanapokamata mawindo yao,

na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.

5:30 Yer 4:23-28; Za 93:3; Yoe 2:10; Isa 2:1; 2:11; 50:3; Yer 50:42; Ay 21:30; Lk 21:25; 1Sam 2:9; Za 18:28Katika siku ile watanguruma juu yake

kama ngurumo za bahari.

Kama mtu akiitazama nchi,

ataona giza na dhiki;

hata nuru itatiwa giza kwa mawingu.

Read More of Isaya 5

Isaya 6:1-13

Agizo Kwa Isaya

6:1 2Nya 26:22-23; Hes 12:8; Ufu 4:2; 1:13; 2Fal 15:7; Kut 24:10; Ufu 4:2; Yn 12:41; 1Fal 22:19Katika mwaka ule Mfalme Uzia alikufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza Hekalu. 6:2 Eze 1:5; 10:15; 1:11; Ufu 4:8Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao, na kwa mawili walikuwa wakiruka. 6:3 Ufu 4:8; Kut 16:7; 15:11; Hes 14:21; Isa 54:5; 11:9; Za 89:9; 72:19; 89:8; Mal 1:11Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake:

“Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;

dunia yote imejaa utukufu wake.”

6:4 Kut 19:18; Eze 43:5; 44:4; Ufu 15:8Kwa sauti zao, miimo ya milango na vizingiti vilitikisika, nalo Hekalu likajaa moshi.

6:5 Isa 59:3; Yer 9:3-8; 51:57; Hes 17:12; Kum 5:26; Kut 6:12; 24:10; Isa 24:23; 5:8; Lk 5:8; Yer 5:3; 51:57; Ay 42:5Ndipo nikalia, “Ole wangu! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

6:6 Law 10:1; Eze 10:2Ndipo mmoja wa wale maserafi akaruka kunijia akiwa na kaa la moto linalowaka mkononi mwake, ambalo alikuwa amelichukua kwa koleo kutoka madhabahuni. 6:7 Dan 10:16; 12:3; 1Yn 1:7; Isa 45:25; Yer 1:9; Law 26:41Akanigusa nalo kinywa changu na kusema, “Tazama, hili limegusa midomo yako, uovu wako umeondolewa, nayo dhambi yako imesamehewa.”

6:8 Mdo 9:4; Ay 40:9; Yer 26:12-15; Mwa 1:26; 22:1; Kut 3:4Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?”

Nami nikasema, “Mimi hapa. Nitume mimi!”

6:9 Mt 13:15; Lk 8:10; Mt 28:196:9 Amo 7:15; Yer 5:21; Eze 3:11; Mt 13:15; Lk 8:10Akasema, “Nenda ukawaambie watu hawa:

“ ‘Mtaendelea daima kusikiliza,

lakini kamwe hamtaelewa;

mtaendelea daima kutazama,

lakini kamwe hamtatambua.’

6:10 Kut 4:21; Kum 32:39; 29:4; Eze 12:2; Isa 44:18; Yn 12:40; Mk 4:12; 8:18Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu,

fanya masikio yao yasisikie,

na upofushe macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

nao wakageuka, nikawaponywa.”

6:11 Yer 4:13; Za 79:5; 79:1; Isa 24:10; Yer 35:17; Za 119:11; Law 26:31, 43Ndipo nikasema, “Hadi lini, Ee Bwana?”

Naye akanijibu:

“Hadi miji iwe imeachwa magofu

na bila wakazi,

hadi nyumba zitakapobaki bila watu,

na mashamba yatakapoharibiwa na kuangamizwa,

6:12 Kum 28:64; Yer 30:17; 4:29; Isa 5:5-9; 60:15; 62:4; 62:4hadi Bwana atakapokuwa amekwisha kumpeleka kila mmoja mbali sana,

na nchi itakapokuwa imeachwa kabisa.

6:13 Rum 11:5; Ay 14:7; 14:8; Isa 10:22; Kum 14:2; Law 27:30; Isa 5:6; 1:9Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi,

itaharibiwa tena.

Lakini kama vile mvinje na mwaloni

ibakizavyo visiki inapokatwa,

ndivyo mbegu takatifu

itakavyokuwa kisiki katika nchi.”

