Kumbukumbu 2:24-37, Kumbukumbu 3:1-29, Kumbukumbu 4:1-14 NEN

Kumbukumbu 2:24-37

2:24 Hes 21:13-14; Amu 11:13-18; Kum 1:7; 3:6“Ondoka sasa na uvuke Bonde la Arnoni. Tazama, nimemweka mikononi mwako Sihoni Mwamori, mfalme wa Heshboni na nchi yake. Anza kuimiliki nchi hiyo na umwingize katika vita. 2:25 Mwa 35:5; Kum 1:25; Yos 2:9-11; 1Nya 14:17; 2Nya 14:14; 17:10; 20:29; Isa 2:19; 13:13; 19:16; Kut 15:14-16Siku hii ya leo nitaanza kuwatia hofu na woga mataifa yote chini ya mbingu wawaogope ninyi. Watakaposikia taarifa zenu, watatetemeka na kufadhaika kwa sababu yenu.”

Kushindwa Kwa Sihoni Mfalme Wa Heshboni

(Hesabu 21:21-30)

2:26 Yos 13:18; 1Nya 6:79; Kum 1:4; Amu 1:11-22; Kum 20:10; Amu 21:13; 2Sam 20:19Kutoka jangwa la Kedemothi nilituma wajumbe wenye maneno ya amani kwa Sihoni mfalme wa Heshboni kusema, 2:27 Hes 21:21-22; Amu 11:19“Turuhusu tupite katika nchi yako. Tutapita katika barabara kuu, hatutageuka kuume wala kushoto. 2:28 Kum 23:4; Hes 20:19Tuuzie chakula tule na maji tunywe kwa thamani yake katika fedha. Turuhusu tu tupite kwa miguu, 2:29 Kum 23:3; Amu 11:17kama wazao wa Esau ambao wanaishi Seiri na Wamoabu ambao wanaishi Ari walivyotufanyia, mpaka tuvuke Yordani kuingia nchi ambayo Bwana Mungu wetu anatupatia.” 2:30 Amu 14:4; 1Fal 12:15; Kut 4:21; Rum 9:18; Kut 14:17; Yos 11:20; Hes 21:23; Mao 3:65; Yos 11:19, 20; Hos 4:17; Yak 1:13-15Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni alikataa kuturuhusu kupita. Kwa kuwa Bwana Mungu wako alikuwa ameifanya roho yake kuwa ngumu na moyo wake kuwa mkaidi ili amweke kwenye mikono yenu, kama alivyofanya sasa.

2:31 Mwa 12:7; Kum 1:8Bwana akaniambia, “Tazama, nimeanza kuwapa Mfalme Sihoni na nchi yake kwako. Sasa anzeni kuishinda na kuimiliki nchi yake.”

2:32 Hes 21:23Wakati Sihoni pamoja na jeshi lake lote walipokuja kukutana nasi katika vita huko Yahazi, 2:33 Kut 23:31; Kum 7:2; 31:5; 29:7; Hes 21:24; Za 135:10-12; 136:18-20Bwana Mungu wetu alimweka mikononi mwetu, nasi tukamwangamiza pamoja na wanawe na jeshi lake lote. 2:34 Hes 21:2; Kum 3:6; 7:2; Za 106:34; Law 27:28; Kum 7:2, 26; Yos 7:11; 8:25, 26; 9:24; 11:14; 1Sam 15:3-9Kwa wakati ule tuliteka miji yake yote na kuiangamiza kabisa: wanaume, wanawake na watoto. Hatukumwacha yeyote. 2:35 Kum 3:7; Mwa 34:29; 49:27Lakini mifugo na nyara tulizoziteka kutoka ile miji tulijichukulia wenyewe. 2:36 Hes 32:34; 32:39; Za 44:3; Yos 13:9Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde, hata mpaka Gileadi, hapakuwa na mji hata mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. Bwana Mungu wetu alitupa yote. 2:37 Hes 21:21; Mwa 32:22; Kum 3:16Lakini kulingana na amri ya Bwana Mungu wetu, hamkujiingiza katika nchi yoyote ya Waamoni, wala katika sehemu yoyote iliyo kandokando ya Mto Yaboki, wala katika miji iliyoko katika vilima.

