1 Wakorintho 1:18-31, 1 Wakorintho 2:1-5 NEN

1 Wakorintho 1:18-31

Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu

1:18 1Kor 2:14; 2Kor 2:15; 4:3; 2The 2:10; Mdo 2:47; Rum 1:16Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 1:19 Isa 29:14; Ay 5:12, 13; Yer 8:9Kwa maana imeandikwa:

“Nitaiharibu hekima ya wenye hekima,

na kubatilisha akili ya wenye akili.”

1:20 Isa 19:11-12; 1Kor 2:6-8; 3:18; 2Kor 4:4; Gal 1:4; Ay 12:17; Isa 44:25; Yer 8:9; Rum 1:22; 1Kor 3:18-19Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? 1:21 1Kor 6:2; 11:32; Rum 11:14; 3:22Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. 1:22 Mt 12:38; Yn 2:11; 4:48Wayahudi wanadai ishara za miujiza na Wayunani wanatafuta hekima. 1:23 1Kor 2:2; Gal 3:1; Lk 2:34Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi. 1:24 Rum 8:28; 1:16; Kol 2:3Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, Wayahudi na pia Wayunani, Kristo ndiye nguvu ya Mungu na pia hekima ya Mungu. 1:25 2Kor 13:4; 1Kor 1:18Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.

1:26 Rum 8:28; 1Kor 1:20; Yn 7:48Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. 1:27 Yak 2:5; Rum 1:22; 1Kor 3:18-19Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu. 1:28 Rum 4:17; 1Kor 2:6Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, 1:29 Efe 2:9ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. 1:30 Rum 16:3; Yer 5:5-6; 33:16; 2Kor 5:21; Flp 3:9; 1Kor 1:2; Rum 3:24Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. 1:31 Yer 9:23; Za 34:2; 44:8; 2Kor 10:17Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”

Read More of 1 Wakorintho 1

1 Wakorintho 2:1-5

Kumtangaza Kristo Aliyesulubiwa

2:1 1Kor 1:17; 2:4; 13; 2Kor 10:10; 11; 1Kor 1:6Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu. 2:2 Gal 6:14; 1Kor 1:23Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote wakati nikiwa nanyi isipokuwa Yesu Kristo aliyesulubiwa. 2:3 Mdo 18:1-18; 1Kor 4:10; 9:22; 2Kor 11:29-30; 12:5-10; 13:9; 7:15Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana. 2:4 Rum 15:13; 1Kor 2:1; 1:17; 2Pet 1:16Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.

Read More of 1 Wakorintho 2