Read More of Isaya 6

Isaya 7:1-25

Ishara Ya Imanueli

7:1 2Fal 16:5; 2Nya 28:5; 2Fal 15:25, 37; 1Nya 3:13; Isa 8:6; 7:5, 9Wakati Ahazi mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, alipokuwa mfalme wa Yuda, Mfalme Resini wa Aramu,7:1 Yaani Shamu. na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli walipanda kupigana dhidi ya Yerusalemu, lakini hawakuweza kuushinda.

7:2 2Sam 7:11; Amo 9:11; Hos 5:8; Isa 16:5; Yer 21:12; Isa 6:4; 22:22; 9:9; Dan 5:6; Hos 5:3Wakati huu nyumba ya Daudi iliambiwa, “Aramu wameungana na Efraimu.” Kwa hiyo mioyo ya Ahazi na watu wake ilitikiswa, kama miti ya msituni inavyotikiswa na upepo.

7:3 2Fal 18:17; Isa 36:2; 10:21-22Ndipo Bwana akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu,7:3 Shear-Yashubu maana yake Mabaki Watarudi. mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi. 7:4 Kum 3:2; 20:3; Mao 3:26; Zek 3:2; Mt 24:6; Isa 54:14; 30:15; 21:4; 8:12; 10:24; 51:13; Mwa 15:1Mwambie, ‘Uwe mwangalifu, utulie na usiogope. Usife moyo kwa ajili ya watu hawa wawili walio kama visiki vya kuni vifukavyo moshi, kwa ajili ya hasira kali ya Resini na Aramu na ya mwana wa Remalia. 7:5 Isa 6:1Aramu, Efraimu na mwana wa Remalia wamepanga shauri baya ili wakuangamize, wakisema, 7:6 Isa 24:3; 25:8; 28:10“Tuishambulie Yuda, naam, tuirarue vipande vipande na kuigawa miongoni mwetu, na kumtawaza mwana wa Tabeeli awe mfalme juu yake.” 7:7 Mdo 4:25; Isa 24:3; 25:8; 28:16; 8:10; 40:8; 46:10; 14:24; Za 2:1Lakini Bwana Mwenyezi asema hivi:

“ ‘Jambo hili halitatendeka,

halitatokea,

7:8 Mwa 3:15; 14:15; 2Sam 8:6; 2Fal 17:24; Isa 9:11; 17:1-3; 8:4; 17:1-3kwa kuwa kichwa cha Aramu ni Dameski,

na kichwa cha Dameski ni Resini peke yake.

Katika muda wa miaka sitini na mitano,

Efraimu atakuwa ameharibiwa

kiasi kwamba hataweza tena kuwa taifa.

7:9 2Nya 20:20; Isa 8:6-8; 30:12-14; 9:9; 9:1, 3; Za 20:8; 2Fal 15:29Kichwa cha Efraimu ni Samaria,

na kichwa cha Samaria

ni mwana wa Remalia peke yake.

Kama hamtasimama thabiti katika imani yenu,

hamtaimarika kamwe.’ ”

Bwana akasema na Ahazi tena, 7:11 Kum 13:2; Za 139:8; Kut 7:9“Mwombe Bwana Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.”

7:12 Kum 4:34Lakini Ahazi akasema, “Sitaomba; sitamjaribu Bwana.”

7:13 Za 63:1; 118:28; Mwa 30:15; Isa 1:14; 49:4; 61:10Ndipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? 7:14 Mwa 5:13; 21:22; 24:43; Kut 3:12; Lk 2:12; Mt 1:23; Mwa 3:15; 21:22; Lk 1:31Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli.7:14 Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi. 7:15 Mwa 18:8; Isa 8:4; Kum 1:39; 13:16Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. 7:16 Isa 8:4; 17:3; Yer 13:5; 7:15; Kum 13:16; 1:39; Hos 5:9-13Lakini kabla mtoto hajajua kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ya wafalme hao wawili unaowaogopa itafanywa ukiwa. 7:17 2Nya 28:20; 1Fal 12:16; Neh 9:32; 2Nya 7:18; Isa 17:9; 34:13Bwana ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”

