Habakuki 1:1-17, Habakuki 2:1-20, Habakuki 3:1-19 NEN

Habakuki 1:1-17

1:1 Nah 1:1Neno alilopokea nabii Habakuki.

Lalamiko La Habakuki

1:2 Za 13:1-2; 22:1-2; 6:3; 27:7; Yer 14:9Ee Bwana, hata lini nitakuomba msaada,

lakini wewe husikilizi?

Au kukulilia, “Udhalimu!”

Lakini hutaki kuokoa?

1:3 Ay 9:23; Yer 20:8; Za 55:9Kwa nini unanifanya nitazame dhuluma?

Kwa nini unavumilia makosa?

Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu;

kuna mabishano na mapambano kwa wingi.

1:4 Ay 12:6; Za 12:8; 58:2Kwa hiyo sheria imepotoshwa,

nayo haki haipo kabisa.

Waovu wanawazunguka wenye haki,

kwa hiyo haki imepotoshwa.

Jibu La Bwana

“Yatazame mataifa,

uangalie na ushangae kabisa.

Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu

ambacho hungeamini,

hata kama ungeambiwa.

Nitawainua Wakaldayo,

watu hao wakatili na wenye haraka,

ambao hupita dunia yote

kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe.

Ni watu wanoogopwa na wanaotisha;

wenyewe ndio sheria yao,

na huinua heshima yao wenyewe.

Farasi wao ni wepesi kuliko chui,

na wakali kuliko mbwa mwitu wakati wa machweo.

Askari wapanda farasi wao huenda mbio;

waendesha farasi wao wanatoka mbali.

Wanaruka kasi kama tai ili kurarua;

1:9 Hab 2:5wote wanakuja tayari kwa fujo.

Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele

kama upepo wa jangwani,

na kukusanya wafungwa

kama mchanga.

1:10 2Nya 36:6; Yer 33:4Wanawabeza wafalme,

na kuwadhihaki watawala.

Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma;

wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.

1:11 Yer 4:11-12; Dan 4:30Kisha wanapita kasi kama upepo na kusonga mbele:

watu wenye hatia, ambao nguvu zao ndio mungu wao.”

Lalamiko La Pili La Habakuki

1:12 Mwa 21:33; Isa 31:1; 37:23; Kut 33:22; Isa 10:6; Mwa 49:24; Za 118:17Ee Bwana, je, wewe sio wa tangu milele?

Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa.

Ee Bwana, umewachagua wao ili watekeleze hukumu;

Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu.

1:13 Za 18:26; Mao 3:34-36; Za 25:3; Ay 21:7Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu,

wala huwezi kuvumilia makosa.

Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu?

Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu

wanawameza wale wenye haki

kuliko wao wenyewe?

Umewafanya watu kama samaki baharini,

kama viumbe wa bahari wasio na mtawala.

1:15 Yer 5:26; Isa 19:8; Ay 18:8; Yer 16:16Adui mwovu anawavuta wote kwa ndoana,

anawakamata katika wavu wake,

anawakusanya katika juya lake;

kwa hiyo anashangilia na anafurahi.

1:16 Yer 44:8Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake,

na kuchoma uvumba kwa juya lake,

kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe,

na anafurahia chakula kizuri.

1:17 Isa 14:6; 19:8Je, aendelee kuwatoa walio katika wavu wake,

akiangamiza mataifa bila huruma?

Read More of Habakuki 1

Habakuki 2:1-20

2:1 Isa 21:8; Za 48:13; 85:8; Eze 3:17; Za 73:16, 17; 5:3Nitasimama katika zamu yangu,

na kujiweka mwenyewe juu ya maboma;

nitatazama nione atakaloniambia,

na ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili.

Jibu La Bwana

2:2 Isa 8:1; 30:8; Kum 27:8; Rum 4:24; 15:4; Yer 36:2; Eze 24:2; Ufu 1:19Kisha Bwana akajibu:

“Andika ufunuo huu,

na ukaufanye wazi juu ya vibao,

ili mpiga mbiu akimbie nao.