Read More of Kumbukumbu 2

Kumbukumbu 3:1-29

Kushindwa Kwa Ogu Mfalme Wa Bashani

(Hesabu 21:31-35)

3:1 Hes 21:33; 32:19Kisha tukageuka tukakwea kufuata njia iliyoelekea Bashani, Ogu mfalme wa Bashani akaondoka na jeshi lake lote kupigana na sisi huko Edrei. 3:2 Yos 10:8; 2Fal 19:6; Isa 7:4Bwana akaniambia, “Usimwogope kwa kuwa nimekwisha mkabidhi mikononi mwako pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Umfanyie sawasawa na ulivyomfanyia Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”

3:3 Hes 21:24; 21:35Hivyo Bwana Mungu wetu pia akamweka Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote mikononi mwetu. Tuliwaangamiza wote, hakubakia hata mmoja. 3:4 Hes 21:24, 33; 1Fal 4:13Wakati huo tuliteka miji yake yote. Hakuna mji hata mmoja kati ya ile sitini ambao hatukuuteka, yaani eneo lote la Argobu, utawala wa Mfalme Ogu katika Bashani. Miji yote hii ilijengewa ngome zenye kuta ndefu zenye malango na makomeo, pia kulikuwako na vijiji vingi ambavyo havikujengewa kuta. 3:6 Kum 2:24; Za 135:10-12; 136:19-21Tuliwaangamiza kabisa, kama tulivyomfanyia Sihoni mfalme wa Heshboni, tukiangamiza kila mji, yaani wanaume, wanawake na watoto. 3:7 Kum 2:35Lakini wanyama wote wa kufuga pamoja na nyara kutoka kwenye miji yao tulichukua vikawa vyetu.

3:8 Hes 32:33; Yos 13:8-12; Kum 4:48; Yos 11:3; 12:1; 13:5; Amu 3:3; 1Nya 5:23; Za 42:6; 89:12; 133:3; Wim 4:8Hivyo kwa wakati huo tukachukua kutoka kwa wafalme hawa wawili wa Waamori nchi ya mashariki ya Yordani, kutoka Bonde la Arnoni mpaka kufika kwenye Mlima Hermoni. 3:9 Za 29:6; 89:12; 1Nya 5:23; Wim 4:8; Eze 27:5; Kum 4:48(Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, nao Waamori huuita Seniri.) 3:10 Yos 12:5; 13:11; 1Nya 5:11; Kum 4:49Tuliteka miji yote kwenye uwanda wa juu, Gileadi yote, Bashani yote mpaka kufika Saleka na Edrei, miji ya utawala wa Ogu huko Bashani. 3:11 Mwa 14:5; Yos 13:25; 15:60; 2Sam 11:1; 12:26; 17:27; 1Nya 20:7; Yer 49:2; Eze 21:20; 25:5; Amo 1:14; 2:9(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa3:11 Dhiraa tisa ni sawa na mita 4. na upana wa dhiraa nne.3:11 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.)

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani

(Hesabu 32:1-42)

3:12 Kum 2:36; Hes 32:32-38; Yos 13:8-13Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake. 3:13 Kum 29:8; Mwa 14:5Kisha nusu ya kabila la Manase niliwapa sehemu ya Gileadi iliyobaki pamoja na Bashani yote, ambayo ilikuwa utawala wa Ogu. (Eneo lote la Argobu katika Bashani lilikuwa linajulikana kama nchi ya Warefai. 3:14 Hes 32:41; Yos 12:5; 13:11-13; 2Sam 10:6; 23:34; 2Fal 25:23; 1Nya 4:19; Yer 40:8; Yos 19:46-47; Za 49:11; 1Nya 2:22Yairi, mzao wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka, ukaitwa kwa jina lake; kwa hiyo mpaka leo hii Bashani inaitwa Hawoth-Yairi.) 3:15 Mwa 50:23; Hes 32:39-40Nikampa Makiri nchi ya Gileadi. 3:16 Hes 21:24; 2Sam 24:5; Hes 21:24Lakini niliwapa Wareubeni na Wagadi eneo kuanzia Gileadi hadi Bonde la Arnoni (katikati ya bonde ulikuwa ndio mpaka), kuelekea mpaka Mto Yaboki, ambao ndio mpaka wa Waamoni. 3:17 2Sam 2:29; 4:7; Eze 47:8; Hes 34:11; 14:3; Yos 12:3; 13:27Kwa upande wa magharibi mpaka wao ulikuwa Yordani katika Araba, toka ziwa Galilaya hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), kwenye miteremko ya Pisga upande wa mashariki.

3:18 Yos 1:13; Hes 32:17Wakati huo nilikuamuru: “Bwana Mungu wako amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ngʼambo wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli. 3:19 Yos 1:14; Hes 32:16Lakini wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu (kwani najua mnayo mifugo mingi) wanaweza kukaa katika miji niliyowapa, 3:20 Yos 22:4mpaka hapo Bwana atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, ngʼambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”

Mose Akatazwa Kuvuka Yordani

Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo Bwana Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. Bwana atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo. 3:22 Kum 1:29; 7:18; 20:4; 31:6; 2Nya 32:8; Za 23:4; Isa 41:10; Kut 14:143:22 Yos 23:10Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”

3:23 Kum 1:37; 31:2; 32:52; 34:4Wakati huo nilimsihi Bwana: 3:24 Kum 5:24; 11:2; 32:3; Kut 8:10; Za 71:16; 86:8; 106:2; 145:12; 150:2; 2Sam 7:22; Neh 9:32; Yer 32:18-21; Kut 15:11“Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe? 3:25 Kum 4:25; 1:7; Yos 1:4; 9:1; 11:17; 12:7; 13:5; Amu 3:3; 9:13; 1Fal 4:33Acha niende nikaione hiyo nchi nzuri ngʼambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni.”