7:18 Isa 5:26; 13:5; 7:25Katika siku ile Bwana atawapigia filimbi mainzi kutoka vijito vya mbali vya Misri, na nyuki kutoka nchi ya Ashuru. 7:19 Isa 2:19; 7:25; 17:9; 34:13; 55:13Wote watakuja na kukaa kwenye mabonde yenye miteremko, na kwenye nyufa za miamba, kwenye vichaka vyote vyenye miiba, na kwenye mashimo yote ya maji. 7:20 Isa 10:15; 29:16; 8:7; 11:15; 2Fal 18:16; Yer 27:6-7; 2:18; 2Sam 10:4; Kum 28:40Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ngʼambo ya Mto,7:20 Yaani Frati. yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. 7:21 Isa 2:17; Yer 39:10Katika siku ile, mtu atahifadhi hai ndama mmoja na kondoo wawili. 7:22 Mwa 18:8; Isa 14:30Kwa ajili ya wingi wa maziwa watakayotoa, atapata jibini ya kula. Wote watakaobakia katika nchi watakula jibini na asali. 7:23 Isa 5:6; 8:11; 7:2; Hos 2:12Katika siku ile, kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu moja yenye thamani ya shekeli 1,0007:23 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha, patakuwa na michongoma na miiba tu. 7:24 Isa 5:6Watu watakwenda huko wakiwa na upinde na mshale, kwa maana nchi itafunikwa na michongoma na miiba. 7:25 Isa 5:17; Hag 1:11Kuhusu vilima vyote vilivyokuwa vikilimwa kwa jembe, hamtakwenda huko tena kwa ajili ya hofu ya michongoma na miiba. Patakuwa mahali ambapo ngʼombe wataachiwa huru, na kondoo kukimbia kimbia.

Read More of Isaya 7

Isaya 8:1-10

Ashuru, Chombo Cha Bwana

8:1 Kum 27:8; Ay 19:23; Yer 20:3; 51:60; Isa 30:8; 8:3; Hos 1:4Bwana akaniambia, “Chukua gombo kubwa, uandike juu yake kwa kalamu ya kawaida jina: Maher-Shalal-Hash-Bazi.8:1 Maher-Shalal-Hash-Bazi maana yake ni Haraka kuteka nyara, Upesi kwenye hizo nyara. 8:2 2Fal 16:10; Yos 24:22; Rut 4:9; Yer 10:10-12; 32:10Nami nitawaita kuhani Uria, na Zekaria mwana wa Yeberekia kama mashahidi wangu waaminifu.”

8:3 Kut 15:20; Mwa 3:15Kisha nikaenda kwa nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mwana. Kisha Bwana akaniambia, “Mwite huyo mtoto Maher-Shalal-Hash-Bazi. 8:4 Isa 7:8, 16; Mwa 14:15; Isa 7:8Kabla mtoto hajaweza kusema ‘Baba yangu’ au ‘Mama yangu,’ utajiri wa Dameski na nyara za Samaria zitachukuliwa na mfalme wa Ashuru.”

Bwana akasema nami tena:

8:6 Neh 3:15; Isa 5:24; 7:1; Yn 9:7“Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu

wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia,

8:7 Isa 7:20; Dan 11:40; Nah 1:8; 2Nya 28:20; Isa 17:12-13; 30:28; Yos 3:15; Isa 10:16kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao

mafuriko makubwa ya Mto:8:7 Yaani Frati.

yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote.

Yatafurika juu ya mifereji yake yote,

yatamwagikia juu ya kingo zake zote,

8:8 Isa 7:14; 28:15; 18:6; 46:11; Yer 4:13; 48:40na kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake,

yakipita katikati na yakifika hadi shingoni.

Mabawa yake yaliyokunjuliwa

yatafunika upana wa nchi yako,

Ee Imanueli!”8:8 Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.

8:9 Isa 17:12-13; Eze 38:7; 38:3; Zek 14:2-3; Ay 34:24; Yer 46:3; 6:4; Zek 14:2; Yos 6:5Inueni kilio cha vita, enyi mataifa,

na mkavunjwevunjwe!

Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali.

Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!

Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!

8:10 Ay 5:12; Isa 7:7, 14; Rum 8:31; Mit 19:21; Mt 1:23Wekeni mikakati yenu, lakini itashindwa;

fanyeni mipango yenu, lakini haitafanikiwa,

kwa maana Mungu yu pamoja nasi.8:10 Kiebrania ni Imanueli.

Read More of Isaya 8