Kutoka 39:1-43, Kutoka 40:1-38 NEN

Kutoka 39:1-43

Mavazi Ya Kikuhani

(Kutoka 28:1-14)

39:1 Kut 35:19-23; 28:2; Za 93:5; Eze 43Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Aroni mavazi matakatifu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Kisibau

39:2 Kut 28:6; Law 8:7Akatengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kitani iliyosokotwa vizuri. Akafua vipande vyembamba vya dhahabu kwa nyundo na kutengeneza nyuzi nyembamba ili kuzifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi, kazi ya fundi stadi. 39:4 Law 24:7; Yos 4:7Akatengeneza vipande vya mabegani vya kisibau, vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kukifungia kisibau. 39:5 Isa 11:5; Ufu 1:13Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

39:6 Kut 28:9; Ay 28:16; Isa 49:16; Ufu 1:17Akatengeneza vito vya shohamu vilivyowekwa katika vijalizo vya dhahabu, navyo vilichorwa na majina ya wana wa Israeli kama vile muhuri huchorwa. 39:7 Law 24:7; Yos 4:7; Kut 28:12; Yos 4:7; Neh 2:20Kisha akavifungia kwenye vipande vya mabega ya kisibau kuwa vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Kifuko Cha Kifuani

(Kutoka 28:15-30)

39:8 Law 8:8; Kut 28:15; Isa 59:17Akafanyiza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. Kifuko hicho kilikuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja39:9 Shibiri moja ni sawa na sentimita 22. na upana wa shibiri moja, nacho kilikunjwa mara mbili. 39:10 Kut 28:17; Eze 28:13; Ufu 21:19, 20; Isa 54:12Kifuko hicho kilipambwa kwa safu nne za vito vya thamani. Safu ya kwanza ilikuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 39:11 Ufu 4:3; Isa 54:11; Yer 17:1safu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; safu ya tatu ilikuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 39:13 Dan 10:6; Ay 28:16; Ufu 21:11katika safu ya nne ilikuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Vito hivyo vilitiwa kwenye vijalizo vya dhahabu. 39:14 Ufu 21:12Palikuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kikiwa na jina mojawapo la wana wa Israeli; kila kimoja kilichorwa kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.

Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani akakitengenezea mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. Akatengeneza vijalizo viwili vya dhahabu na pete mbili za dhahabu, na kuzifungia pete hizo kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. Akafunga hiyo mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, nazo zile ncha nyingine za mkufu akazifunga kwenye vile vijalizo viwili, na kuzishikamanisha na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuzishikamanisha kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. Kisha akatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuzishikamanisha sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. Akafunga pete za hicho kifuko cha kifuani kwenye pete za kisibau kwa kamba ya buluu, wakiziunganisha na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Mavazi Mengine Ya Kikuhani

(Kutoka 28:31-43)

39:22 Kut 28:31; Law 8:7; 1Sam 2:18; 2Sam 6:14Akashona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, kazi ya mfumaji, na lilikuwa na nafasi ya shingo katikati ya joho lile iliyofanana na ukosi, na utepe ulioshonwa kuizunguka nafasi hiyo ili isichanike. Akatengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na ya kitani iliyosokotwa vizuri kuzunguka pindo la hilo joho. 39:25 Kut 28:33Kisha akatengeneza vikengele vya dhahabu safi na kuvishikamanisha kuzunguka pindo hilo kati ya hayo makomamanga. Hivyo vikengele na makomamanga vilipishana kuzunguka upindo wa joho ili livaliwe kwa kuhudumu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

39:27 Kut 28:39, 40; 39:27; Law 8:13; Kut 28:4; Isa 61:10; Rum 3:22; Gal 3:27Pia akamtengenezea Aroni na wanawe makoti ya kitani safi, kazi ya mfumaji, 39:28 Law 6:10; 8:2; Kut 28:39, 42; Eze 44:17, 18na kilemba cha kitani safi, tepe za kichwani za kitani, na nguo za ndani za kitani iliyosokotwa vizuri. Mshipi ulikuwa wa kitani iliyosokotwa vizuri ya rangi ya buluu, na zambarau, na nyekundu, kazi ya mtarizi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

39:30 Isa 23:18; Zek 14:20; Za 93:5; Isa 23:18Kisha akatengeneza lile bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana. Kisha wakalifunga kwa kamba ya rangi ya buluu ili kulishikamanisha na kile kilemba kama Bwana alivyomwagiza Mose.

