Kutangatanga Jangwani
12:1 Kut 14:27; Hes 21:4; 24:18Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama Bwana alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka vilima katika nchi ya Seiri.
2Kisha Bwana akaniambia, 32:3 Kum 1:6“Umetembea kuzunguka hii nchi ya vilima kwa muda wa kutosha; sasa geukia kaskazini. 42:4 Hes 20:14-21; Mwa 36:8; Kut 15:16Wape watu maagizo haya: ‘Mko karibu kupita katikati ya nchi ya ndugu zako ambao ni wazao wa Esau, ambao wanaishi Seiri. Watawaogopa, lakini mwe waangalifu. 52:5 Yos 24:4; Mwa 36:8; Kum 32:8; 2Nya 20:10-12; Mdo 17:26Msiwachokoze kwa vita kwa maana sitawapa ninyi sehemu yoyote ya nchi yao, hata sehemu ya kutosha kuweka wayo wenu juu yake. Nimempa Esau nchi ya vilima ya Seiri kama yake mwenyewe. 6Mtawalipa fedha kwa chakula mtakachokula na maji mtakayokunywa.’ ”
72:7 Kum 8:2-4; Kut 13:21; Kum 1:19; Hes 14:33; 32:13; Yos 5:6; Neh 9:21; Amo 2:10Bwana Mungu wenu amewabariki kwa kazi yote ya mikono yenu. Amewalinda katika safari yenu katikati ya jangwa hili kubwa. Kwa miaka hii arobaini Bwana Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamkupungukiwa na kitu chochote.
82:8 Hes 20:8; 33:35; 1Fal 9:26; Hes 21:4Basi tulipita kwa ndugu zetu wazao wa Esau ambao wanaishi Seiri. Tuligeuka kutoka njia ya Araba ambayo inatokea Elathi na Esion-Geberi, tukasafiri kufuata njia ya jangwa la Moabu.
92:9 Hes 21:15; Mwa 19:38; Za 83:8Kisha Bwana akaniambia, “Usiwasumbue Wamoabu kwa vita, kwa kuwa sitawapa sehemu yoyote ya nchi yao. Nimetoa nchi ya Ari kwa wazao wa Loti kama milki yao.”
102:10 Mwa 14:5; Hes 13:22; 33; Kum 9:2(Waemi walikuwa wakiishi huko hapo zamani, watu wenye nguvu na wengi, warefu kama Waanaki. 112:11 Mwa 14:5Kama walivyokuwa Waanaki, hao pia walikuwa kama Warefai, lakini Wamoabu waliwaita Waemi. 122:12 Mwa 14:6; Hes 21:25-35Wahori waliishi Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafukuza. Waliwaangamiza Wahori na kukaa mahali pao, kama Waisraeli walivyofanya katika nchi ambayo Bwana aliwapa kama milki yao.)
132:13 Hes 21:12Bwana akasema, “Sasa ondokeni mvuke Bonde la Zeredi.” Hivyo tukavuka bonde.
142:14 Kum 1:2; Hes 13:26; 14:29-35; Kum 1:34-35; Yos 5:6Miaka thelathini na minane ilipita tangu wakati tulipoondoka Kadesh-Barnea mpaka tulipovuka Bonde la Zeredi. Kwa wakati huo kile kizazi chote cha wanaume kuanzia wale wawezao kwenda vitani kilikuwa kimekufa, kama Bwana alivyokuwa amewaapia. 152:15 Za 106:26; Yud 5; 1Sam 5:6-11; 7:13; Za 95:10, 11; Ebr 4:1-5Mkono wa Bwana uliwakabili hadi alipowaangamiza wote huko kambini.
16Ikawa baada ya mtu wa mwisho kuanzia wale wawezao kwenda vitani kufa, 17Bwana akaniambia, 182:18 Hes 21:15“Leo utapita katika nchi ya Moabu huko Ari. 192:19 Mwa 19:38; 2Nya 20:10Utakapokuja kwa Waamoni, msiwasumbue wala kuwachokoza kwa vita, kwa kuwa sitawapa ardhi yoyote iliyo ya Waamoni kuwa milki yenu. Nimeitoa kama milki ya wazao wa Loti.”