2:3 Dan 10:14; 11:27; 8:17; Za 27:14; Eze 12:25Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika;

unazungumzia mambo ya mwisho,

na kamwe hautakosea.

Iwapo utakawia, wewe usubiri;

kwa hakika utakuja na hautachelewa.

2:4 Eze 18:9; Yn 3:36; 2Kor 5:7; Rum 1:17; Gal 3:11; Ebr 10:37-38“Tazama, amejaa majivuno;

anavyovitamani si vya unyofu:

lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake:

2:5 Mit 20:1; Isa 2:11; Mit 27:20; 30:15-16; Hab 1:9hakika mvinyo humsaliti;

ni mwenye kiburi na hana amani.

Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu

na kama kifo kamwe hatosheki;

anajikusanyia mataifa yote

na kuchukua watu wote mateka.

2:6 Isa 14:4; Amo 2:8“Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema,

“ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa

na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu!

Ataendelea hivi kwa muda gani?’

2:7 Mit 29:1Je, wadai wako hawatainuka ghafula?

Je, hawataamka na kukufanya utetemeke?

Kisha utakuwa mhanga kwao.

2:8 Zek 1:122:8 Isa 33:1; Yer 50:17-18; Oba 1:15; Zek 2:8-9; Eze 39:10Kwa kuwa umeteka nyara mataifa mengi,

watu waliobaki watakuteka nyara wewe.

Kwa kuwa umemwaga damu ya mtu;

umeharibu nchi na miji, na kila mmoja ndani yake.

2:9 Yer 22:13; 51:13; Ay 39:27; Isa 10:14“Ole wake yeye ajengaye milki yake kwa mapato ya udhalimu,

awekaye kiota chake juu,

ili kukimbia makucha ya uharibifu!

2:10 Yer 26:19; Nah 3:6Umefanya shauri la maangamizi ya watu wengi,

ukiaibisha nyumba yako mwenyewe, na kupotewa na maisha yako.

2:11 Yos 24:27; Zek 5:4; Lk 19:40Mawe ya kuta yatapiga kelele,

na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake.

2:12 Eze 22:2; Mik 3:10“Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga

damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!

2:13 Isa 50:11; 47:13Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha

kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto,

na kwamba mataifa

yanajichosha bure?

2:14 Kut 16:7; Hes 14:21; Isa 11:9Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana,

kama maji yaifunikavyo bahari.

2:15 Mit 23:20“Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo,

akiimimina kutoka kwenye kiriba

cha mvinyo mpaka wamelewa,

ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.

2:16 Eze 23:32-34; Hos 4:7; Law 10:9; Mao 4:21; Za 16:5; Isa 51:22Utajazwa na aibu badala ya utukufu.

Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue!

Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa Bwana kinakujia,

na aibu itafunika utukufu wako.

2:17 Yer 50:33; 51:35; 50:15Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika,

na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha.

Kwa sababu umemwaga damu ya mtu;

umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.

2:18 1Sam 12:21; Amu 10:14; Isa 40:19; Yer 5:21; 14:22; 10:14; 1Kor 12:2“Sanamu ina thamani gani,

kwani mwanadamu ndiye alichonga?

Ama kinyago kinachofundisha uongo?

Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza

hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe;

hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.

2:19 1Fal 18:27; Yer 10:4; Hos 4:12; Dan 5:4, 23Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’

Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’

Je, linaweza kuongoza?

Limefunikwa kwa dhahabu na fedha;

hakuna pumzi ndani yake.

2:20 Za 11:4; Isa 41:1Lakini Bwana yuko katika Hekalu lake takatifu;

dunia yote na inyamaze mbele yake.”