Mose Akagua Maskani Ya Mungu

(Kutoka 35:10-19)

39:32 Kut 25:9; 25:40Kwa hiyo kazi yote ya maskani, Hema la Kukutania ikakamilika. Waisraeli wakafanya kila kitu sawasawa kama vile Bwana alivyomwagiza Mose. 39:33 Kut 25:8-40; 36:10-16; Ebr 9:1-28Ndipo wakaleta maskani kwa Mose: hema pamoja na vifaa vyake vyote, vibanio vyake, mihimili yake, mataruma yake, nguzo na vitako vyake; kifuniko cha ngozi za kondoo dume kilichotiwa rangi nyekundu, kifuniko cha ngozi za pomboo,39:34 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. pazia la kufunikia; 39:35 Kut 30:6; 37:1Sanduku la Ushuhuda pamoja na mipiko yake na kiti cha rehema, 39:36 Kut 25:23-30; 37:10-16meza pamoja na vyombo vyake vyote na mikate ya Wonyesho; 39:37 Kut 25:31-39; 25:6; Ufu 1:13-20; Mt 5:14; Flp 2:15kinara cha taa cha dhahabu safi, safu zake za taa pamoja na vifaa vyake vyote pamoja na mafuta kwa ajili ya taa; 39:38 Kut 31:1-10; 37:25-28; 30:22-32; 37:29; 30:34-38; 36:35madhabahu ya dhahabu, mafuta ya upako, uvumba wenye harufu nzuri na pazia la ingilio la hema; 39:39 Kut 37:1-8; 38:1-7; 30:18madhabahu ya shaba, pamoja na wavu wa shaba, nguzo zake na vyombo vyake vyote, sinia, na tako lake; 39:40 Kut 27:9-19; 38:9-20; Ufu 3:12mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania; na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.

39:42 Kut 25:9Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose. 39:43 Kut 25:9; 35:10; Mwa 31:55; Law 9:22-23; Hes 6:23-27; Kum 26:15; 2Sam 6:18; 1Fal 8:14, 55; 1Nya 16:2; 2Nya 30:27Mose akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Mose akawabariki.

Read More of Kutoka 39

Kutoka 40:1-38

Kuweka Wakfu Maskani Ya Mungu

Kisha Bwana akamwambia Mose: 40:2 Kut 26:30; Law 3:2; 6:26; 9:23; 16:16; Hes 7:89; 11:16; 17:4; 20:6; Yos 18:1; 19:51; Yer 7:12; Kut 12:2; Hes 9:1“Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. 40:3 Kut 26; 33; Hes 4:5Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake. 40:4 Kut 25:23; 25:30-31; 26:33Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake. 40:5 Kut 30:1Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la Maskani ya Mungu.

40:6 Kut 27:1; 2Fal 16:14; 2Nya 4:1“Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania; 40:7 Kut 30:18weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake. 40:8 Kut 27:9Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua.

40:9 Kut 30:26; Hes 7:1; Law 8:10“Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu. 40:10 Kut 29; 36Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana. Paka sinia mafuta pamoja na kishikilio chake na uviweke wakfu.

40:12 Hes 8:9; Kut 29:4; 30:19“Mlete Aroni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 40:13 Kut 28:41; Law 8:1-12Kisha mvike Aroni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani. 40:14 Kut 28:40; Law 10:5Walete wanawe na uwavike makoti. 40:15 Kut 29:9; Hes 25:13Kisha watie mafuta kama ulivyomtia baba yao, ili nao pia wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutiwa mafuta kwao kutakuwa kwa ajili ya ukuhani utakaoendelea kwa vizazi vyote vijavyo.” 40:16 Mwa 6:22Mose akafanya kila kitu sawa kama vile Bwana alivyomwagiza.

40:17 Hes 7:10Kwa hiyo Maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili. 40:18 2Nya 1:3; Kut 36:20-34Mose alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo. 40:19 Kut 36:19; Mwa 6:22Kisha akalitandaza hema juu ya Maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama Bwana alivyomwagiza.

40:20 Kut 16:34; Ebr 9:4; 1Fal 8:9; Kut 25:17-22; 26:34; 31:7Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. 40:21 Kut 26:33; Mwa 6:22Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Bwana alivyomwagiza.

40:22 Kut 25:23Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia 40:23 Kut 25:30; Law 24:5-8; Mwa 6:22na kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

40:24 Kut 25:31; 26:35Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu 40:25 Kut 25:37; 37:23; Mwa 6:22na kuziweka taa mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

40:26 Kut 30:1Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia 40:27 Mwa 6:22; Kut 30:7na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama Bwana alivyomwagiza. 40:28 Kut 26:36Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu.

40:29 Kut 20:24; 29:38-42; Mwa 6:22Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama Bwana alivyomwagiza.

40:30 Kut 30:18Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, 40:31 Kut 30:19-21Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. 40:32 Kut 30:20; Mwa 6:22Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama Bwana alivyomwagiza Mose.

40:33 Kut 27:9; 38:9-20; 27:16Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi.

Utukufu Wa Bwana

(Hesabu 9:15-23)

40:34 Kut 19:16; 16:7; Law 16:2; Hes 9:15-23; 1Fal 8:12; 2Nya 5:13; Isa 6:4; Eze 10:4; Kut 19:16; 23; 2Nya 5:13; Yn 1:14; 12:41; Ufu 15:8Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu. 40:35 Kut 16:10; 1Fal 8:11; 2Nya 5:13-14; 7:2Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu.

40:36 Hes 9:17-23; 10:13; Neh 9:19Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya Maskani ya Mungu, wangeondoka; lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, mpaka siku lilipoinuka. 40:38 Hes 9:15; Kut 13:21; 1Kor 10:1Kwa hiyo wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.

Read More of Kutoka 40