202:20 Mwa 14:5(Hiyo pia ilidhaniwa kuwa nchi ya Warefai waliokuwa wakiishi huko, lakini Waamoni waliwaita Wazamzumi. 21Walikuwa watu wenye nguvu na wengi, warefu kama Waanaki. Bwana akawaangamiza kutoka mbele ya Waamoni, ambao waliwafukuza na kukaa mahali pao. 222:22 Mwa 14:6; 36:8; Ay 12:23Bwana alikuwa amefanya vivyo hivyo kwa wazao wa Esau, ambao waliishi Seiri, wakati alipowaangamiza Wahori watoke mbele yao. Waliwafukuza na wao wakaishi mahali pao mpaka leo. 232:23 Yos 13:3; 18:23; 2Fal 17:31; Mwa 10:14; 19; Yer 47:4; Amo 9:7; Sef 2:4Nao Waavi ambao waliishi katika vijiji mpaka Gaza, Wakaftori waliokuja kutoka Kaftori waliwaangamiza na kukaa mahali pao.)
242:24 Hes 21:13-14; Amu 11:13-18; Kum 1:7; 3:6“Ondoka sasa na uvuke Bonde la Arnoni. Tazama, nimemweka mikononi mwako Sihoni Mwamori, mfalme wa Heshboni na nchi yake. Anza kuimiliki nchi hiyo na umwingize katika vita. 252:25 Mwa 35:5; Kum 1:25; Yos 2:9-11; 1Nya 14:17; 2Nya 14:14; 17:10; 20:29; Isa 2:19; 13:13; 19:16; Kut 15:14-16Siku hii ya leo nitaanza kuwatia hofu na woga mataifa yote chini ya mbingu wawaogope ninyi. Watakaposikia taarifa zenu, watatetemeka na kufadhaika kwa sababu yenu.”
Kushindwa Kwa Sihoni Mfalme Wa Heshboni
(Hesabu 21:21-30)
262:26 Yos 13:18; 1Nya 6:79; Kum 1:4; Amu 1:11-22; Kum 20:10; Amu 21:13; 2Sam 20:19Kutoka jangwa la Kedemothi nilituma wajumbe wenye maneno ya amani kwa Sihoni mfalme wa Heshboni kusema, 272:27 Hes 21:21-22; Amu 11:19“Turuhusu tupite katika nchi yako. Tutapita katika barabara kuu, hatutageuka kuume wala kushoto. 282:28 Kum 23:4; Hes 20:19Tuuzie chakula tule na maji tunywe kwa thamani yake katika fedha. Turuhusu tu tupite kwa miguu, 292:29 Kum 23:3; Amu 11:17kama wazao wa Esau ambao wanaishi Seiri na Wamoabu ambao wanaishi Ari walivyotufanyia, mpaka tuvuke Yordani kuingia nchi ambayo Bwana Mungu wetu anatupatia.” 302:30 Amu 14:4; 1Fal 12:15; Kut 4:21; Rum 9:18; Kut 14:17; Yos 11:20; Hes 21:23; Mao 3:65; Yos 11:19, 20; Hos 4:17; Yak 1:13-15Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni alikataa kuturuhusu kupita. Kwa kuwa Bwana Mungu wako alikuwa ameifanya roho yake kuwa ngumu na moyo wake kuwa mkaidi ili amweke kwenye mikono yenu, kama alivyofanya sasa.
312:31 Mwa 12:7; Kum 1:8Bwana akaniambia, “Tazama, nimeanza kuwapa Mfalme Sihoni na nchi yake kwako. Sasa anzeni kuishinda na kuimiliki nchi yake.”
322:32 Hes 21:23Wakati Sihoni pamoja na jeshi lake lote walipokuja kukutana nasi katika vita huko Yahazi, 332:33 Kut 23:31; Kum 7:2; 31:5; 29:7; Hes 21:24; Za 135:10-12; 136:18-20Bwana Mungu wetu alimweka mikononi mwetu, nasi tukamwangamiza pamoja na wanawe na jeshi lake lote. 342:34 Hes 21:2; Kum 3:6; 7:2; Za 106:34; Law 27:28; Kum 7:2, 26; Yos 7:11; 8:25, 26; 9:24; 11:14; 1Sam 15:3-9Kwa wakati ule tuliteka miji yake yote na kuiangamiza kabisa: wanaume, wanawake na watoto. Hatukumwacha yeyote. 352:35 Kum 3:7; Mwa 34:29; 49:27Lakini mifugo na nyara tulizoziteka kutoka ile miji tulijichukulia wenyewe. 362:36 Hes 32:34; 32:39; Za 44:3; Yos 13:9Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde, hata mpaka Gileadi, hapakuwa na mji hata mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. Bwana Mungu wetu alitupa yote. 372:37 Hes 21:21; Mwa 32:22; Kum 3:16Lakini kulingana na amri ya Bwana Mungu wetu, hamkujiingiza katika nchi yoyote ya Waamoni, wala katika sehemu yoyote iliyo kandokando ya Mto Yaboki, wala katika miji iliyoko katika vilima.