Isaya 24:1-23, Isaya 25:1-12, Isaya 26:1-21 NEN

Isaya 24:1-23

Dunia Kuharibiwa Upesi

24:1 Isa 2:19-21; Yer 25:29; Yos 6:17; Isa 13:5; 33:9; Mwa 11:9Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa

na kuiharibu,

naye atauharibu uso wake

na kutawanya wakaao ndani yake:

24:2 Eze 7:12; Hos 4:9; 1Kor 7:29-31; Law 25:35-37; Kum 23:19-20; Law 25:35-37; Isa 3:1-7ndivyo itakavyokuwa

kwa makuhani na kwa watu,

kwa bwana na kwa mtumishi,

kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike,

kwa muuzaji na kwa mnunuzi,

kwa mkopaji na kwa mkopeshaji,

kwa mdaiwa na kwa mdai.

24:3 Isa 6:11-12; 10:6; 7:7; Mwa 6:13Dunia itaharibiwa kabisa

na kutekwa nyara kabisa.

Bwana amesema neno hili.

24:4 Yos 12:11; Yer 14:4; Isa 15:6; 1Sam 2:12; Yoe 1:10Dunia inakauka na kunyauka,

dunia inanyongʼonyea na kunyauka,

waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea.

24:5 Mwa 3:17; Hes 35:33; Law 18:25; Isa 59:12; 9:17; Yer 7:28; 11:10; Mwa 9:11Dunia imetiwa unajisi na watu wake;

wameacha kutii sheria,

wamevunja amri

na kuvunja agano la milele.

24:6 Yer 50:15; Isa 20:624:6 Kum 28:15; Law 26:15; Dan 9:11; Yos 23:15Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia,

watu wake lazima waichukue hatia yao.

Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa,

nao waliosalia ni wachache sana.

24:7 Isa 32:10; 7:23; Yoe 1:10-12; Isa 16:8-10Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka,

watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.

24:8 Mwa 31:27; Isa 5:14; Mao 5:14; Eze 26:13; Yer 7:34; 16:9; Ufu 5:14Furaha ya matoazi imekoma,

kelele za wenye furaha zimekoma,

shangwe za kinubi zimenyamaza.

24:9 Isa 5:11, 20-22Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo,

kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.

24:10 Isa 25:2; 26:5; 6:11Mji ulioharibiwa umekuwa ukiwa,

mlango wa kila nyumba umefungwa.

24:11 Isa 15:6; 16:10; 32:13; Yer 14:3; Za 144:14; Mao 2:12Barabarani wanalilia kupata mvinyo,

furaha yote imegeuka kuwa majonzi,

furaha yote imefukuziwa mbali na dunia.

24:12 Isa 19:18; 3:26; 13:2Mji umeachwa katika uharibifu,

lango lake limevunjwa vipande.

24:13 Kum 30:4; Isa 17:6; Mik 7:1Ndivyo itakavyokuwa duniani

na miongoni mwa mataifa,

kama vile wakati mzeituni upigwavyo,

au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa.

24:14 Isa 12:6; 43:5; 49:12Wanainua sauti zao, wanapiga kelele kwa furaha,

kutoka magharibi wanasifu kwa ukelele utukufu wa Bwana.

24:15 Isa 45:12; 2The 1:12; Mal 1:11; Kut 15:2; Za 113:3; Isa 25:3; 12:4; 59:19Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu,

liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli,

katika visiwa vya bahari.

24:16 Isa 28:5; Yer 3:20; 9:2; 10:19; Za 48:10; Hos 5:7; Ezr 9:15; 1Sam 4:8Kutoka miisho ya dunia tunasikia uimbaji:

“Utukufu kwa Yule Mwenye Haki.”

Lakini nilisema, “Ninadhoofika, ninadhoofika!

Ole wangu!

Watenda hila wanasaliti!

Kwa hila watenda hila wanasaliti!”

24:17 Isa 8:14; Yer 48:43; Amo 5:19; Kum 32:23-25; Lk 21:35Hofu, shimo na mtego vinakungojea,

ewe mtu ukaaye duniani.

24:18 Mwa 7:11; Amu 5:4; Ay 18:19; 20:24; Za 18:7; Isa 42:22; Mao 3:47; Eze 38:15Kila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu

atatumbukia shimoni,

naye yeyote apandaye kutoka shimoni,

atanaswa kwenye mtego.

Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa,

misingi ya dunia inatikisika.

24:19 Yer 4:23; Kum 11:6; Za 46:2Dunia imepasuka,

dunia imechanika,

dunia imetikiswa kabisa.

24:20 Ay 12:15; 27:18; Isa 1:2, 28; 19:14; 43:27; Za 46:2; Isa 58:1; Ay 12:14, 25Dunia inapepesuka kama mlevi,

inayumbayumba kama kibanda kwenye upepo;

imelemewa sana na mzigo wa hatia ya uasi wake

na ikianguka kamwe haitainuka tena.

