Maombi Ya Habakuki
1Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi.3:1 Ni kifaa cha uimbaji chenye nyuzi; pia maombi kutumia kifaa hiki.
23:2 Ay 26:14; Za 119:120; 90:16; 44:1; 85:6; Isa 54:8Bwana, nimezisikia sifa zako;
nami naogopa kwa matendo yako, Ee Bwana.
Fufua kazi yako katikati ya miaka,
katikati ya miaka tangaza habari yako;
katika ghadhabu kumbuka rehema.
33:3 Mwa 36:11, 15; Isa 31:1; Hes 10:12; Za 48:10Mungu alitoka Temani,
yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani.
Utukufu wake ulifunika mbingu,
na sifa zake zikaifunika dunia.
43:4 Isa 18:4; Ay 9:6Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo;
mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake,
ambako nguvu zake zilifichwa.
53:5 Law 26:25Tauni ilimtangulia;
maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.
63:6 Za 46:2; 114:1-6; 18:7; Kut 19:18; 23:31; Kum 32:8; Hes 21:24, 34; Mwa 49:26; 21:33Alisimama, akaitikisa dunia;
alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke.
Milima ya zamani iligeuka mavumbi
na vilima vilivyozeeka vikaanguka.
Njia zake ni za milele.
73:7 Mwa 25:2; Hes 25:15; Amu 7:24-25; Kut 15:14Niliona watu wa Kushani katika dhiki,
na makazi ya Midiani katika maumivu makali.
83:8 Kut 7:20; 14:21, 22; 2Fal 2:11; Za 77:16; 68:17Ee Bwana, uliikasirikia mito?
Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito?
Je, ulighadhibikia bahari
ulipoendesha farasi wako
na magari yako ya ushindi?
93:9 Kum 32:23; Za 7:12-13Uliufunua upinde wako
na kuita mishale mingi.
Uliigawa dunia kwa mito;
103:10 Za 77:16; 98:7; 93:3milima ilikuona ikatetemeka.
Mafuriko ya maji yakapita huko;
vilindi vilinguruma
na kuinua mawimbi yake juu.
113:11 Yos 10:13; Za 18:14; 144:6; Zek 9:14Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni
katika mngʼao wa mishale yako inayoruka,
na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.
123:12 Za 44:2, 3; Mik 4:13; Isa 41:15Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia,
na katika hasira ulikanyaga mataifa.
133:13 Kut 13:21; Za 20:6; 28:8; 68:21; 2Sam 5:20; 23:1Ulikuja kuwaokoa watu wako,
kumwokoa uliyemtia mafuta.
Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu,
ukamvua toka kichwani hadi wayo.
143:14 Amu 7:22; Za 64:2-5Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake
wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya,
wakifurahi kama walio karibu kutafuna
wale wanyonge waliokuwa mafichoni.
153:15 Ay 9:8; Kut 15:8Ulikanyaga bahari kwa farasi wako,
ukisukasuka maji makuu.
163:16 Ay 4:14; Za 37:7Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu,
midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti;
uchakavu ukanyemelea mifupa yangu,
na miguu yangu ikatetemeka.
Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa
kuyajilia mataifa yaliyotuvamia.
173:17 Yoe 1:10-18; 2Kor 4:8, 9; Yer 5:17Ingawa mtini hauchanui maua
na hakuna zabibu juu ya mizabibu,
ingawaje mzeituni hauzai,
na hata mashamba hayatoi chakula,
iwapo hakuna kondoo katika banda,
wala ngʼombe katika zizi,
183:18 Za 42:5; 97:12; Isa 61:10; Kut 15:2; Lk 1:47; Flp 4:4hata hivyo nitashangilia katika Bwana,
nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.
193:19 Kum 32:13; 33:29; Za 27:1; 46:1-5; 18:33Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu;
huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala,
huniwezesha kupita juu ya vilima.
Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.