3:26 Kum 1:37; 31:2Lakini kwa sababu yenu Bwana alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. Bwana aliniambia, “Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena. 3:27 Hes 21:20; 27:12; Mwa 13:14; Hes 20:12; Kum 32:52Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie magharibi, kaskazini, kusini na mashariki. Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile wewe hutavuka Yordani. 3:28 Hes 27:18-23; Kum 31:7; 1:38; 31:3-23Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ngʼambo na kuwarithisha nchi utakayoiona.” 3:29 Hes 23:28; Kum 4:46; 34:6; Yos 13:20Kwa hiyo tulikaa kwenye bonde karibu na Beth-Peori.

Read More of Kumbukumbu 3

Kumbukumbu 4:1-14

Waamriwa Utii

4:1 Law 18:4-5; Kum 1:3; 30:15-20; Rum 10:5; Eze 20:11; Rum 10:5Sikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zako anawapa. 4:2 Kum 12:32; Yos 1:7; Mit 30:6; Ufu 22:18-19; Yer 26:2; Law 22:31; Kum 10:12-13; Mhu 12:13Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya Bwana Mungu wenu ambayo nawapa.

4:3 Hes 25:1-9; Za 106:28Mliona kwa macho yenu wenyewe kile Bwana alichokifanya kule Baal-Peori. Bwana Mungu wenu aliwaangamiza kutoka miongoni mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori, lakini ninyi nyote mlioshikamana na Bwana kwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo.

4:5 Za 71:17; 119:102; Yer 32:33; Kut 18:20; Law 27:34; Ezr 9:11Tazama, nimewafundisha amri na sheria kama Bwana Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki. 4:6 Kum 29:9; 1Fal 2:3; Kum 30:19-20; 32:46-47; Za 19:7; 119:98; Mit 1:7; 2:5; 2Tim 3:15; Ay 28:28; Za 111:10; Mit 3:7; 9:10; Mhu 12:13; Eze 5:5Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.” 4:7 2Sam 7:23; Hes 23:21; Za 46:1; Mdo 17:27; Kut 25:8; 29:45; Law 26:12; 1Fal 6:13; Isa 55:6; Zek 2:10; Efe 2:17; Yak 4:8Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama Bwana Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba? 4:8 Za 89:14; 97:2; 119:7, 62, 144, 160, 172; Rum 3:2Nalo ni taifa gani jingine lililo kubwa hivi lenye kuwa na amri na sheria za haki kama hizi ninazoweka mbele yenu leo?

4:9 Kut 23:13; Mwa 14:14; 18:19; Kum 6:20-25; Efe 6:4; Kut 10:2; Mit 4:23; Za 78:5-6; Mit 4:23; 23:19; 3:1, 3; 4:21; Mwa 18:19; Mit 22:6; Efe 6:4Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.

4:10 Kut 3:1; 19:9, 16; Kum 14:23; 17:19; 31:12-13; Za 2:11; 111:10; 147:11; Isa 8:13; Yer 32:40; Kut 20:20; Kum 12:1Kumbuka siku uliyosimama mbele za Bwana Mungu wako kule Horebu, wakati aliponiambia, “Wakutanishe watu mbele yangu wasikie maneno yangu ili kwamba waweze kujifunza kuniheshimu kwa muda wote watakaoishi katika nchi, nao waweze kuwafundisha watoto wao maneno hayo.” 4:11 Kut 3:1; 19:17-18; 19:9; Za 18:11; 97:2; Ebr 12:18-19Mlisogea karibu na mkasimama chini ya mlima wakati ulipowaka moto mpaka mbinguni juu, pamoja na mawingu meusi na giza nene. 4:12 Kut 20:22; Mt 3:17; Kum 5:4-20; Ebr 12:19; Yn 5:37; Kut 19:9Ndipo Bwana alipozungumza nanyi kutoka moto. Mkasikia sauti ya maneno lakini hamkuona umbo, kulikuwa na sauti tu. 4:13 Kum 9:9-11; Rum 9:4; Kut 24:12; 31:18; 4:14; 21:1Aliwatangazia Agano lake na Amri Kumi, ambazo aliwaamuru mzifuate, kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe. Naye Bwana alinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.

Read More of Kumbukumbu 4