Isaya 6 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 6:1-13

Agizo Kwa Isaya

16:1 2Nya 26:22-23; Hes 12:8; Ufu 4:2; 1:13; 2Fal 15:7; Kut 24:10; Ufu 4:2; Yn 12:41; 1Fal 22:19Katika mwaka ule Mfalme Uzia alikufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza Hekalu. 26:2 Eze 1:5; 10:15; 1:11; Ufu 4:8Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao, na kwa mawili walikuwa wakiruka. 36:3 Ufu 4:8; Kut 16:7; 15:11; Hes 14:21; Isa 54:5; 11:9; Za 89:9; 72:19; 89:8; Mal 1:11Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake:

“Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;

dunia yote imejaa utukufu wake.”

46:4 Kut 19:18; Eze 43:5; 44:4; Ufu 15:8Kwa sauti zao, miimo ya milango na vizingiti vilitikisika, nalo Hekalu likajaa moshi.

56:5 Isa 59:3; Yer 9:3-8; 51:57; Hes 17:12; Kum 5:26; Kut 6:12; 24:10; Isa 24:23; 5:8; Lk 5:8; Yer 5:3; 51:57; Ay 42:5Ndipo nikalia, “Ole wangu! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninaishi katikati ya watu wenye midomo michafu, nayo macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

66:6 Law 10:1; Eze 10:2Ndipo mmoja wa wale maserafi akaruka kunijia akiwa na kaa la moto linalowaka mkononi mwake, ambalo alikuwa amelichukua kwa koleo kutoka madhabahuni. 76:7 Dan 10:16; 12:3; 1Yn 1:7; Isa 45:25; Yer 1:9; Law 26:41Akanigusa nalo kinywa changu na kusema, “Tazama, hili limegusa midomo yako, uovu wako umeondolewa, nayo dhambi yako imesamehewa.”

86:8 Mdo 9:4; Ay 40:9; Yer 26:12-15; Mwa 1:26; 22:1; Kut 3:4Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?”

Nami nikasema, “Mimi hapa. Nitume mimi!”

96:9 Mt 13:15; Lk 8:10; Mt 28:196:9 Amo 7:15; Yer 5:21; Eze 3:11; Mt 13:15; Lk 8:10Akasema, “Nenda ukawaambie watu hawa:

“ ‘Mtaendelea daima kusikiliza,

lakini kamwe hamtaelewa;

mtaendelea daima kutazama,

lakini kamwe hamtatambua.’

106:10 Kut 4:21; Kum 32:39; 29:4; Eze 12:2; Isa 44:18; Yn 12:40; Mk 4:12; 8:18Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu,

fanya masikio yao yasisikie,

na upofushe macho yao.

Wasije wakaona kwa macho yao,

na wakasikiliza kwa masikio yao,

wakaelewa kwa mioyo yao,

nao wakageuka, nikawaponywa.”

116:11 Yer 4:13; Za 79:5; 79:1; Isa 24:10; Yer 35:17; Za 119:11; Law 26:31, 43Ndipo nikasema, “Hadi lini, Ee Bwana?”

Naye akanijibu:

“Hadi miji iwe imeachwa magofu

na bila wakazi,

hadi nyumba zitakapobaki bila watu,

na mashamba yatakapoharibiwa na kuangamizwa,

126:12 Kum 28:64; Yer 30:17; 4:29; Isa 5:5-9; 60:15; 62:4; 62:4hadi Bwana atakapokuwa amekwisha kumpeleka kila mmoja mbali sana,

na nchi itakapokuwa imeachwa kabisa.

136:13 Rum 11:5; Ay 14:7; 14:8; Isa 10:22; Kum 14:2; Law 27:30; Isa 5:6; 1:9Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi,

itaharibiwa tena.

Lakini kama vile mvinje na mwaloni

ibakizavyo visiki inapokatwa,

ndivyo mbegu takatifu

itakavyokuwa kisiki katika nchi.”