24:21 Isa 13:11; 2:11; Yer 25:29; Za 76:12; Isa 10:20; Ufu 16:14; 1Kor 6:3; Efe 6:12Katika siku ile Bwana ataadhibu

nguvu zilizoko mbinguni juu,

na wafalme walioko duniani chini.

24:22 Isa 42:7, 22; Lk 8:31; Eze 38:8; Isa 10:4; Ufu 20:7-10Watakusanywa pamoja

kama wafungwa waliofungwa gerezani,

watafungiwa gerezani

na kuadhibiwa baada ya siku nyingi.

24:23 Za 97:1; Ufu 22:5; Ebr 12:22; Ufu 21:23; Isa 13:10; 28:5; 41:16Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa;

kwa maana Bwana Mwenye Nguvu Zote atawala

juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu,

tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.

Read More of Isaya 24

Isaya 25:1-12

Msifuni Bwana

25:1 Hes 23:19; Za 40:5; Yoe 2:21-26; Isa 7:13; 14:24; 37:26; Efe 1:11Ee Bwana, wewe ni Mungu wangu,

nitakutukuza na kulisifu jina lako,

kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu

umetenda mambo ya ajabu,

mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.

25:2 Isa 37:26; Yer 51:37; Isa 17:3; 13:22; Kum 13:16; Ay 12:14Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi,

mji wenye ngome kuwa magofu,

ngome imara ya wageni kuwa si mji tena,

wala hautajengwa tena kamwe.

25:3 Kut 6:2; Za 22:23; Isa 11:14; 13:11; Ufu 11:13Kwa hiyo mataifa yenye nguvu yatakuheshimu,

miji ya mataifa katili itakuheshimu wewe.

25:4 Yoe 3:16; Isa 33:16; Za 46:1-11; Isa 49:25; 2Sam 22:3; Za 118:8; Isa 3:14Umekuwa kimbilio la watu maskini,

kimbilio la mhitaji katika taabu yake,

hifadhi wakati wa dhoruba

na kivuli wakati wa hari.

Kwa maana pumzi ya wakatili

ni kama dhoruba ipigayo ukuta

25:5 Yer 51:25; Za 18:44; Isa 13:11na kama joto la jangwani.

Wewe wanyamazisha makelele ya wageni;

kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu,

ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.

25:6 Mt 22:4; Mit 9:2; Dan 7:14; Mwa 29:22; Za 36:8Juu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa

karamu ya vinono kwa mataifa yote,

karamu ya mvinyo wa zamani,

nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.

25:7 2Kor 3:15-16; Efe 4:8; 1:17; Ay 4:9Juu ya mlima huu ataharibu

sitara ihifadhiyo mataifa yote,

kile kifuniko kifunikacho mataifa yote,

25:8 Hos 13:14; 1Kor 15:54-55; Yer 31:16; Ufu 7:14-17; Ebr 2:14; Isa 26:19yeye atameza mauti milele.

Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;

ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.

Bwana amesema hili.

25:9 Isa 40:9; Yer 14:8; Za 20:5; Kum 32:43; Isa 2:11; 49:25-26; Za 145:19Katika siku ile watasema,

“Hakika huyu ndiye Mungu wetu;

tulimtumaini, naye akatuokoa.

Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini;

sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”

25:10 Mwa 19:37; Hes 21:29; Kum 23:6; Isa 11:14; Amo 2:1-2Mkono wa Bwana utatulia juu ya mlima huu,

bali Moabu atakanyagwa chini

kama majani makavu yakanyagwavyo kwenye shimo la mbolea.

25:11 Isa 5:25; 14:26; Law 26:19; Ay 40:12; Isa 2:10-17; 16:14Watakunjua mikono yao katikati yake,

kama vile mwogeleaji akunjuavyo mikono yake ili aogelee.

Mungu atashusha kiburi chao

licha ya ujanja wa mikono yao.

25:12 Ay 40:11; Isa 26:5; Yer 51:44; Isa 2:15Atabomoa kuta ndefu za maboma yako

na kuziangusha chini,

atazishusha chini ardhini,

mpaka mavumbini kabisa.

Read More of Isaya 25

Isaya 26:1-21

Wimbo Wa Ushindi

26:1 Isa 14:32; Zek 2:5; Isa 10:20; 30:29; 32:18; Zek 9:8; Za 48:13Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda:

Tuna mji ulio na nguvu,

Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake.

26:2 Isa 58:8; 62:2; Ufu 21:13; Za 24:4-7; 83:13; Isa 1:26; 50:8Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia,

taifa lile lidumishalo imani.

