Isaya 24 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 24:1-23

Dunia Kuharibiwa Upesi

124:1 Isa 2:19-21; Yer 25:29; Yos 6:17; Isa 13:5; 33:9; Mwa 11:9Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa

na kuiharibu,

naye atauharibu uso wake

na kutawanya wakaao ndani yake:

224:2 Eze 7:12; Hos 4:9; 1Kor 7:29-31; Law 25:35-37; Kum 23:19-20; Law 25:35-37; Isa 3:1-7ndivyo itakavyokuwa

kwa makuhani na kwa watu,

kwa bwana na kwa mtumishi,

kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike,

kwa muuzaji na kwa mnunuzi,

kwa mkopaji na kwa mkopeshaji,

kwa mdaiwa na kwa mdai.

324:3 Isa 6:11-12; 10:6; 7:7; Mwa 6:13Dunia itaharibiwa kabisa

na kutekwa nyara kabisa.

Bwana amesema neno hili.

424:4 Yos 12:11; Yer 14:4; Isa 15:6; 1Sam 2:12; Yoe 1:10Dunia inakauka na kunyauka,

dunia inanyongʼonyea na kunyauka,

waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea.

524:5 Mwa 3:17; Hes 35:33; Law 18:25; Isa 59:12; 9:17; Yer 7:28; 11:10; Mwa 9:11Dunia imetiwa unajisi na watu wake;

wameacha kutii sheria,

wamevunja amri

na kuvunja agano la milele.

624:6 Yer 50:15; Isa 20:624:6 Kum 28:15; Law 26:15; Dan 9:11; Yos 23:15Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia,

watu wake lazima waichukue hatia yao.

Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa,

nao waliosalia ni wachache sana.

724:7 Isa 32:10; 7:23; Yoe 1:10-12; Isa 16:8-10Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka,

watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.

824:8 Mwa 31:27; Isa 5:14; Mao 5:14; Eze 26:13; Yer 7:34; 16:9; Ufu 5:14Furaha ya matoazi imekoma,

kelele za wenye furaha zimekoma,

shangwe za kinubi zimenyamaza.

924:9 Isa 5:11, 20-22Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo,

kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.

1024:10 Isa 25:2; 26:5; 6:11Mji ulioharibiwa umekuwa ukiwa,

mlango wa kila nyumba umefungwa.

1124:11 Isa 15:6; 16:10; 32:13; Yer 14:3; Za 144:14; Mao 2:12Barabarani wanalilia kupata mvinyo,

furaha yote imegeuka kuwa majonzi,

furaha yote imefukuziwa mbali na dunia.

1224:12 Isa 19:18; 3:26; 13:2Mji umeachwa katika uharibifu,

lango lake limevunjwa vipande.

1324:13 Kum 30:4; Isa 17:6; Mik 7:1Ndivyo itakavyokuwa duniani

na miongoni mwa mataifa,

kama vile wakati mzeituni upigwavyo,

au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa.

1424:14 Isa 12:6; 43:5; 49:12Wanainua sauti zao, wanapiga kelele kwa furaha,

kutoka magharibi wanasifu kwa ukelele utukufu wa Bwana.

1524:15 Isa 45:12; 2The 1:12; Mal 1:11; Kut 15:2; Za 113:3; Isa 25:3; 12:4; 59:19Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu,

liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli,

katika visiwa vya bahari.

1624:16 Isa 28:5; Yer 3:20; 9:2; 10:19; Za 48:10; Hos 5:7; Ezr 9:15; 1Sam 4:8Kutoka miisho ya dunia tunasikia uimbaji:

“Utukufu kwa Yule Mwenye Haki.”

Lakini nilisema, “Ninadhoofika, ninadhoofika!

Ole wangu!

Watenda hila wanasaliti!

Kwa hila watenda hila wanasaliti!”

1724:17 Isa 8:14; Yer 48:43; Amo 5:19; Kum 32:23-25; Lk 21:35Hofu, shimo na mtego vinakungojea,

ewe mtu ukaaye duniani.

1824:18 Mwa 7:11; Amu 5:4; Ay 18:19; 20:24; Za 18:7; Isa 42:22; Mao 3:47; Eze 38:15Kila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu

atatumbukia shimoni,

naye yeyote apandaye kutoka shimoni,

atanaswa kwenye mtego.

Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa,

misingi ya dunia inatikisika.

1924:19 Yer 4:23; Kum 11:6; Za 46:2Dunia imepasuka,

dunia imechanika,

dunia imetikiswa kabisa.

2024:20 Ay 12:15; 27:18; Isa 1:2, 28; 19:14; 43:27; Za 46:2; Isa 58:1; Ay 12:14, 25Dunia inapepesuka kama mlevi,

inayumbayumba kama kibanda kwenye upepo;

imelemewa sana na mzigo wa hatia ya uasi wake

na ikianguka kamwe haitainuka tena.

2124:21 Isa 13:11; 2:11; Yer 25:29; Za 76:12; Isa 10:20; Ufu 16:14; 1Kor 6:3; Efe 6:12Katika siku ile Bwana ataadhibu

nguvu zilizoko mbinguni juu,

na wafalme walioko duniani chini.

2224:22 Isa 42:7, 22; Lk 8:31; Eze 38:8; Isa 10:4; Ufu 20:7-10Watakusanywa pamoja

kama wafungwa waliofungwa gerezani,

watafungiwa gerezani

na kuadhibiwa baada ya siku nyingi.

2324:23 Za 97:1; Ufu 22:5; Ebr 12:22; Ufu 21:23; Isa 13:10; 28:5; 41:16Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa;

kwa maana Bwana Mwenye Nguvu Zote atawala

juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu,

tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.