Read More of Habakuki 2

Habakuki 3:1-19

Maombi Ya Habakuki

Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi.3:1 Ni kifaa cha uimbaji chenye nyuzi; pia maombi kutumia kifaa hiki.

3:2 Ay 26:14; Za 119:120; 90:16; 44:1; 85:6; Isa 54:8Bwana, nimezisikia sifa zako;

nami naogopa kwa matendo yako, Ee Bwana.

Fufua kazi yako katikati ya miaka,

katikati ya miaka tangaza habari yako;

katika ghadhabu kumbuka rehema.

3:3 Mwa 36:11, 15; Isa 31:1; Hes 10:12; Za 48:10Mungu alitoka Temani,

yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani.

Utukufu wake ulifunika mbingu,

na sifa zake zikaifunika dunia.

3:4 Isa 18:4; Ay 9:6Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo;

mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake,

ambako nguvu zake zilifichwa.

3:5 Law 26:25Tauni ilimtangulia;

maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.

3:6 Za 46:2; 114:1-6; 18:7; Kut 19:18; 23:31; Kum 32:8; Hes 21:24, 34; Mwa 49:26; 21:33Alisimama, akaitikisa dunia;

alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke.

Milima ya zamani iligeuka mavumbi

na vilima vilivyozeeka vikaanguka.

Njia zake ni za milele.

3:7 Mwa 25:2; Hes 25:15; Amu 7:24-25; Kut 15:14Niliona watu wa Kushani katika dhiki,

na makazi ya Midiani katika maumivu makali.

3:8 Kut 7:20; 14:21, 22; 2Fal 2:11; Za 77:16; 68:17Ee Bwana, uliikasirikia mito?

Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito?

Je, ulighadhibikia bahari

ulipoendesha farasi wako

na magari yako ya ushindi?

3:9 Kum 32:23; Za 7:12-13Uliufunua upinde wako

na kuita mishale mingi.

Uliigawa dunia kwa mito;

3:10 Za 77:16; 98:7; 93:3milima ilikuona ikatetemeka.

Mafuriko ya maji yakapita huko;

vilindi vilinguruma

na kuinua mawimbi yake juu.

3:11 Yos 10:13; Za 18:14; 144:6; Zek 9:14Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni

katika mngʼao wa mishale yako inayoruka,

na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.

3:12 Za 44:2, 3; Mik 4:13; Isa 41:15Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia,

na katika hasira ulikanyaga mataifa.

3:13 Kut 13:21; Za 20:6; 28:8; 68:21; 2Sam 5:20; 23:1Ulikuja kuwaokoa watu wako,

kumwokoa uliyemtia mafuta.

Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu,

ukamvua toka kichwani hadi wayo.

3:14 Amu 7:22; Za 64:2-5Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake

wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya,

wakifurahi kama walio karibu kutafuna

wale wanyonge waliokuwa mafichoni.

3:15 Ay 9:8; Kut 15:8Ulikanyaga bahari kwa farasi wako,

ukisukasuka maji makuu.

3:16 Ay 4:14; Za 37:7Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu,

midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti;

uchakavu ukanyemelea mifupa yangu,

na miguu yangu ikatetemeka.

Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa

kuyajilia mataifa yaliyotuvamia.

3:17 Yoe 1:10-18; 2Kor 4:8, 9; Yer 5:17Ingawa mtini hauchanui maua

na hakuna zabibu juu ya mizabibu,

ingawaje mzeituni hauzai,

na hata mashamba hayatoi chakula,

iwapo hakuna kondoo katika banda,

wala ngʼombe katika zizi,

3:18 Za 42:5; 97:12; Isa 61:10; Kut 15:2; Lk 1:47; Flp 4:4hata hivyo nitashangilia katika Bwana,

nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

3:19 Kum 32:13; 33:29; Za 27:1; 46:1-5; 18:33Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu;

huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala,

huniwezesha kupita juu ya vilima.

Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.

Read More of Habakuki 3