26:3 Ay 22:21; Flp 4:7; Isa 9:6-7; 1Nya 5:20; Za 28:7; 22:5Utamlinda katika amani kamilifu

yeye ambaye moyo wake ni thabiti

kwa sababu anakutumaini wewe.

26:4 Isa 12:2; 50:10; Za 62:8; Mwa 49:24Mtumaini Bwana milele,

kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele.

26:5 Isa 25:12; 25:5; Eze 26:11Huwashusha wale wajikwezao,

huushusha chini mji wenye kiburi,

huushusha hadi ardhini

na kuutupa chini mavumbini.

26:6 Isa 5:5; 49:26; 3:15; 14:30Miguu huukanyaga chini,

miguu ya hao walioonewa,

hatua za hao maskini.

26:7 Kum 32:4; Kut 14:19; Isa 42:16; Za 26:12; 25:8; Isa 40:4Mapito ya wenye haki yamenyooka.

Ewe uliye Mwenye Haki,

waisawazisha njia ya mtu mnyofu.

26:8 Za 18:22; 145:2; Isa 12:4; Kum 18:18; Isa 65:5; Za 37:9Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako,

twakungojea wewe,

jina lako na sifa zako

ndizo shauku za mioyo yetu.

26:9 Za 42:1-2; Mt 6:33; Za 63:6; 119:55; 1Nya 16:14; Za 78:34Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku,

wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku.

Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia,

watu wa ulimwengu hujifunza haki.

26:10 Isa 32:6; 1Sam 12:24; Rum 2:4; Mhu 8:12; Mt 5:45; Isa 22:12-13; Yer 2:19; Yn 5:38Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu,

hawajifunzi haki,

hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya

wala hawazingatii utukufu wa Bwana.

26:11 Ay 34:27; Isa 18:3; 44:9, 18; Ebr 10:27; Za 10:12; Yoe 2:18; Zek 1:14; Mik 7:16Ee Bwana, mkono wako umeinuliwa juu,

lakini hawauoni.

Wao na waone wivu wako kwa ajili ya watu wako tena waaibishwe,

moto uliowekwa akiba kwa ajili ya adui zako na uwateketeze.

26:12 Za 119:165; Isa 9:6; Za 68:28Bwana, unaamuru amani kwa ajili yetu,

yale yote tuliyoweza kuyakamilisha ni wewe uliyetenda kwa ajili yetu.

26:13 Za 66:12; Isa 42:8; 2:8; 63:7Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametutawala,

lakini jina lako pekee ndilo tunaloliheshimu.

26:14 Kum 4:28; Za 9:5; Isa 10:3; Ay 28:5Wao sasa wamekufa, wala hawako tena hai,

roho za waliokufa hazitarudi tena.

Uliwaadhibu na kuwaangamiza,

umefuta kumbukumbu lao lote.

26:15 Isa 33:17; 14:2; Ay 12:23Umeliongeza hilo taifa, Ee Bwana,

umeliongeza hilo taifa.

Umejipatia utukufu kwa ajili yako mwenyewe,

umepanua mipaka yote ya nchi.

26:16 Amu 6:2; Hos 5:15; Isa 5:30; Za 39:11; Isa 29:4Bwana, walikujia katika taabu yao,

wewe ulipowarudi,

waliweza kuomba kwa kunongʼona tu.

26:17 Isa 21:3; Ufu 12:2; Yn 16:21Kama mwanamke mwenye mimba aliyekaribia kuzaa

anavyogaagaa na kulia kwa ajili ya maumivu yake,

ndivyo tulivyokuwa mbele zako, Ee Bwana.

26:18 Isa 59:4; Mwa 49:10; Za 17:14; Isa 42:6; 49:6; 51:4; Yer 12:16Tulikuwa na mimba, tuligaagaa kwa maumivu,

lakini tulizaa upepo.

Hatukuleta wokovu duniani,

hatujazaa watu katika ulimwengu huu.

26:19 Hos 13:14; Efe 5:14; Isa 25:8; Eze 37:1-14; Dan 12:2; Isa 18:4; Mwa 27:28; Za 22:29Lakini wafu wenu wataishi,

nayo miili yao itafufuka.

Ninyi mnaokaa katika mavumbi,

amkeni mkapige kelele kwa furaha.

Umande wenu ni kama umande wa asubuhi,

dunia itawazaa wafu wake.

26:20 Kut 12:23; Za 30:5; Ay 14:13; 2Kor 4:17; Isa 10:25; 30:27Nendeni, watu wangu, ingieni vyumbani mwenu

na mfunge milango nyuma yenu,

jificheni kwa kitambo kidogo

mpaka ghadhabu yake ipite.

26:21 Yud 14; Mik 1:3; Ay 16:18; Isa 29:6; 18:4; Lk 11:50-51; Isa 30:12-14Tazama, Bwana anakuja kutoka makao yake

ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao.

Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake,

wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.

Read More of Isaya 26