Kutoka 40 – Kiswahili Contemporary Version NEN

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 40:1-38

Kuweka Wakfu Maskani Ya Mungu

1Kisha Bwana akamwambia Mose: 240:2 Kut 26:30; Law 3:2; 6:26; 9:23; 16:16; Hes 7:89; 11:16; 17:4; 20:6; Yos 18:1; 19:51; Yer 7:12; Kut 12:2; Hes 9:1“Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. 340:3 Kut 26; 33; Hes 4:5Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake. 440:4 Kut 25:23; 25:30-31; 26:33Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake. 540:5 Kut 30:1Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la Maskani ya Mungu.

640:6 Kut 27:1; 2Fal 16:14; 2Nya 4:1“Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania; 740:7 Kut 30:18weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake. 840:8 Kut 27:9Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua.

940:9 Kut 30:26; Hes 7:1; Law 8:10“Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu. 1040:10 Kut 29; 36Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana. 11Paka sinia mafuta pamoja na kishikilio chake na uviweke wakfu.

1240:12 Hes 8:9; Kut 29:4; 30:19“Mlete Aroni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 1340:13 Kut 28:41; Law 8:1-12Kisha mvike Aroni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani. 1440:14 Kut 28:40; Law 10:5Walete wanawe na uwavike makoti. 1540:15 Kut 29:9; Hes 25:13Kisha watie mafuta kama ulivyomtia baba yao, ili nao pia wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutiwa mafuta kwao kutakuwa kwa ajili ya ukuhani utakaoendelea kwa vizazi vyote vijavyo.” 1640:16 Mwa 6:22Mose akafanya kila kitu sawa kama vile Bwana alivyomwagiza.

1740:17 Hes 7:10Kwa hiyo Maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili. 1840:18 2Nya 1:3; Kut 36:20-34Mose alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo. 1940:19 Kut 36:19; Mwa 6:22Kisha akalitandaza hema juu ya Maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama Bwana alivyomwagiza.

2040:20 Kut 16:34; Ebr 9:4; 1Fal 8:9; Kut 25:17-22; 26:34; 31:7Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. 2140:21 Kut 26:33; Mwa 6:22Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Bwana alivyomwagiza.

2240:22 Kut 25:23Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia 2340:23 Kut 25:30; Law 24:5-8; Mwa 6:22na kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

2440:24 Kut 25:31; 26:35Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu 2540:25 Kut 25:37; 37:23; Mwa 6:22na kuziweka taa mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza.

2640:26 Kut 30:1Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia 2740:27 Mwa 6:22; Kut 30:7na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama Bwana alivyomwagiza. 2840:28 Kut 26:36Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu.

2940:29 Kut 20:24; 29:38-42; Mwa 6:22Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama Bwana alivyomwagiza.

3040:30 Kut 30:18Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, 3140:31 Kut 30:19-21Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. 3240:32 Kut 30:20; Mwa 6:22Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama Bwana alivyomwagiza Mose.

3340:33 Kut 27:9; 38:9-20; 27:16Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi.

Utukufu Wa Bwana

(Hesabu 9:15-23)

3440:34 Kut 19:16; 16:7; Law 16:2; Hes 9:15-23; 1Fal 8:12; 2Nya 5:13; Isa 6:4; Eze 10:4; Kut 19:16; 23; 2Nya 5:13; Yn 1:14; 12:41; Ufu 15:8Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu. 3540:35 Kut 16:10; 1Fal 8:11; 2Nya 5:13-14; 7:2Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa Bwana ukaijaza Maskani ya Mungu.

3640:36 Hes 9:17-23; 10:13; Neh 9:19Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya Maskani ya Mungu, wangeondoka; 37lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, mpaka siku lilipoinuka. 3840:38 Hes 9:15; Kut 13:21; 1Kor 10:1Kwa hiyo wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.